siku moja kabla ya kuolewa nilikua naona siku haiendi kesho ifike na mimi niwe na uhakika wa mtu wa kulala nae siku 365 na robo,siku ilipofika asubuhi mpaka mida ya jioni ilikua ni furaha tu, nilianza kulengwa lengwa na machozi pale nilipopewa wosia wa wazazi kwenye sherehe na Kubabidhia katika familia mpya "nikajisemea eeh inamaana ni kweli mimi na familia yangu niliyoizoea ndio tunatengana kweli" Nikalia tena baba yangu aliponiambia "ukifanyiwa baya lolote usije kwangu kuanzia Leo nimekukabidhi kwa baba mwingine wa kushughulikia matatizo yako,ukija kwangu nitakuondoa kabla hujakaa chini, ukiwa na mazuri njoo hata usiku unigongee dirishani" nikalia kwa maana niliwaza huyu baba baba gani anayenitaka kwa mazuri tu tofauti na zamani?
Kimbembe pale nilipopigiwa wimbo wa Twanga pepeta "ayaya kuolewa, nitarudi nyumbani kutembea........!! Hakii chozi liliongezeka kwa kweli" sitaisahau ile siku maana ilikua nzito kuliko siku zangu zoote ,Alhamdullilah maisha yamekua mazuri mpaka hii Leo