Unajua Kaizer - kitchen party haifundishi tu namna ya kumfurahisha mwandani wako.Kuna mambo mengine kwamfano matumizi ya vifaa na technoljia mbalimbali za usafi, kuhuisha kazi na maisha ya kifamilia kwa career women, kupunguza migogoro - hivi ni vitu ambavyo vina evolve with time.Yapo mengi sana..usiangalie upande mmoja tu.Kama ni hilo tu mbona kila mtu angejitafutia namna yake ya survival?
Ofcourse inategemea mtu anaenda KP gani....
Kitu nimejifunza ni kuwa KP pia ni class issue!
Enhe..Vera,, tukiweka suala la class kwenye equation, nadhani utakubaliana na mimi kuwa kwa wale wa relatively lower classess ndo wako most likely kuengage kwenye KP zinazofundisha mambo ya kitandani tu..kwa sababu asset restrictions zao zinawafanya washindwe kujadili mengine ambayo kwa wale walio kwenye class za juu wangejadili kama mambo ya teknolojia ulivosema hapo juu. Na pia, nina wasi wasi kuwa suala la career bado halijawa mainstream kwenye KP...kwa nyingi wanapractice traditional KP ambayo ina mazaga zaga kibao ysiyo na maana au ambayo yanajulikana tayari. kama ulivosema, haya yatachukua muda na by the inaweza hata kubadilika jina isiwe KP tena.
Mimi naona si kweli kwamba zinaharibu, inategemea na wewe mwenyewe unavyotaka ,na type ya wewe mwenyewe ulivyo pamoja na ndugu, jamaa na marafiki ulionao jinsi walivyo. kwa ufupi Kitchen part inaku potray wewe ulivyo, kama ni shangingi na kampani yako ya mashangingi, obvious hata kp itakuwa ya rusha roho na mwaga radhi na matusi kibao, lakini kama ni mtu wa church mwenye maadili itajaa marafiki wacha Mungu na wamama wenye heshima zao na watakufundisha kimaadili na mistari ya neno la Mungu kibao, yani ni gospel songs kwa kwenda mbele.
Lakini pia kama si shangingi na si mcha Mungu kivile lakini mstaarabu yani uko reserved pia watu utakaowaalika watakua hivyo na sherehe itakuwa ya kistaarabu kuanzia mavazi , nyimbo zitazochezwa hadi manebno yatayozungumzwa.
Ka ufupi unao uwezo wa kuamua kitu gani unataka kwenye kp yako according to your behaviour and lifestyle, mi nimeona nyingi tu zenye heshima za kutosha, hizo za ajabu sijawahi kuudhuria ndo maana nasema it depends.
Carmel
Asante kwa kuchangia mtizamo chanya kuhusu KP... nadhani point yangu juu ya class uneiweka vizuri mno.
asante DCDada iwe mchango ni chanya au hasi, usijali. Hizo zote ni packages kutegemea na mahitaji ya mtu. Kama KP itakuwa ya kipuuzi mwanangu au my wife wangu hawezi kwenda kwa sababu mim na family yangu hatuko kwenye hizo line. Kwa hiyo waache watu wajirushe wanavyopenda. Kitu cha muhimu ni mtu binafsi kuchagua anachotaka!
asante DC
Nilikuwa namshukuru Carmel kwa kutupatia positive side maana wengi walionyesha negative side tu kama vile KP zote ni mbaya.
Haya mambo ya akina dada kufundwa kwa one event ya kitchen party ni ulaghai mtupu.
Vera, natumaini umeona video hii: https://www.jamiiforums.com/mambo-ya-kikubwa/40268-mpo-kisusio-hichoooo.html... unategemea binti/dada atajifunza nini kutoka katika hiyo party kubwa kama inavyoonekana hapo?
Jando na unyago vilikuwa/vina maana zaidi ya haya mambo ya kuigaiga ya kimjini ambapo focus kubwa inakuwa kuoneshana ukubwa wa party na wageni rasmi na minjonjo ya kitandani.
Bora sisi wanaume tumekata shauri kabisa kwenye stag nights zetu ya kwamba; huko ni mwendo wa booze kwa sana na private dancers!! (https://www.jamiiforums.com/494896-post13.html)
Najisikia nianzishe darasa hapahapa kinyume na taratibu za elimu hiii, kharr
Ndugu yangu
unavyojisikia ndivyo nami najisikia...... mambo yamekuwa diluted mno hadi kukosa ladha na maana.
Hiki tunachojadili ni darasa la introduction.Full programme baadae.
That will be perfect!So, Vera.... would you wanna team with me to get this programme going?! what do you say.... I too am interested. I see you've been on this case for a while.
una uhakika na maneno yako asilimia mia mkuu?Huu ni uswahili swahili (whatever the hell that means) tu na elimu ndogo. Huwezi kumkuta mtu aliyeelimika kama Mama Migiro akimfanyia bintiye huu ujinga ujinga. Hata wanawake wale wanaofagilia huu upuuzi ukiangalia elimu zao ndi ndogo sana.
Nyambaaaf kabisa...
Huu ni uswahili swahili (whatever the hell that means) tu na elimu ndogo. Huwezi kumkuta mtu aliyeelimika kama Mama Migiro akimfanyia bintiye huu ujinga ujinga. Hata wanawake wale wanaofagilia huu upuuzi ukiangalia elimu zao ndi ndogo sana.
Nyambaaaf kabisa...
una uhakika na maneno yako asilimia mia mkuu?
...vipi kuhusu jando na swala zima la kufundwa?
Huu ni uswahili swahili (whatever the hell that means) tu na elimu ndogo. Huwezi kumkuta mtu aliyeelimika kama Mama Migiro akimfanyia bintiye huu ujinga ujinga. Hata wanawake wale wanaofagilia huu upuuzi ukiangalia elimu zao ndi ndogo sana.
Nyambaaaf kabisa...