Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Kitila Mkumbo: Ndalichako amekosea

Mfumo wa GPA ulikuwa unawachanganya wengi katika kusoma ufaulu binafsi Mimi mwenyewe nilikuwa sielewi ila mfumo wa division wengi wana ujuwa na hata mzazi wengi wameuzoea huwo
 
Kitila Mkumbo anataka kutupotezea muda tuu..yaani anataka mjadala huku watu wakiendelea kubebwa? Prof Ndalichako alisema wazi kuwa Baraza warudishe mfumo wa zamani na marks pia!

Haya mambo ya kupenda kujadili watu wote kila jambo ndio yanayo tufanya tusiendelee...kwanza Kitila mkumbo aache kupotosha Prof Ndalichako hajafanya jipya hapo bali amerudisha mfumo wa zamani na wala sio kubabishwa au kuzungushwa kama anavyo jaribu kutuambia!

Hawa Baraza walipewa wiki nzima kutoa sababu za kisayansi wakashindwa na kuna siku katibu mtendaji aliambiwa ajieleze alishindwa cha kusema!

Sasa kila kitu mnataka mjadala uende bungeni?
 
Kwa hili la kuturudisha kwenye DIVISION kutoka kwenye GPA,wadau tuna muunga mkono Mh. Waziri wa elimu, kwani mfumo huu Watanzania wote tuliuzoea,ila walikuja watu wachache wavivu walio na madaraka wakataka kuwayumbisha Watanzania.Nakumbuka hata Mh. Spika wa bunge la Tanzania wakati huo aliupinga mswada huo wa kubadilisha utaratibu wa ufaulu kutoka DISION kwenda GPA.

Asanteni.
Kama watu wanataka kubaki kwenye GPA basi marks zisishushwe zirudishwe juu! Mfumo wa GPA si mbaya bali taratibu za utumiaji wake kwa ngazi ya chini bado ni tatizo maana sidhani hata hizo marks zinazo jazwa kama maendeleo zina utaratibu maalum..nina hakika kuna wengine wanajaziwa tuu ili wafaulu mitihani! Huu mfumo kwa ngazi ya chini ni mbaya mbaya ....
 
Nashukuru kitila kwa kuliona hili.tatizo wasomi wetu hawaishi na yale waliyoyasomea,wanaishi kwa kufuata mioyo yao na nafsi zao ndiyo maana maamuzi yao yanaonekana ya kukurupuka kwasababu yamejaa chuki,visasi kiburi na dharau.katika hili joice kathibitisha jinsi wasomi wetu wasivyoishi na elimu yao.
 
Tatizo wanasiasa wetu usukumwa na mihemko na ushabiki wa kisiasa wakati hili suala la ufaulu lilipopitishwa kwamba sasa tutumie mfumo wa GPA walikaa kimya na kuunga mkono hoja kama kawaida yao,tufikie mahali tuweke mbele masuala ya kitaifa yanayomgusa Mwananchi moja kwa moja na tuyasimamie vizuri,weledi tulishaona huo mfumo haufai, kuurudisha mfumo wa awali wa ufaulu kutumia Division nampongeza sana Waziri .
 
Tunapoteza muda kubishana mambo yasiyo na msingi. Kama mwanafunzi Ana akili hata uweke mfumo gani atafaulu tu.
 
Nchi gani imewahi fanya public debate ya mifumo ya elimu? , anatafuta sifa za kijinga. Nchi yetu inavitengo vinavyoshughulikia maswala ya taaluma, kama unawazo bunafsi unapeleka huko wazo lako kisha linafanyiwa kazi.
 
huyu Profesa anaingiza siasa kwenye elimu yeye mwenyewe anaeleza ulipoletwa mfumo wa gpa walipinga pia anasema uliletwa ili kuficha udhaifu wa serikali sababu wanafunzi wengi walikuwa wanafeli sasa anataka mjadala uitishwe wa nini, kma baraza ambalo lilibadirishwa limeulizwa limeshindwa kutoa majibu hao watakao kuja kwenye mjadala watatoa majibu gani.Kwa kifupi anataka aonekane kwenye media maana sasa hivi majipu yanatumbuliwa hivyo watu kama yeye wamesahaulika
 
Hivi huko UDSM kila mtu akina senior lecturer anapewa u-professor ? Mbona naona utitiri wa maprofessor lakini wengi wao ni wakawaida sana, na yule mnamuita Dr Bana sijui, mmeshampa u-professor?
 
