Kitendawili Tega?

Jiko la gesi nalo lina mafiga? Mkubwa wa jiko ni chumvi bibie hujuwi kuwa Chakula bila ya chumvi hakinogi? Sawasawa na mwanamme asiye kuwa na Mwanamke hana raha ya maisha.

Hata mwenye swali hajui jibu, kwani vyakula vyote vyatiwa chumvi? Mkubwa wa jiko moto, hakuna chakula kipikwacho bila moto
 
kama wahitaji kunogesha then si lazima uingie jikoni waweza nogeshea hata mezani, ila kama wataka kupika sharti uingie jikoni, na ili ukipike chakula lazima ukitie motoni ili kiweze kuiva. chumvi ni kiungo tuu, kwani sio vyakula vyoote hutiwa chumvi, wengine twala ugali kwa maziwa no chumvi involved
 
Hata mwenye swali hajui jibu, kwani vyakula vyote vyatiwa chumvi? Mkubwa wa jiko moto, hakuna chakula kipikwacho bila moto
Na huo moto utawashwa na nani kama si mpishi?
Mkubwa wa jiko mpishi bana!
Na isitoshe si kila viliwavyo lazima vipikwe..........Kachumbari yapikwa?
 
Na huo moto utawashwa na nani kama si mpishi?
Mkubwa wa jiko mpishi bana!
Na isitoshe si kila viliwavyo lazima vipikwe..........Kachumbari yapikwa?

Babu kwanza Shikamoooo! Hapa napata picha kuwa neno jiko ni neno tata, labda mtunzi atueleweshe amemaanisha nini aliposema jiko? By the way kwani kachumbari yahusisha jiko? Mie sijambo
 
Na huo moto utawashwa na nani kama si mpishi?
Mkubwa wa jiko mpishi bana!
Na isitoshe si kila viliwavyo lazima vipikwe..........Kachumbari yapikwa?
Nakuslimia kwa jina la bwana babu,nimefurahi kwa vile kumbe hata mambo kitchen uko pouwa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom