Kitabu: Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)

Ndugu yangu,
Hapa ndipo mnapokosea.Binafsi naamini kwa mfano harakati za uhuru wa nchi kama Tanganyika iliyokuwa Trusteeship ya UN chini ya Waingereza ulikuwa tofauti na Kenya ambapo "waliopigana kikwelikweli" dhidi ya Ukoloni wa Waingereza na kujipatia uhuru kwa kumwaga damu.Sina maana ya kubeza "harakati za Uhuru" wa Tanganyika lakini nataka kusema kuwa kuendelea kulilia credit kuhusu nani " alileta uhuru' kunanifanya nicheke kidogo. Besides, kipindi kile wimbi la kuyaachia makoloni unproductive lilikuwa linafagia kila mahali! Wawepo waislam au wapagani bado Uhuru ungekuja tu! Hivi tu tunataka kutoana roho kuhusu " nani alileta uhuru, ingekuwaje kama watu kweli wangeingia kwenye mapambano? Na ndio maana kwangu mimi na baadhi ya wengine hapa, tumeuliza mara nyingi - je katika " real" mapambano kama yale yaliyofanywa dhidi ya Wajerumani (na wajerumani wakaenda kuleta Mamluki wa kiislam akina Sykes kama Mwandishi wa hiki kitabu alivyoandika) je mchango wa wapagani, wakristo na hata waislam ulikuwaje?

Samahani kama nitasomeka ndivyo sivyo.

Kuhusu Ukatoliki wa Nyerere na kuhusishwa kwa Kanisa katika lawama na shutuma nzito hizi, hamuoni mnakosea? Ni kama kuhusisha vitendo vya mtu mmoja muislam na Uislam ( assuming kweli mtu huyo alitumia dini/imani yake kufanya dhuluma au uonevu)!

Hiki ni kitabu tu nimeandika kuhusu historia ya wazee wangu.

Soma chukua kile unachoona kinakufaa kile unachoona hakina maana kiache.
 
yaani Mkristu mwingine; kwanini asingependekezwa Skyes mwenyewe au Muislamu mwingine kama mzee wako au wazee wako wengine?

Paradox of a paradox!
Kwanini Waislam walipokuwa na nafasi ya kupendekeza au kuchagua mara zote tunaambiwa "walimchagua Mkristo"?Tafadhali tutegulieni hiki kitendawili.
 
Kila utachoandika hapa kitachambuliwa......hakuna kuchoka na wala hakuna vurugu mechi

Nakubali lakini inapendeza kusoma maandiko yaliyoandikwa kwa utulivu na mpangilio wa mantiki. Katika hali kama hiyo hata mimi nashawishika kusoma yote na kutoa fikra zangu.
 
Paradox of a paradox!
Kwanini Waislam walipokuwa na nafasi ya kupendekeza au kuchagua mara zote tunaambiwa "walimchagua Mkristo"?Tafadhali tutegulieni hiki kitendawili.

Yote hayo nimeeleza katika kitabu.

Tujitahidi kusoma kitabu kabla ya kuchangia vinginevyo tutakuwa tunarudia humu kwa humo.
 
Nadhani umepata kusikia watu wakisema "ilikuwa vurugu mechi." Tulipokuwa watoto tukicheza mpira Jangwani na Kidongo Chekundu na mechi hizi zilikkuwa kali na watazamaji walijaa uwanjani. Hiyo ndiyo ilikuwa Dar es Salaam ya wakati ule.

Basi hutokea tukapandwa na hasira na mpira ukavurugika kwa kuwa hatukuwa tukitandaza mpira bali kukwatuana.

Naona tumechoka na mjadala unapoteza mwelekeo unakuwa "vurugu mechi."

Naona baadhi yetu wangepumzika kidogo kwani hakika kazi yoyote ya kutumia akili si nyepesi kama watu wanavyodhani.

Naona hii afadhali maana umenijibu moja kwa moja kwa 'quote'. Shukran kwa uungwana, mzee umeghafilika kidogo hukutumia adab ya ilm na munkasha, inshallah tuendelee na hadhira kwa kadri mwenyezi atakavyotujaali.

