Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Huyu Kitila analeta siasa kwenye mambo yasiyohitaji siasa. Hao wananchi anaotaka watoe maoni yao ni pamoja na hawa wa mkwajuni waliogoma kuondoka na sasa mvua zinawaathiri? Na hao wabunge ni hadi kina Lusinde? Aache mtaalamu Ndalichako afanye kazi yake.
 
Tafiti ya nini kama ile iliyotenguliwa haikuja na tafiti mujarabu si unarudi kule ulikokuwa mpaka ije tafiti nyingine ya kubadilisha hii ya DIVISHENI.

Waliulizwa siku ile mbele ya press na umma wakawa wanajiumauma tu.
Na kimsingi aliwapa siku saba wadau watoe sababu kwa nini mfumo wa GPA uliwekwa na sababu za kitaalam za mabadiliko hayo wadau wote walishindwa kutoa sababu na hivyo akarudisha kilicho halali na kuondoa haramu yao!!
 
Moja ya kitu ambacho sikubaliani na mtoa mada ni kusema Prof Ndalichako ameamua mwenyewe, hapana Ndali aliwataka walibadilisha mfumo watoe sababu za kisayansi maana mfumo wenyewe haueleweki na ulikuwa wa ghafla, baada ya waliobadilisha kushindwa kutoa sababu za kisayansi ndio akaona hauna tija, so hatua ya kwanza ni kutoa haramu ndo tuangalie mfumo unaotakiwa, kingine Ndalichako hana influence wala hana mamlaka ya kuvunja mfumo lakini kama ilikuwa haramu hakuna haja ya kubeza, anachotakiwa kuleta na SERa ya Elimu ambayo ilizinduliwa na kitila akawa anachekelea, Huyu ni msomi mchumia tumbo kama Banner tu....
 
Kwa msiokua na fikra za mbali ameshindwa kumwelewa Prof Mkumbo! Kinachozungumzwa hapa ni hakuna consistance! Kila awamu ni kubadili mfumo tu, kila waziri na lake! Kilichotakiwa hapa ni kuboresha mfumo hasa kupanfisha alama za ufaulu badala ya kuzishusha.
Tumemwelewa ndalichako zaidi kwa kuwa ameturudisha kwenye ukweli maana hapo ndipo tutaona kwa uwazi ubovu wa elimu yetu na kuanza kujipanga upya kutoka kwenye kiini cha tatizo maana tatizo si upimaji, Elimu kwa hakika imeoza na mfumo wa GPA uliochakachuliwa kwa sababu za kisiasa ili kufikia malengo ya MATOKEO MAKUBWA SASA ulitumika ili walau kuficha uozo huo kwa muda maana athari zake za uozo zimeonekana vyuoni na mtaani kwa hao waliofaulu kutokuwa na uwezo hata wa kuandika insha ya kiingereza walau kujitambulisha au hata kushindwa kujaza fomu za udahili wa chuo. Huko mtaani ndio hawana la ziada zaidi ya kuwa madereva wa bodaboda na wa dada kujisalimisha kwenye kuolewa, kukaanga vitumbua na ile biashara isiyo na utu!
Hivyo bora tujue wanafeli na tuone tutauobereshaje huo mfumo wa elimu yetu ili kuwa na matokeo chanya kwa taifa letu
 
Tunapoteza muda kubishana mambo yasiyo na msingi. Kama mwanafunzi Ana akili hata uweke mfumo gani atafaulu tu.
Hatupotezi Muda tunataka kuweka Sawa haya ili huyo mwanafunzi mwenye akili atambulike vyema na huyo mwenye akili lakini viwango vyake viko chini atambuliwe pia haina maana kuwa na mfumo wenye kutoa matokeo ya mwenye uwezo na asiye na uwezo wote waonekane na uwezo!!!
 
Hivi umekisoma alicho kiandika Kitila? ni wapi wana tofautiana na Ndalichako? Anacho hitaji Kitila ni msimamo na Debate! Muulize Kitila atupe mifano ya nchi iliyo andaa Debate ili kujadili mfumo wa elimu au upangaji matokeo!

Mimi ninachojua hapa kinacho hitajika ni utafiti wa kisayansi na sio kelele za kwenye Debate!
Tafiti zilifanyika zikaona mfumo wa division ndio unafaa na kama kuna tafiti zilifanyika kuonesha GPA ndio mfumo mzuri na pia kwa kushusha marks vile basi walitakiwa wawe wametuonesha na kueleza..! Wameshindwa kuitetea GPA ndio maana tumerudi kule tulipokuwa.

Hatuhitaji Debate kwenye mambo ya msingi bali tunahitaji tafiti!
Kila mtu anauelewa wake juu ya jambo hili,kitila anaelezea umuhimu wa kuwa na sera ya elimu katika taifa ambayo itazuia mihemko ya viongozi wetu katika maamuzi,miaka michache iliyopita tuliitangazia dunia tumetoka katika division kwenda GPA mfumo ambao mataifa mengi wanautumia, badala ya kuuboresha kiongozi anauondoa kwasababu ambazo hazina mashiko .eti anataka majibu ya kisayansi wakati ameshakamia kuundoa.viongozi wetu katika hili wameongozwa na chuki na visasi kwahiyo lazima tutafute njia ya kuweza kudhibiti haya yasitokee tena.
 
mfumo wa GPA uliwekwa na serikali ili kuficha aibu ya serikali kwa watoto kufeli....
 
Kila mtu anauelewa wake juu ya jambo hili,kitila anaelezea umuhimu wa kuwa na sera ya elimu katika taifa ambayo itazuia mihemko ya viongozi wetu katika maamuzi,miaka michache iliyopita tuliitangazia dunia tumetoka katika division kwenda GPA mfumo ambao mataifa mengi wanautumia, badala ya kuuboresha kiongozi anauondoa kwasababu ambazo hazina mashiko .eti anataka majibu ya kisayansi wakati ameshakamia kuundoa.viongozi wetu katika hili wameongozwa na chuki na visasi kwahiyo lazima tutafute njia ya kuweza kudhibiti haya yasitokee tena.
Pengine hujui kinacho endelea kuhusu huo mfumo wa GPA unao tumiwa na baraza! Baraza wameenda mbali na kushusha viwango vya ufaulu...hivi hii ndio kuboresha? Waziri aliwapa siku saba watoe sababu za kisayansi za kutumia mfumo wa GPA dhidi ya mfumo wa Division wakashindwa ulitegemea nini?
Mfumo wa GPA sio mbaya lakini mbaya kutumiwa na elimu ya chini hasa wanapo ongeza na kushusha viwango vya ufaulu!

Isitoshe kutumia marks za maendeleo kama kigezo bado ni kujidanganya kabisa maana walimu wanaweza kumjazia tuu mwanafunzi marks zozote...!
 
Sasa huyu Prof naye shida tu naye anataka kuwa profesa wa siasa. Tulikuwa na mfumo wa Division akaja mwingine akauondoa akaleta mfumo wa GPA huyu wa sasa ka-restore system, hivi ku-restore ni kufanya kitu kipya? Mimi nadhani sasa ni nafasi kwa huyu profesa kutoa maoni yake kwanini anadhani tuhame kwenye division na kwenda kwenye GPA maana kwa jinsi nilivyomsoma ni kwamba waziri wa elimu aliyeondoa division na kuleta GPA hakushrikisha wadau kwa hiyo huyu sasa ame-restore sysytem ili mtoe mawazo yenu
Sababu ya Kitila ni anaogopa kuwaambia watu kuwa tulikuwa division tukaenda GPA na sasa tumerudi tena Divion.

