Kitendo cha watu kulia harusini, tatizo ni nini?

Kitendo cha watu kulia harusini, tatizo ni nini?

Ni hisia kali haswa ya kumbukumbu zilizopita, ama wosia unaopewa pale mbele ya kadamnasi.
 
Kwa wanume wanalia majukumu ya pande zote mbili hasa ukweni kutoa mchango wa huduma za kimaisha
 
Kutoka moyoni mwangu, mimi nililia pale nilipoenda kupeleka keki kwa wazazi wangu, mc akasema ndio uende ukaage hivyo, kurudi ni maajaliwa ya mwenyezi mungu, kwakweli nililia had mama naye akalia. Siku hizi hakuna kilio full kuchekelea, kwanza niliwaza naenda familia tofauti, nawaacha ndugu zangu, yaani acheni had leo huwa mume wangu ananiuliza wee ulilia sana siku ya send off ulikuwa unawaza nini???? Had na yeye aliingia simanzi. Huwa sipendi kuikumbuka siku yangu ya send off, niliumia sana kuondoka nyumbani. Had leo nina miaka 14 ya ndoa. Ila ndoa ina mambo mengi jamani unatakiwa ujitoe katika nafsi.
 
Back
Top Bottom