Kitanda cha VONO!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,731
Wakuu,
Wakongwe kidogo kama mimi mnavikumbuka vitanda vya namna hii?
Mi nakumbuka tumevitumia sana enzi hizo, hata wazee wetu tulikuta wanavitumia!

Ninachojiuliza ni kuwa wazungu walikuwa na sababu gani kueneza vitanda vya namna hii kwa wingi huku Africa, wakati miti ya mbao ilikuwa kwa wingi nchini?...Au tuseme ilianza teknolojia ya chuma kwanza ndipo ikafuatia ya mbao?
Nashukuru Mungu zama hizo hatukuwa watundu kama walivyo dot.com wa leo, vinginevyo ingekuwa aibu majumbani!...Lol!
kitanda vono.jpg
 
Attachments

  • edwardian-metal-kitanda vono.jpg
    edwardian-metal-kitanda vono.jpg
    35.1 KB · Views: 371
Kulikuwa na vitanda vya miti (na kamba) vinaitwa 'telemka, tukaze'! Sina uhakika kama ilikuwa ni kukopi kutoka hiyo 'vono' au vilikuwapo kabla yake. Lakini kiasili, makabila mengi walikuwa wanalala chini au wanatengeneza kama kichanja hivi.
 
Mazee vijana wa Do.com walivyo na mbwembwe hizo spiringi zisingehimili vishindo maana geuka huku geuka kule mguu pande mguu sawa ingekuwa tabu kabisa.
 
Kulikuwa na vitanda vya miti (na kamba) vinaitwa 'telemka, tukaze'! Sina uhakika kama ilikuwa ni kukopi kutoka hiyo 'vono' au vilikuwapo kabla yake. Lakini kiasili, makabila mengi walikuwa wanalala chini au wanatengeneza kama kichanja hivi.
Mkuu!
Unavikumbuka vya aina hii nini?
IMG_4061.JPG
 
Mkuu!
Unavikumbuka vya aina hii nini?

Exactly!....unafanya research ya vitanda nini? Kuna maneno kama 'tendegu' yanaanza kupotea taratibu kwa kuadimika kwa viatanda hivi. Inavutia kuona kumbe bado vinatumika/vinatengenezwa na kuuzwa (maana hiyo picha inaonekana ni recent tu).
 
maybe wazungu waliona mbali kuhusu uharibifu wa mazingira. angalia tulipo sasa, vitanda vya mbao na makabati bei haishikiki. ukitaka kitu cha mbao ya mnazi, mkoko, mpingo ama mninga inabidi ulipie huku umejishikilia mahali kwa jinsi bei ilivyo mbaya.
PJ:hivyo vitanda pia viliitwa banco?
 
haaa haaa umenikumbusha mbali sana
tulikuwa tuna toa hizo coil spring ili kisipige kelele
!:becky:
Aisee!
Nakumbuka nikiwa sekondari, baadhi ya wanafunzi watundu walikuwa wanatoa spring zote, kitanda kinalegea kiasi kwamba mtu analala na kuwekewa godoro juu, na kitanda kinaonekana flat tu, na hivyo anakwepa kuingia darasani, hata mwalimu akipita mabwenini hagundui kitu!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
maybe wazungu waliona mbali kuhusu uharibifu wa mazingira. angalia tulipo sasa, vitanda vya mbao na makabati bei haishikiki. ukitaka kitu cha mbao ya mnazi, mkoko, mpingo ama mninga inabidi ulipie huku umejishikilia mahali kwa jinsi bei ilivyo mbaya.
PJ:hivyo vitanda pia viliitwa banco?
Sure,
Inabidi ujishikilie ukutani ili usidondoke kwa Presha!...lol!

King'asti
Umefuatilia kwa umakini hii habari!...Nadhani kwa sasa haya mavitanda ya special yanayotoka Dubai, China nk yako cheaper kuliko vya kibongo!
 
Exactly!....unafanya research ya vitanda nini? Kuna maneno kama 'tendegu' yanaanza kupotea taratibu kwa kuadimika kwa viatanda hivi. Inavutia kuona kumbe bado vinatumika/vinatengenezwa na kuuzwa (maana hiyo picha inaonekana ni recent tu).
Na ukitaka kupajua hapo ambako bado wanatumia vitanda hivyo angalia picha kwa umakini!
Utaona Minazi, miembe, barabara kubwa ya lami na picha za kampeni za mgombea fulani!
Ukichanganya na zako utajua ni wapi!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
hahaha,unajua tena za wamama,kila siku unataka nyumba ibadilike. hivyo vitanda vya chuma kutoka japani vitakua havidumu nadhani. kuna vijana wa mitaani wanatengeneza anything hata ukileta picha tu. wanatumia nondo kabisa za mikocheni,lol! hapo kitanda hakiliwi na wadudu wala nini.wanatengeneza even shelves za bafuni, kabati u name it.problem ni kwamba hata ukijilipua na hizo mbao,watakupa ambazo hazijakomaa ama kukauka, or else wakushikishe soft wood waliochakachua. taabu tupu,tumerudi eden!
Sure,
Inabidi ujishikilie ukutani ili usidondoke kwa Presha!...lol!

King'asti
Umefuatilia kwa umakini hii habari!...Nadhani kwa sasa haya mavitanda ya special yanayotoka Dubai, China nk yako cheaper kuliko vya kibongo!
 
dah, long time ago! Nakumbuka nilikuwa nikiunga vile vi-mnyororo nafungia popi wangu alafu kule naweka katani bila wazee kujua
 
Hivo vitanda havina ADABU especially ukiwa nacho kwenye chumba cha kupanga ambacho juu hakina Dari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom