Kiti moto vs viagra

Whisper

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
502
207
Rais Adai Nyama ya Nguruwe Ina Nguvu Kuliko ViagraRais wa Argentina, Bi. Cristina Fernandez amedai kuwa kula ya nyama ya nguruwe kunaongeza nguvu za kimapenzi kuliko viagra.

"Niliambiwa kitu ambacho nilikuwa sikijui, kula nyama ya nguruwe kunaongeza nguvu za mapenzi", alisema bi Cristina akiwaambia viongozi wa viwanda vya nyama ya nguruwe.

"Naweza kuwaambia kuwa ni bora kula nyama ya nguruwe kuliko kutumia viagra".

Bi Cristina aliongeza kuwa mwishoni mwa wiki yeye na mumewe ambaye alikuwa rais wa Argentina kabla ya kumaliza muda wake, walikula nyama ya nguruwe na baada ya hapo mambo ya malavi davi yalienda vizuri sana kulikon kawaida.

"Inaweza kuwa kweli, jaribu ujionee mwenyewe", aliongeza rais huyo wa Argentina katika hotuba yake ambayo ilirushwa live kwenye luninga.

Argentina ndio nchi inayoongoza duniani kwa kula nyama ya ng'ombe lakini kutokana na kuongezeka kwa bei ya nyama ya ng'ombe, serikali ya Argentina imekuwa ikipiga kampeni watu waanze kula nyama za nguruwe.

Naye mkuu wa umoja wa wazalishaji wa nyama ya nguruwe nchini humo, Juan Uccelli, alimuunga mkono rais Fernandez kuhusiana na matumizi ya nyama ya nguruwe kwaajili ya nguvu za kimapenzi.

Juan alisema kuwa watu katika nchi za Denmark na Japan ambazo zinaongoza duniani kwa ulaji wa nyama ya nguruwe, wana maisha mazuri ya kimapenzi kuliko watu wa Argentina.

Source: AFP
 
Hii ikidhibitika, bei ya mkuu wa meza itaspike vibaya kwa hapa Tz.
Let it not be the case!!
 
aisee naunga mkono, hii ni post bora kuliko zote leo maana imetoa taarifa ya jambo la msingi sana.....asante sana.
 
WACHA NIWAI MAENEO SAHIZI MAANA NDIO WEEKEND IYOOOO!!

Nenda kwa Kinibu anasema bado ipo shazi na kwaminie wewe 1KG alone
icon10.gif
 
ZA mBEYA ZIMELISHWA ARV'S,
TUWE MAKINI NA TUNACHOKILA
mAGUFULI NA WAFUGAJI WENZAKE KULE wIZARANI Kwao wametuhakikishia hakuna mahusiano chanya kati ya Kitimoto ya mbeya na kulishwa ARV, maneno yawazandiki , wanatutazama kwa macho ya wivu na husuda tukijilia mnyama wetu.....lete kitimoto kilo moja , Rost na ndizi mbili.
 
du bonge la kampeni hilo from rais angetu pm sasa kashatangaza hadharani watatupandishia bei hawa ah
 
Kata kilo 2, ndizi 6, kachumbali bakuli na mchicha. Waiter, leta mzaramo na water soda. Hii ndio weekend yangu. Jioni nguvu zitakuwa 4x4x4xfar
 
mAGUFULI NA WAFUGAJI WENZAKE KULE wIZARANI Kwao wametuhakikishia hakuna mahusiano chanya kati ya Kitimoto ya mbeya na kulishwa ARV, maneno yawazandiki , wanatutazama kwa macho ya wivu na husuda tukijilia mnyama wetu.....lete kitimoto kilo moja , Rost na ndizi mbili.

Acha bwana ya Mbeya so mchezo halafu unapewa na mboga ya majani pembeni kwa kujali zaidi afya yako-I real miss that thing
 
Acha bwana ya Mbeya so mchezo halafu unapewa na mboga ya majani pembeni kwa kujali zaidi afya yako-I real miss that thing
waacha , maana Mbeya unapewa Mboga ya majani, ndizi za kuchoma ama kungaa rost , na kipande cha parachichi ...buree ofa mdau, niliwahi kufika huko miaka ya 90, nitarudi tena Mbeya.
 
aaaah !!! waungwana mlikuwa hamlitambui hilo, hiyo kitu kiboko inaongeza nguvu zote: za kike, za kiume, za giza, za nuru, za kiroho, za kimwili, hata popobawa hakugusi ati!
firstlady1-test japo 0.5kg utaniambiiiiiiiia, kileleni 10 times within 2min na unalia kama beberu la kitimoto vile.
Ila kama mtu hujaoa au kuolewa - PLEASE DON'T TRY THIS AT HOME -
 
Back
Top Bottom