Kama alivyosema Ogah jambo likitua hapa litachambuliwa tu hakuna jinsi, lau kama unaona vurugu mechi una hiyari wewe si mimi.
Tutatumia akili zetu kufikiri na kuuliza maswali au kutoa hoja hata kama hazipendezi, lakini ukweli hupendeza zaidi.

Kama kuna jambo la hatari ninaloliogopa maishani mwangu ni kutosimamia ukweli.
Sikubaliani hata kidogo na dhana ya kulishwa bila kutafakari, wala sipo tayari kusoma magazeti, vitabu, hadithi au hekaya na riwaya bila kutumia chembe ya akili, ingawaje pia ni hiari ya mtu kusoma Newsweek au Annur kwa mtazamo wake.
Tutachambua mada bila upendeleo, huruma au kumuonea mtu. Bado narejea kauli yako Mohamed 'Kama uongo ni haram hadi pale utakapotumika kusuluhisha' je uvumi unaangukia wapi?

Kumbuka hii mada ipo JF intellegence, na itapewa heshima yake kwa uchambuzi yakinifu na kamilifu. No more no less!

Tuendelee na mjadala.

Shukran.
 
samahani nakurupuka
je hiki kitabu kipo madukani au nikipate vipi?

Bila samahani.

Kitabu kinauzwa Tanzania Publishing House Samora Avenue na Ibn Azm Media Centre Msikiti wa Mtoro Dar es Salaam.

Hivi karibuni Insha Allah kitapatikana Kase Bookshop Arusha.
 
Hiki ni kitabu tu nimeandika kuhusu historia ya wazee wangu.

Soma chukua kile unachoona kinakufaa kile unachoona hakina maana kiache.

Nashukuru kwa ushauri.

Nami nakushauri hivi: Kama umeandika historia ya wazee wako basi edit uondoe kashfa dhidi ya Watu wengine. Hizi kashfa ndizo zina agitate watu hapa na kutufanya tutake kujua zaidi ilhali kumbe wewe umelenga kuandika historia ya wazee wako na hutaki mtu akuulize.
 
mbona kwenye maduka tajwa sijapata hiki kitabu, nielekeze kwingine au wasiliana nao mleta sred
 
Bila samahani.

Kitabu kinauzwa Tanzania Publishing House Samora Avenue na Ibn Azm Media Centre Msikiti wa Mtoro Dar es Salaam.

Hivi karibuni Insha Allah kitapatikana Kase Bookshop Arusha.
Kwnye hayo maduka niliona kitabu cha Salman Rashidie wa iran je wewe umewahi kikisoma?
 
Naona hii afadhali maana umenijibu moja kwa moja kwa 'quote'. Shukran kwa uungwana, mzee umeghafilika kidogo hukutumia adab ya ilm na munkasha, inshallah tuendelee na hadhira kwa kadri mwenyezi atakavyotujaali.

Kama alivyosema Ogah jambo likitua hapa litachambuliwa tu hakuna jinsi, lau kama unaona vurugu mechi una hiyari wewe si mimi.
Tutatumia akili zetu kufikiri na kuuliza maswali au kutoa hoja hata kama hazipendezi, lakini ukweli hupendeza zaidi.

Kama kuna jambo la hatari ninaloliogopa maishani mwangu ni kutosimamia ukweli.
Sikubaliani hata kidogo na dhana ya kulishwa bila kutafakari, wala sipo tayari kusoma magazeti, vitabu, hadithi au hekaya na riwaya bila kutumia chembe ya akili, ingawaje pia ni hiari ya mtu kusoma Newsweek au Annur kwa mtazamo wake.
Tutachambua mada bila upendeleo, huruma au kumuonea mtu. Bado narejea kauli yako Mohamed 'Kama uongo ni haram hadi pale utakapotumika kusuluhisha' je uvumi unaangukia wapi?

Kumbuka hii mada ipo JF intellegence, na itapewa heshima yake kwa uchambuzi yakinifu na kamilifu. No more no less!

Tuendelee na mjadala.

Shukran.