Namshauri Ndalichako, alielekeze baraza wale wote walipewa vyeti vya GPA wavirudishe na kupewa vya division
 
Ruta, ngoja tusubiri tuone. Utakumbuka kuwa kipindi wanaanzisha GPA serikali ilisema kwamba wameamua kutumia GPA kwa sababu ni mfumo unao tumika katika nchi nyingi duniani. Hivyo kuepuka usumbufu kwa watahiniwa wetu kufanyiwa ulinganifu wa division vs gpa wanapo taka kujiunga na elimu ya juu au kazi nje ya Tanzania.
Nchi zote walishusha marks kama walivyo fanya baraza? Tatizo kubwa hapa ni kitendo cha Necta kushusha viwango vya ufaulu...! Halafu bado hatujawa na mfumo mzuri wa kutumia GPA kupanga matokeo kwa level ya chini!...
 
Pengine hujui kinacho endelea kuhusu huo mfumo wa GPA unao tumiwa na baraza! Baraza wameenda mbali na kushusha viwango vya ufaulu...hivi hii ndio kuboresha? Waziri aliwapa siku saba watoe sababu za kisayansi za kutumia mfumo wa GPA dhidi ya mfumo wa Division wakashindwa ulitegemea nini?
Mfumo wa GPA sio mbaya lakini mbaya kutumiwa na elimu ya chini hasa wanapo ongeza na kushusha viwango vya ufaulu!

Isitoshe kutumia marks za maendeleo kama kigezo bado ni kujidanganya kabisa maana walimu wanaweza kumjazia tuu mwanafunzi marks zozote...!
Nadhani hatujaelewana! Mimi ninaufahamu mfumo huu wa GPA vizuri tu, Kama dada joice angeondoa mihemko,angeuboresha mfumo huu pendwa wa nchi nyingi duniani ungeleta tija kwa taifa.ukweli kutoka moyoni mwake alishapania kuuondoa mfumo wa GPA, kuwapa siku saba NECTA ni geresha tu kwa wananchi ili wamuunge mkono, hatakama NECTA wangepewa miaka kumi wasingeweza kubadili adhma ya moyo wake juu ya jambo hili kwasababu alishapania.jiulize? majibu aliyopewa na NECTA aliwasomea yote?.alama za maendeleo zilitimika hata wakati wa division,na zitaendelea kutumika.
 
Hivi kuwambia watu warudishe mfumo wa zamani kwa kuwa uliopo hauna tija ni mihemko? Nikwambie tuu mfumo wa GPA kamwe haufai kwa muundo wetu wa elimu ya chini..zaidi unatumika kuwabeba watu kwa marks za kupewa bure na walimu wao....hakuna chombo cha kupima kama kweli hizo marks za maendeleo wanazopewa ni halali...mfumo huo ni wakuwapumbaza watu tuu!

Kama kweli walikuwa na sababu za msingi wasinge weza kushindwa hata kuuelezea kisayansi hata siku hiyo hiyo waliyo pewa tasks!

Yani tuchukue mfumo kisa tuu unatumika na nchi nyingine? Je tunaweza kumonitor alama za maendeleo wanazo pewa wanafunzi?
 
Ni kawaida ya wanataaluma kujaribu kuibua mijadala. Huu ni utamaduni wa kawaida kwao. Kwangu naungana na Kitila kwa kujaribu kuleta changamoto juu ya maamuzi ya Mwalimu wake (Prof. Ndalichako). Kama alivyosema kwenye andiko lake, anaunga mkono ila anasikitishwa na maamuzi kwa kufanywa pasi na kushirikisha umma ama washikadau wa elimu ama sababu za kisayansi. Swali ninalojiuliza hapa ni kuwa je, wote Profs. Ndalichako na Kitila, mbali na weaknesses zingine, hawakutoa maamuzi kutokana na sababu za kisayansi?

Hapa namaanisha kuwa Kitila (Prof) alipaswa kupata taarifa toka ofisi ya Waziri (mhadhiri mwenzie na mwalimu wake) Prof. Ndalichako kuhusu maamuzi aliyoyafanya. Tunakumbuka kabla ya kutoa maelezo kwa Baraza la Mitihani (NECTA) kufuta mara moja mfumo wa GPA, aliwataka baraza wawasilishe kwake taarifa za kisayansi ni kwa nini waliamua kufuta mfumo wa DIVISION na kutumia mfumo wa GPA. Je, ni kutokana na kukosekana kwa sababu mujarabu za kisayansi ndipo Prof. Ndalichako (Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia) aliamua kutengua mfumo wa GPA na kurejesha mfumo wa DIVISION??? Je, Kitila alibahatika kuziona sababu zilizowasilishwa kwa Waziri (kama ziliwasilishwa)? Na, je, anakubaliana na udhaifu katika sababu zilizowasilishwa kwa Waziri toka Baraza la Mitihani?

Ninapotafakari maamuzi ya Prof. Ndalichako juu ya hili nashawaishika kuona mijadala ya kitaaluma ikiibuliwa katika kutafakari maamuzi mazito juu ya ELIMU YA TANZANIA. Tunapata wigo mpana wa kuona ni kwa jinsi gani kama Taifa tunahitaji kupiga hatua toka kwenye "MAKITAIMU" za mfumo wa madaraja ya ufaulu. Naiona SERA ya ELIMU katika changamoto kubwa sana.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Issue ya GPA Versus DIVISION halina impact sana kwenye ubora wa wahitimu..
Sasa ni wakati wa Prof. Kureview curricula katika levels zote za Elimu... Waunde ya chekechea and pre-schools, waje primary, secondary na high school..

Kuna upotoshaji mkubwa unaendelea watu wakituambia curriculum iliyopo ni Competence based ilhali mashuleni kinachoendelea ni Content based na hata items kwenye mitihani zina reflect hivyo
 
Ndalichako ameamua turudi kule tulikokua kwa sababu yule waziri hakushirikisha wadau kama mkumbo anavyodai. ndiyo maana aliwapa kwanza siku saba NECTA wamwambie kisayansi ni kwa nini walibadili mfumo ili kama mdau wa Elimu haweze kujiridhisha,lakini walishindwa kumpa majibu ndipo akaamua turudi tulopotoka kwanza. na hili alilifanya baada ya malalamiko ya wadau wa Elimu kama akina mkumbo kama anavyodai kuwa walicheka kinafki ilipo badilishwa, Hivyo tumuunge mkono Ndalichako katika hili.
 
Sasa huyu Prof naye shida tu naye anataka kuwa profesa wa siasa. Tulikuwa na mfumo wa Division akaja mwingine akauondoa akaleta mfumo wa GPA huyu wa sasa ka-restore system, hivi ku-restore ni kufanya kitu kipya? Mimi nadhani sasa ni nafasi kwa huyu profesa kutoa maoni yake kwanini anadhani tuhame kwenye division na kwenda kwenye GPA maana kwa jinsi nilivyomsoma ni kwamba waziri wa elimu aliyeondoa division na kuleta GPA hakushrikisha wadau kwa hiyo huyu sasa ame-restore sysytem ili mtoe mawazo yenu
wewe umesoma habari ipi? kama ni hiyo hapo juu inaelezea aliyebadili mfumo bila kushirikisha wadau ni mungai aliyeunganisha hesabu na civics, biology na kiswahili, physics na historia na chemistry na arabic.
wewe unaongelea Dr. kawambwa aliyebadilisha mfumo wa div kwenda GPA? mbona huyo alishirikisha wadau? au unaongelea habari ipi? nauliza!
 
Kweli siasa hukuangusha na pia siasa hukuinua,haya ni maisha na maendeleo ya watu.
 
Akili zetu zinaumbwa na wanasiasa? Wana uwezo kiasi gani kutupangia ukomo wa kufikiri katika kujiletea maendeleo ya kielimu? Kumbe tulivyo wametuumba wao!
 
Back
Top Bottom