Kitchen Party: Yatokanayo... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kitchen Party: Yatokanayo...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by WomanOfSubstance, Oct 8, 2009.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kitchen party ni biashara kubwa sana kadri miaka inavyoenda.Nielewavyo mimi KP ( kufundwa bi harusi) huko nyuma,makabila mbalimbali yalitumia siku chache kabla y aharusi kukaa na bi harusi mtarajiwa kumshauri kuhusu majukumu atakayoenda kukutana nayo kama mke na hata mama.Alipewa mawaidha mbalimbali yanayohusu usafi wake binafsi, usafi wa nyumbani kwake, umuhimu wa kuwa mchapakazi na siyo mvivu, kumheshimu na kumpenda mume wake; kuwajali ndugu wa mume, kukaa na marafiki/mashoga na hatari ya kuwavuta karibu na mumewe; na mengine mengi.

  Katika kabila langu mimi jukumu hili lilibebwa na wanawake walioko kwenye ndoa tu na walioheshimika kwenye jamii na si vinginevyo.Shughuli hii ilikuwa private na haikuhusisha watu wengi sana na wala haikuhitaji gharama kubwa sana.Mfundaji hakulipwa ujira au malipo ya pesa, sana sana aliweza kutunukiwa zawadi ndogondogo kadri mtu alivyoona inafaa.Wanaume hawakuhusishwa kwa namna yoyote ile maana na wao walikuwa na utaratibu wao wa kuandaa bwana harusi.( Makabila yanatofautiana na hapa ndipo nitaomba michango yenu)

  Katika ustaarabu wa wenzetu wazungu kuna kitu kinaitwa bridal shower ambacho asili yake ni nchi za Ulaya ukasambaa na kukomaa na kudumu nchi za America ya kaskazini.Bridal Shower ilikuwa ni tafrija iliyoandaliwa mahususi na wale wasichana wa kusimamia harusi - Bridesmaids( marafiki na ndugu wa bi harusi mtarajiwa) kumzawadia bibi harusi wiki chache kabla ya siku yenyewe ya harusi.Vilevile kufuatana na historia hii ilikuwa siku maalum pia "kumfunda" mtarajiwa kuhusu majukumu yake kama mke na mama.

  Kwa Tanzania shughuli hii imeendelea kukua siku hadi siku na kuongezeka ukubwa na gharama na hata maudhui na mpangilio wake.Inaunganisha watu wa marika tofauti, makabila na dini mbalimbali.Inaanza na kukusanya michango, kununua sare, kuandaa vyakula na vinywaji,anakuwepo mshereheshaji mwenye kutumia kipaza sauti ( hakuna siri tena), wapiga picha za mnato na video na muziki ambao mara nyingi ni wanaume ( wanaume wameanza kuingia kwenye KP!!) na pia utoaji mada na nasaha .Muziki unakuwa mchanganyiko lakini mara nyingi ni rusha roho na vijembe vya hapa na pale.Shughuli haifanyiki nyumbani ( kitchen)tena kama huko nyuma - sasa imehamia kwenye kumbi na kumbi nyingi unakutana kuna wanaume .

  Kwenye maudhui watu hutoafautiana katika KP nilizowahi kuhudhuria.Kuna wale wenye kutoa mada zilizoandaliwa kitaalam kulenga kumpa mawaidha mema yenye staha ( nimeona wakinukuu hata vitabu vya dini) na kuna wale wenye kumwaga radhi - kuongea maneno makali yasiyo na staha, kuonyesha kwa vitendo namna ya kumfurahisha mume na wakati mwingi ni aibu tupu kuona wanawake wenye umri wa kutosha wakisimulia mambo ya chumbani bila haya wala soni kwenye kadamnasi yenye watu wa marika mbalimbali.Niliwahi kuona KP moja vijana wa kiume wakiona aibu na kucheka kiaibuaibu maana walitakiwa kukoleza hayo mawaidha kwa kibwagizo maalum kilichochaguliwa na huyo MC! - ILILKUWA AIBU KUBWA.
  Kwa kifupi kwa maoni yangu nimeona kuwa KP hizi ni mchanganyiko usioleweka - kuna elements za Bridal shower ya kizungu, kuna mambo ya Pwani ya kurushana roho, kuna mambo ya kidini kwa maana ya mawaidha ya dini, alimradi ni vurugu tupu.Sijawahi kusikia utafiti wowote uliofanyika kutathmini kama KP zinasaidia kudumisha ndoa au la, au kuona kama mafunzo yanayotolewa kwenye KP yanatumika na walioolewa ili kudumisha ndoa zao.Kama kunautafiti huo, naomba tuhabarishane na kupeana rejea ili tuusake tujisomee wenyewe.