Waswahili tuna msemo, "Domo tindi maziwa kwa mwenye ng'ombe."

Hakika khiyari ni yangu.

Ndio pale hukaa kimya sijibu kwa ile mantiki kuwa kuwa kimya ni jibu tosha kwa mtu safii.
 
Kitabu kipo labda kama kilikuwa kimekwisha lakini kuanzia Jumanne vimekuwepo hapo Mtoro na Tanzania Publishing House.
 
Paradox of a paradox!
Kwanini Waislam walipokuwa na nafasi ya kupendekeza au kuchagua mara zote tunaambiwa "walimchagua Mkristo"?Tafadhali tutegulieni hiki kitendawili.

Yote hayo nimeeleza katika kitabu.

Tujitahidi kusoma kitabu kabla ya kuchangia vinginevyo tutakuwa tunarudia humu kwa humo.

Ndugu yangu,
Swali langu ni general na sitegemei kupata jibu kwenye Kitabu cha Historia ya Wazee wako. Maadam umeonyesha ndani ya kitabu chako kuwa mara zote waislam walichagua wakristo - Walimchagua "msomi " Nyerere wakaacha wasomi kama akina Fundikira na Mwapachu na umejitahidi kuonyesha tena Sykes akimchagua Chifu Makwaia kusoma hotuba aliyoiandika yeye Sykes kuhutubia UN, basi huu ni mtiririko (trend) uliyokuwepo. NAJIULIZA KWANINI?

Naamini watakuwepo watu wengine (nje ya wewe) watakaoweza kutupatia ufafanuzi ili tuoanishe na dhana ya kwenye kitabu chako. Swali halikuelekezwa kwako bali kwa hadhira hapa JF.

Kumbuka mimi nimekisoma kitabu hivyo naongea within the context.
 
Marytina we mchokozi sasa...hapa tunasoma na kujadili kitabu cha historia ya wazee wa mwandishi!
Ntatafuta kitabu alichoelekeza niwasome hao wazee wake.Ila anaonekana msomi mzuri wa vitabu kwa hiyo anaweza kunisaidia kunipa hints za vitabu vingine.

Au wewe WOS unaweza kunisaidia hili?waliniambia nitoe kitambulisho changu ndio waniuzie sasa sijui inakuwaje hapo
 
Nashukuru kwa ushauri.

Nami nakushauri hivi: Kama umeandika historia ya wazee wako basi edit uondoe kashfa dhidi ya Watu wengine. Hizi kashfa ndizo zina agitate watu hapa na kutufanya tutake kujua zaidi ilhali kumbe wewe umelenga kuandika historia ya wazee wako na hutaki mtu akuulize.

Minerva Publishers London na Phoenix Publishers Nairobi wasingekubali kuchapa kazi yenye matusi wala Cambridge Journal of African History isingefanya "review" ya kitabu changu. Wala "The East African" (Nairobi) wasingefanya serialisation kwa kazi ya ovyo.

Ingia katika google chakarika utapambana na haya yote.

Nimejitahidi kujibu mengi niliyoulizwa humu.

Fanya rejea utaona majibu yangu na vilevile wakati mwingine naeleza mengi hata yale nisiyoulizwa kwa ajili ya kutaka mtujue.
 
Ndugu yangu,
Hapa ndipo mnapokosea.Binafsi naamini kwa mfano harakati za uhuru wa nchi kama Tanganyika iliyokuwa Trusteeship ya UN chini ya Waingereza ulikuwa tofauti na Kenya ambapo "waliopigana kikwelikweli" dhidi ya Ukoloni wa Waingereza na kujipatia uhuru kwa kumwaga damu.Sina maana ya kubeza "harakati za Uhuru" wa Tanganyika lakini nataka kusema kuwa kuendelea kulilia credit kuhusu nani " alileta uhuru' kunanifanya nicheke kidogo. Besides, kipindi kile wimbi la kuyaachia makoloni unproductive lilikuwa linafagia kila mahali! Wawepo waislam au wapagani bado Uhuru ungekuja tu! Hivi tu tunataka kutoana roho kuhusu " nani alileta uhuru, ingekuwaje kama watu kweli wangeingia kwenye mapambano? Na ndio maana kwangu mimi na baadhi ya wengine hapa, tumeuliza mara nyingi - je katika " real" mapambano kama yale yaliyofanywa dhidi ya Wajerumani (na wajerumani wakaenda kuleta Mamluki wa kiislam akina Sykes kama Mwandishi wa hiki kitabu alivyoandika) je mchango wa wapagani, wakristo na hata waislam ulikuwaje?

