Kitabu Kinachofichua utapeli katika baadhi ya Makanisa

Kitabu Kinachofichua utapeli katika baadhi ya Makanisa

Kafichue wauza unga huko unakoelekea unataka kuokota makopo

Umejuaje kama hayo makanisa kama hayatumiki kwenye biashara ya madawa ya kulevya? Hawezi kuokota makopo kwa sababu ya kufichua majambazi yanayotumia "neno"!!!!! Japo sidhani kama amefanya utafiti wa ndani!
 
Kamanda, heshima yako! Naamini Roho wa Mungu amekuongoza kufanya hilo. Uandike ukiwa na ushahidi kamili.... Tena uweke jinsi wanavyo kaidi maandiko ili tujue the story behind the glory kama Mzee Mwanakijiji anavyosema
 
Umejuaje kama hayo makanisa kama hayatumiki kwenye biashara ya madawa ya kulevya? Hawezi kuokota makopo kwa sababu ya kufichua majambazi yanayotumia "neno"!!!!! Japo sidhani kama amefanya utafiti wa ndani!
Kwa mawazo yako huko kanisani ndiko kuna majambazi waliopitiliza? nchi hii ina matatizo mangapi na je hao watafuna sadaka ndio wanaosababisha maandamano na ngumi bungeni kila uchao? kama haokoti makopo tusubirie kwanini tuandikie mate ukihukumu utahukumiwa
 
Njaa tu ndo inayo kusumbua...Njaa mbaya sana!
  • Sio njaa, Ni kiu yake kutaka watu wafahamu ukweli uliojificha, Mtu paka kufikia kutoa kitabu yawezekana kuna utafiti alioufanya,na bila shaka Kuna jambo ambalo watu wapaswa kufahamu.
 
Kwa mawazo yako huko kanisani ndiko kuna majambazi waliopitiliza? nchi hii ina matatizo mangapi na je hao watafuna sadaka ndio wanaosababisha maandamano na ngumi bungeni kila uchao? kama haokoti makopo tusubirie kwanini tuandikie mate ukihukumu utahukumiwa

Hayo majukumu yote unataka umtwike Kamanda Kazi pekeyake? Na wewe kamata kalamu andika unachoona, yeye anatimiza wajibu wake kufichua majambazi ya upande mmoja, na wewe timiza wajibu wako kwa kufichua upande unaoona! MAKANISA NI UJAMBAZI, AFADHALI HATA MISIKITINI, MAKANISANI KUMEJAA DHULUMA NA WATU KUJIFANYA MIUNGU!
 
Last edited by a moderator:
View attachment 111836
WAVUVI WA PESA
Niko mbioni kutoa kitabu hicho. Kitafichua utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu!
Stay tuned!
0qtb.jpg

  • Ndugu tutarajie lini kitatoka hiki kitabu?
 
Mkuu piga kazi kufichua hawa matapeli wanaotumia jina la mungu kws kujifanya wachungaji.consider me as the first buyer when it is out.achana kabisa na hao mabwege wanaotaka kukuvunja moyo.
 
Hilo kwenye cover ni kasri la Mama Lwakatare nini?

Maana huyu katika hicho kitabu anatakiwa kuwa na chapter yake peke yake kuelezea alivyojipenyeza kwenye siasa, academia na dini.
 
View attachment 111836
WAVUVI WA PESA
Niko mbioni kutoa kitabu hicho. Kitafichua utapeli unaofanywa na baadhi ya watu wanaojiita watumishi wa Mungu!
Stay tuned!

Lakini hiyo cover mkuu haijatulia sana, tafuta mtu akufanyie design nzuri ya cover!
Unaweza kudesign picha ya mchungaji aliyevalia suti za gharama, kanisa amelipamba kwa dhahabu, bodyguards wenye vitambi, huku akihubiria watu wenye njaa vibaya mno, wamevaa ovyoovyo wako peku, wengine wamejipanga kwenye foleni wakikung'uta mifuko yao kutoa sadaka! Itapendeza sana mkuu!
 
Dah! Kaka hiyo cover inapiga kelele. Yaani inatoa hata hamu ya kusoma kitabu. Mtafute mtu aitengeneze vizuri.
 
Hongera mkuu naamini itaungwa mkono na waaopenda haki ,ukiona kuna dalili ya unga huko niambie tuanze kuwashughulikia ,hata kule zanzibar wamedhulumiana na wanamwagiana tindikali
 
Back
Top Bottom