Kitendo cha watu kulia harusini, tatizo ni nini?

Kitendo cha watu kulia harusini, tatizo ni nini?

Mwanaume halii kama akilia inawezekana huyo mwanamke alimpata kwa shida sana mwisho wa siku kampata kwa hiyo kama haamini hivi...



Wanawake wapo too emotional... Wanalia kwa furaha ya kuolewa.. Pia wanalia kuziacha familia zao...
 
Furaha iliyozidi huwezi kuimaliza kwa kucheka ama kununa lazima mtu alie ili amalize furaha yake yote awe huru. Huo ndo ukweli. Siyo harusini tu hata mtu akishinda jambo fulani hulia kwa furaha.
 
Kulia ni kama kinogesho/swaga/mahanjam ya harusi.Ni kama ukitaka kunywa lusekelo wenyewe wanautamaduni wa kuipiga kibao kalioni Alafu wanailaza
 
I can show and then u wont show up. Then likely, i may show the picture which is not of my own. How ar u going to believe that it is the one..... Just the matter of PMing then we shall talk more.... Hahahha
Mhmmhmhmhmhmhmhmhmhmhmh..

Haya bana nimekuelewa
 
siku moja kabla ya kuolewa nilikua naona siku haiendi kesho ifike na mimi niwe na uhakika wa mtu wa kulala nae siku 365 na robo,siku ilipofika asubuhi mpaka mida ya jioni ilikua ni furaha tu, nilianza kulengwa lengwa na machozi pale nilipopewa wosia wa wazazi kwenye sherehe na Kubabidhia katika familia mpya "nikajisemea eeh inamaana ni kweli mimi na familia yangu niliyoizoea ndio tunatengana kweli" Nikalia tena baba yangu aliponiambia "ukifanyiwa baya lolote usije kwangu kuanzia Leo nimekukabidhi kwa baba mwingine wa kushughulikia matatizo yako,ukija kwangu nitakuondoa kabla hujakaa chini, ukiwa na mazuri njoo hata usiku unigongee dirishani" nikalia kwa maana niliwaza huyu baba baba gani anayenitaka kwa mazuri tu tofauti na zamani?
Kimbembe pale nilipopigiwa wimbo wa Twanga pepeta "ayaya kuolewa, nitarudi nyumbani kutembea........!! Hakii chozi liliongezeka kwa kweli" sitaisahau ile siku maana ilikua nzito kuliko siku zangu zoote ,Alhamdullilah maisha yamekua mazuri mpaka hii Leo
Huyo baba ata ingekua mimi ningelia!!! Leo tu kanipiga marufuku kumuomba vocha machozi yakanilenga [emoji4][emoji4][emoji4]
 
Yaani wazee wakishapokea mahari wanatugeukaga balaa hahaha kifupi wanakua wametuuza
Mda mwingine nikiwaza ishu ya ndoa najishisi kama mfugo tu hapa nyumbani!!! Wamejitolea tu kunilea, akija kijana fulani hapo ananichukua kuanzia mwili mpaka jina!!! Daah!!! Wanawake tuna shida, yaani unaanza maisha upya na familia nyingine...
 
Back
Top Bottom