Samahani kama nitasomeka ndivyo sivyo.

Kuhusu Ukatoliki wa Nyerere na kuhusishwa kwa Kanisa katika lawama na shutuma nzito hizi, hamuoni mnakosea? Ni kama kuhusisha vitendo vya mtu mmoja muislam na Uislam ( assuming kweli mtu huyo alitumia dini/imani yake kufanya dhuluma au uonevu)!

WoS,

Naona hujaisoma post yangu uliyoijibu kwa vizuri, hutokuta humo neno kudai "uhuru", sijui umelitowa wapi ukalihusisha na post yangu?

Tuliweke hilo sawa kwanza halafu tuendelee mengine.
 
Ntatafuta kitabu alichoelekeza niwasome hao wazee wake.Ila anaonekana msomi mzuri wa vitabu kwa hiyo anaweza kunisaidia kunipa hints za vitabu vingine.
Au wewe WOS unaweza kunisaidia hili?waliniambia nitoe kitambulisho changu ndio waniuzie sasa sijui inakuwaje hapo

Kitambulisho cha nini katika kununua kitabu?

Mbona tunauza vingi tu na tunashukuru kwa hilo kama Ibn Hazm wamedai kitambulisho (na siamini) basi nenda TPH.
 
Ndugu yangu,
Swali langu ni general na sitegemei kupata jibu kwenye Kitabu cha Historia ya Wazee wako. Maadam umeonyesha ndani ya kitabu chako kuwa mara zote waislam walichagua wakristo - Walimchagua "msomi " Nyerere wakaacha wasomi kama akina Fundikira na Mwapachu na umejitahidi kuonyesha tena Sykes akimchagua Chifu Makwaia kusoma hotuba aliyoiandika yeye Sykes kuhutubia UN, basi huu ni mtiririko (trend) uliyokuwepo.NAJIULIZA KWANINI? Naamini watakuwepo watu wengine (nje ya wewe) watakaoweza kutupatia ufafanuzi ili tuoanishe na dhana ya kwenye kitabu chako.Swali halikuelekezwa kwako bali kwa hadhira hapa JF.

Kumbuka mimi nimekisoma kitabu hivyo naongea within the context.

Abdu Sykes alimtaka Chief Kidaha ajiunge na TAA wamchague kuwa rais siyo kusoma memorandum.
 
Mohamed,

Nimejaribu kupitia baadhi ya maandiko yako (kwa bahati mbaya sijapata kitabu chako kizima). Nimeona umeweka msisitizo mkubwa kwa kwa Abdulwahid (hata title ya kitabu inashiria hivyo). Kwenye maandiko yako mengi unajaribu kumjenga Abdul zaidi kuliko wazee wetu wengine.

Kwa nini umeamua kumwacha Kleist kwa mfano, baba yao kina Abdul na Ally, ambaye ndio aliyeanzisha TAA (1929) pamoja na wajumbe wengine 8? Nina wasiwasi inawezekana unafanya kosa lilelie ambalo unasema wanahistoria wengine wamefanya kwa kuanza na TAA ya Nyerere badala ya ile ya Abdul.

Na kwa mantiki hiyo hiyo mtu mwingine anaweza kuuliza kwa nini tuanzie kwa Kleist na sio wazee wengine wa kabla yake? Nadhani ndio sababu pengine vitabu vingi vya historia mara nyingi vinaweka muda unaozungumziwa (kuanzia 18xx - 19xx etc)
 
MAISHA NA NYAKATI ZA ABDULWAHIS SYKES (1924 -1968)

Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza katika Tanganyika na Mohamed Said

Pitio la Kitabu

Kitabu hiki kilipochapwa kwa mara ya kwanza 1998 kwa Kiingereza nchini Uingereza na kilipoanza kuzagaa katika maktaba na maduka ya vitabu mjini London yanayouza vitabu kuhusu Afrika Watanzania wengi waliokuwa Uingereza walisisimuliwa na yale yaliyokuwa ndani ya kitabu hiki. Kubwa zaidi ilikuwa kule kufunuliwa kwa mara ya kwanza kuwa kumbe TANU chimbuko lake si Julius Nyerere bali ni marehemu Abdulwahid Sykes. Hii ilikuwa habari mpya kwa wengi hasa ikizingatiwa kuwa Nyerere mwenyewe hakuwahi kumtaja Abdulwahid Sykes kama mwenzake katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Hili lilikuwa la kwanza. Kitu cha pili kilichosisimua wasomaji ni kuwa mwandishi kwa kutulia kabisa alionyesha bila woga na kutafuna maneno kuwa TANU kilikuwa chama kilichojengwa katika migongo ya Waislam. Hili alilishaijisha kwa kueleza wazalendo waliokuwa bara ambao kwa umoja wao na wengi wao wakiwa Waislam walipambana na ukoloni wa Kiingereza.

Kubwa zaidi la kusisimua ilikuwa kitabu kilieleza bila kupepesa macho au kutafuna maneno njama alizofanya Nyerere kwanza kumfuta Abdulwahid Sykes katika historia yake binafsi, TANU na katika harakati za kudai uhuru. Lakini kilichotibua sege la nyuki ni pale katika kuhitimisha kitabu mwandishi alipoweka wazi mipango ya Nyerere akishirikiana na Kanisa Katoliki baada ya uhuru kupatikana kupanga njama za kuzuia maendeleo ya Waislam. Katika kipande hiki msomaji atakutana na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa mufti wa Tanganyika na Zanzibar na mwanasiasa shupavu. Msomaji ataziona juhudi za Sheikh Hassan bin Amir katika kupambana na njama za Nyerere na Kanisa Katoliki na nini kilimfika msomi huyu maarufu wa Kiislam. Kwa wakati ule Nyerere akiwa hai ilihitaji ujasiri mkubwa kwa yeyote yule kusema au kuandika hayo.

Nakala za kitabu zilifika Tanzania na kila aliyesoma alipatwa na mshtuko mkubwa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na nje yake. Kitabu kiliwaudhi wapenzi wa Nyerere na wapo waliomwendea kwa kutaka afanye jambo kukomesha uongo wa mwandishi. Wengine hawakuamini kuwa huyo anayejiita Mohamed Said kama kweli yupo. Wengine walitaka kujua kama kweli akina Sykes na baba yao ndio waasisi wa vyama vya Waafrika katika Tanganyika katika 1929 hadi 1954 TANU ilipoasisiwa. Hii ilikuwa bahari kubwa kwa wapenzi wa Nyerere ambao wasingeweza kuogelea bila ya msaada wake Baba wa Taifa. Mawimbi ya bahari hii yalikuwa marefu na yakija kwa kasi. Juu ya haya yote Waswahili wana msemo penye ukweli uongo hujitenga. Nyerere asingeweza kuthubutu kukana mchango wa marehemu Abdulwahid kwake yeye binafsi na kwa TANU. Abdulwahid ndiye aliyempokoea Dar es Salaam ile ya miaka ya 1950 na akamjulisha kwa wenyeji wa mji. Wapenzi wa Nyerere hadi leo ukiwauliza Nyerere alisema nini kuhusu ukweli kuwa si yeye aliyeasisi TANU wamekuwa kimya.