  Ukipiga hesabu ya gharama inayotumika, muda, na kinachotokana na hiyo KP nadhani kwa wale wachumi watasema ni kutupa pesa kwenye shimo.Lakini kwa wanajamii watasema hapana.Hii ni fursa ya akina mama kutandaa ( networking), kujirusha na kuondoa stress - hata kama kinachopatikana hapo kwa maana ya kudumisha ndoa ya mtarajiwa ni nil.
  Ninayo mengi ya kuongea lakini nisimalize uhondo - nawaachia na wengine watoe maoni yao.
  Je- KP hizi zina tija na mwelekeo unafaa?
   
 2. GP

  GP JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  KP totally waste.
   
 3. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,488
  Trophy Points: 280
  Kila siku nawashaurini, tuhusisheni sisi wazoefu kuwafunda hao mashosti nyie hamtaki. Tena mi ntafanya free of charge especially kwenye practical.
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kitchen pati miyeyusho mkuu, mi nikitaka kuoa binti ntamwambia kabisa NO KITCHEN PARTY, akifanya tu basi ajue NO MARRIAGE.
  wewe si umeiona hii hapa inaitwa kisusio??, khaaa ndio upuuzi gani huo, ntamfundisha mie mwenyewe, Alaa.
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  HIVI SHEMEJI UPO?hebu ni piemu basi tutete!..........
   
 6. GP

  GP JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nipo mkuu,
  halafu siku hizi mbona hupatikani hewani?
   
 7. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Kp??! no 4 me. Mi hata harus yangu nataka iwe simpo. Ntaalika washkaji zangu wa karibu sana, ndugu wale wanaonijali kwishney. Hii ni kuepuka unnecessary costs. 2 me y kp, maharus makubwa? Twaweza fanya mambo ya maana zaidi kulikokuchoma mamilioni ya fweza.
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  GP usinichekeshe mie...
  Kuna shostito mmoja alikuwa anaolewa, familia ikamwambia hawatakuwa na uwezo kumfanyia KP bali send-off tu.Wacha aangue kilio! Akasema kuliko asifanyiwe KP bora send off ife!
  Ndio uelewe KP inavyoshabikiwa.
   
 9. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Binamu
  Ina maana hiyo practical utaosha vyombo, utapika au utajipamba?
   
 10. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Huko wenyewe wanaita " Kusasambua"-au kutoa sanduku la mwali..
   
 11. GP

  GP JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  eeeeh abari ndo iyo!!,
  KP wizi mtupu, nyingi zinafundisha uhuni tu hamna lolote.
  basi na sie wanaume tuwe na nini sasa, sitting room party au??
   
 12. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Nyie mnayo bachelors party..ila sina uhakika ya kinachoendelea humo ndani.Tumsubiri Fidel na wengineo watuhabarishe.
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,488
  Trophy Points: 280
  Kule ni bia na kufunzwa jinsi ya kucheat na kusepa ukifumaniwa.
   
 14. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #14
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kwa mtazamo wangu naona kitchen party aisaidii chochote zaidi ya kuharibu.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  eheee..tuhabarishe mkuu
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  ina maana hakuna faida yoyote kwenye KP?Inaharibu nini kwani?
  Ingependeza watu wakitupa mifano hai...
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,488
  Trophy Points: 280
  Unataka kujua zaidi ya hayo? Tatizo nikiyaweka hewani wakiingia kina nanihino wananishambuliaga sana bana.
   
 18. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #18
  Oct 8, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  I am missing Yo Yo and my Mpwa Fidel80 hawa huwa wanaenda live kwenye KP! na wana clips
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Chrispin unasma uongo jamani weye kaka teh teh teh
   
 20. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,860
  Likes Received: 23,488
  Trophy Points: 280
  Ikiwa nimesema uongo, toa ushahidi wa uongo wangu, lakini kama nimesema vema, kwanini wanipinga?
   
Loading...