Prof. Mkumbo umesema na yangu. Lengo la prof Ndalichako si baya. Utaratibu wa maamuzi si mzuri kwa kweli. Lkn walivyokuwa wameshusha viwango vya ufaulu ilikuwa inaboa sana. Mtu ana D mbili amefaulu?
Sasa siasa basi kwenye elimu, weleji ujidhihirishe.

Mkuu kuna maana gani ya kufanya mjadala ambao wote tunajua tutafika kwenye same conclusion?

Yaani sote tunajua tunataka kile na siyo hiki, kwa nini isiamuliwe moja tu kupunguza muda wa kufanya kazi zingine?
 
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anataka tena kuturudisha nyuma, upele umepata mkunaji tena naona asiishie kwenye GPA tu aende mbele kuangalia degree za pili zinazotolewa na vyuo vya hasa Vodafasta Mzumbe na kwingineko kama hazina viwango futa zote tuanze upya.Tulishakosea mwanzo kwa Shukuru Kawambwa sasa tusiendelee kukosea, bora afumue ujinga wote tuchelewe kufika ila tuwe tumetengeneza
 
Sasa huyu Prof naye shida tu naye anataka kuwa profesa wa siasa. Tulikuwa na mfumo wa Division akaja mwingine akauondoa akaleta mfumo wa GPA huyu wa sasa ka-restore system, hivi ku-restore ni kufanya kufanya kitu kipya? Mimi nadhani sasa ni nafasi kwa huyu profesa kutoa maoni yake kwanini anadhani tuhame kwenye division na kwenda kwenye GPA maana kwa jinsi nilivyomsoma ni kwamba waziri wa elimu aliyeondoa division na kuleta GPA hakushrikisha wadau kwa hiyo huyu sasa ame-restore sysytem ili mtoe mawazo yenu
mfumo wa divisheni ni mzuri na wadau wa elimu wanaukubali. mfumo huu umenuia kurudisha ubora wa elimu ulioharibiwa na mfumo wa GPA baada ya wanasiasa kushusha mpango wa ufaulu ili kupata wanafunzi wa kujaza sekondari za kata. sasa hv wanafunzi wanafunzi hawachaguliwi kulingana na ufaulu bali wanachaguliwa kwenda kujaza nafasi katika sekonadari za kata.

dr msonde na wanasiasa wake waliobadili mfumo walishindwa umuhimu wa mfumo wa GPA...hauna tija.
 
Kwani mfumo wa division ulianza mwaka gani..!?? Kabla haujaanza si watu walifanya tafiti wakaukubali kutokana na grading system yake..!? Maana 'division' Ni jina tu linawakilisha ufaulu wa kiwango fulani... Sasa kuna watu kwa malengo yao ya kisiasa na kutambua kwamba wananchi wengi JAPO hawajui numerically kwamba mfano mtoto akipata division 3 ana interval gani ya marks za ufaulu , tayari WANAJUA division ipi ni ufaulu mzuri sana, mzuri au mbaya sana... Wanasiasa wakawapoteza kwa kubadilisha majina badala ya division wakaita GPA huku pia wakishusha marks za madaraja yaliyo ndani ya GPA...(Wameficha Ujinga ndani ya jina) Sasa Ndalichako anahitaji discussion gani kurestore mfumo to division wakati tafiti zinazosupport mfumo wa division zipo na anajua kwa nini watu fulani walibadili jina toka division kwenda GPA!?
 
Mkuu huu uandishi ndo ulifundishwa hivi shuleni au umejiamulia tu!!
hahaha! huyu jamaa atakuwa anatetea mfumo uliomvusha kiubwete ndio maana anamshambulia sana prof ndalichako. serikali ya ccm imeiharibu elimu yetu kabisa. eti paper 2 inaitwa continous assesment...hiki akili za kimulugo ndizo zilizoifikisha hii nchi hapa ilipo.
 
Binafsi sioni sababu yoyote ya msingi ya kubadili mfumo wa kutoa matokeo kutoka kwenye DIVISION kwenda kwenye GPA kwa sababu mfumo wa DIVISION haukuwa na tatizo lolote. Wazungu wanasema "If it aint broke, dont fix it."
 
Back
Top Bottom