Msomi maarufu wa Chuo Kikuu cha Cambridge John Illife ambae ameandika sana historia ya Tanganyika alikasirishwa na msimamo wa mwandishi khasa pale aliposema kuwa inastaajabisha kuwa Illife ingawa alitegemea nyaraka za akina Sykes katika kuandika historia ya African Association inastaajabisha hakuona umuhimu wa kutaka kumhoji marehemu Abduwahid aliyekuwa katibu na rais wake kati ya 1951 hadi 1953. Akiandika pitio la kitabu hiki katika Cambridge Journal of African History Illife alimshambulia mwandishi katika njia ambayo haikuwa staili yake msomi mkubwa kama yeye. Illife alikuwa ameghadhibishwa kwa kuambiwa katika kitabu kuwa alimzuia mwanafunzi wake katika Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa 1969, Daisy Sykes ambae alikuwa binti ya Abdulwahid asiandike maisha ya baba yake. Daisy wakati huo msichana mdogo alikuwa amekasirishwa na jinsi TANU na magazeti yake yote, The Nationalist chini ya uhariri wa Benjamin Mkapa na Uhuru yalivyoshindwa kumwandika baba yake kwa hadhi aliyostahili. Magazeti hayo yaliripoti kifo cha Abdulwahid Sykes kwa kuwa Nyerere alikwenda mazikoni. Hapakuwa na jingine. Brendon Grimshaw ambae alikuwa Mhariri Mkuu wa The Tanganyika Standard na akimfahamu vyema Abdulwahid ndiye aliyendika tanzia ya maana katika Sunday News akasema kuwa Nyerere asingelifika pale alipofika kama si kwa msaada wa Abdulwahid Sykes na ni juhudi za ukoo wa Kleist ndiyo uliowezesha watu wa Tanganuyika kuwa na chama cha siasa. The Standard na Sunday News wakati ule lilikuwa gazeti huru halikuwa na hofu ya Nyerere. Hii ilikuwa mwaka 1968.

Kilipotoka kitabu hiki mwaka 1998 walikuwepo watu walioona ukweli wa kuwa historia ya TANU bado haijaandikwa na kuna baadhi ya shutuma zilizoelekezwa kwake Nyerere ni muhimu yeye mwenyewe akazijibu akiwa hai kwa faida ya jamii isijesemwa kuwa kasingiziwa, walimsubiri afe ndipo wamzushie la kumzushia. Mmoja wi wa kundi hili la pili alikuwa marehemu Prof. Haroub Othman. Yeye alimkabili Nyerere uso kwa macho na kumuomba atoe majibu kujibu shutuma za waandishi wawili. Kwanza ajibu shutuma za Sheikh Ali Muhsin Barwani aliiyekuwa kiongozi wa Zanzibar Nationalist Party (Hizbu) katika kitabu chake Conflict and Harmony in Zanzibar na kitabu cha Mohamed Said The Life and Times of Abdulwahid Sykes (19241968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika. Sheikh Ali Muhsin akimtuhumu Nyerere kwa kupeleka mamluki Zanzibar kuipindua serikali ya wananchi na Mohamed Said akimtuhumu kwa chuki dhidi ya Waislam na kupotosha historia ya uhuru wa Tangnayika. Prof. Haroub alimshauri Nyerere kuwa njia nzuri ya kuiweka historia yake na uhusiano wake na Waislam sawa ni kwa yeye kuandika historia ya maisha yake. Hadi Nyerere anaingia kaburini hiili halikufanyika.

Kitabu hiki ni muhimu kwa Waislam na wananchi wote kwa ujumla kukisoma na kuwahimiza watoto wao nao wakisome wapate kujifahamu na kufahamu changamoto za udini na chanzo chake. Ndani ya kitabu hiki mwandishi amejitahidi kukusanya mashujaa waliotupwa waliopigania uhuru wa Tanganyika hata kabla hawajasikia jina la Nyerere wala kuona sura yake, wazalendo kama Hassan Suleiman na Juma Ponda wa Dodoma. Wazalendo waliohutubia mikutano ya hadhara na kuhamasisha watu kudai uhuru hata Nyerere hawamjui kama Titi Mohamed na wengine wengi kutoka katika majimbo ya Tanganyika. Ukikianza kitabu hiki huwezi kukiweka chini hadi umefika mwisho.

Kitabu hiki kinapatikana Ibn Hazim Bookshop Mtoro na Manyema na Tanzania Publishing House, Samora Avenue.
Ni taarifa nzuri maana kwenye ukweli uongo hujitenga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom