Kitabu cha Outliers na elimu yetu

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Hiki kitabu Outliers kimeandikwa na Malcom Gladwell. Kinaelezea kwanini watu hufanikiwa. Kuna sehemu kinazungumzia kuhusu mafanikio ya kielimu. Anasema Waasia wanaonekana wana akili sana sababu wana muda mwingi wa kusoma kuliko watu wengine.

Anasema kwa mwaka mwanafunzi wa Marekani anasoma siku 180. Mwanafunzi wa Korea kusini anasoma siku 220 kwa mwaka wakati mwanafunzi wa Japan anasoma siku 243 kwa mwaka.

sasa nikajiuliza mwanafunzi wa Tanzania anasomaje, kuna siku 60 za likizo ya mwezi wa sita na kumi na mbili. jumamosi na jumapili kwa mwaka ni siku 106. kuna wiki moja ya pasaka na wiki moja ya mwezi wa 9 jumla siku kama 10 ukitoa jmosi na jpili. kuna sikukuuu tufanye siku 5 hivi. jumla ni siku 171. ukichukua siku 365-171 unapata siku 194 kwa mwaka. tofauti ya siku 49 na japan. Huu ni muda mwingi sana wa kujifunza.

Aliendelea kuandika kuwa huko bronx New York. Ni asilimia 16 tu ya wanafunzi wanaweza kufanya hesabu vizuri. Wakaanzisha shule za majaribio. Shule hizi huanza saa moja na nusu hadi saa kumi na moja jioni. Hapo unapewa na Homework za kutosha. Jumamosi darasa linaanza saa 3 asubuhi ha saa 7 mchana. Likizo ilipunguzwa kwa wiki tatu na siku za likizo darasa lilianza saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Matokea yalikuwa asilimia 84 ya wanafunzi waliweza kufanya hesabu vizuri na 80% walifanikiwa kufika chuo kikuu. Ila hili linahitaji kupata chakula shuleni.

Kwa hiyo niliona kwamba Tanzania watoto hawasomi vya kutosha. Kwanza kuna upungufu wa waalimu na muda mchache wa kusoma unaongezeka juu. Mwanafunzi anaanza saa mbili asubuhi mpaka nane mchana. Masaa sita tu ya kusoma.

Naonelea tuongeze muda wa kusoma labda toka moja na nusu hadi saa kumi jioni. masaa kama 8 na nusu. Tuongeze siku za kusoma walau zifike 230 kwa mwaka. Pia tujitahidi hata uji upatikane shuleni.

Malcom Lumumba , Rebeca 83 Nalendwa James Comey Wick mitale na midimu
 
Tuna changamoto nyingi sana katka mfumo wetu wa turathi ya maarfa kias kwamba kutatua changamoto moja au mbili ilhali zilizobak nazo n tegemezi kataka kuamua hatma ya urithi wa kimaarfa ...sidhani kama ni sahh....

Hao wa shule za majaribio za marekani walifanyia utafit mfumo wao wa urithishanaji wa maarfa(Elimu) wakaona Tatizo kuu n suala la muda...ili walitatue vzur ni lazma wadhibit na mfumo wa lishe(ni jambo muhimu sana...kuna uzi wa kitafit humu JF ambao unaegemeza Lishe (Upatikanaji wa chakula na IQ ya mtu au jamii fulan kwa mnyumbuliko wa kijiografia) ndio maana waliweza kufanyia experiment hypothesis yao na ikazaa matunda. Hopefully Iliwezekana tu kwasabab factors nyingne zilikuwa n zenye kujitosheleza.

Asante kwa mada nzuri!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3

Kweli mkuu usemayo tatizo la elimu lina mkusanyiko wa matatizo mengi, ukianza kusolve moja moja ni hatua japo hautatatua tatizo lote. Lishe duni inadumaza uwezo wa kujifunza, fikiria mtu mwenye uwezo duni wa kujifunza sababu ya lishe duni halafu anakuwa na muda mfupi zaidi wa kujifunza kuliko Mjapan mwenye ana afya njema ya akili na kila kitu.
 
Kuongeza mda sio suluhisho, suluhisho ni kuanzisha semina zitakazo wapa wanafunzi mbinu za kusoma na kupenda kujituma, kwani huo mda wa free mwanafunzi anaweza akachimba vitu vingi sana, na kitu utakachokitafuta mwenyewe ni ngumu kusahau kuliko kufundishwa mda mrefu kuna kuchoka pia na mwanafunzi akakosa hata mda wa kupitia kile anachofundishwa na kufeli kukawa palepale, hivyo mda wa kutosha wa kupumzisha ubongo ili uweze kuwa fit kugain kitu kipya ni muhimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Moja ya mambo hiki kitabu kilikataa ni kuwa umuhimu wa muda mrefu wa watoto kupumzika ili akili ijichaji na kushika mambo.

Huyo mtoto wa kuanza shule saa 1 na nusu hadi saa 11 jioni alikuwa na miaka 12 tu. Huyu hata ukimpiga semina hawezi kuelewa. na kwa kumuangali unaweza sema hawezi kuhimili masaa mengi ya shule na homework kibao, ikaonekana inawezekana.
 
Mtoto kama huyo sio lazima kumkazania sana ila kuanzia level za highschools anakuwa tayari amejielewa, na semina hizi pamoja na kula nzuri zitamsaidia, ila kwa hao wa primary schools unaweza ukamsimamia kama mzazi au mlezi au mwalimu kwa kumkumbusha kujisomea na kufanya homework na akafanya vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
Yap, primary unawwza msimamia vizuri. System kama hii nzuri ikianzia pale sekondari kidato cha kwanza mtu anapoanza kujifunza vitu vikubwa.
 
Mada nzuri sana hii.
Lakini nadhani kabla ya kuongeza siku na masaa katika elimu yetu, cha kwanza ni kufumua mfumo wa elimu ili ubebe maana hasa ya elimu.

Elimu maana yake ni kufuta ujinga na kujenga nuru fulani kwenye akili lakini pia kuuwezesha uwezo wa ndani alioumbwa nao mtu ukae kwenye shape uweze kumnufaisha yeye alio nao lakini pia wale wanaomzunguka.

Mtu kazaliwa kwa mfano na kipaji cha muziki, anakwenda kusoma anapelekwa kusoma O level shule ya ufundi Tanga Tech, anasoma kozi za umeme, mabomba, kujenga matofali, magari mpaka kupiga randa.

Baadaye kijana huyo anafaulu kwa division one ya points 14 anakwenda kusoma PCM shule labda Milambo pale kwa miaka 2 tena.
Baada ya hapo anafaulu kwenda chuo kikuu anachukua kozi za Computer Science.

Sasa jiulize.
1.Kipaji chake cha muziki elimu yake ya miaka zaidi ya 19 mbona hakijawahi kuguswa na mfumo wa elimu??
2.Kama mwisho ulikuwa ni computer Science kwa nini kumsumbua kwa miaka yote hiyo anapiga randa na ufundi mabomba??, kwa nini asingemaliza tu darasa la saba pale pale anaanza kupiga kozi ndogo ndogo za computer huku anaendelea na masomo mengine ya msingi kama Civics, Basic Maths, History, Geography na Biology??

3.Kwa nini alienda high school kukariri ma-formula ya Organics Chemistry kumchosha tu ubongo??, kwa nini miaka hiyo miwili asingepiga diploma ya Computer Science ili akifika chuo kikuu awe ameiva vya kutosha??, badala ya kuanza kusoma what is a computer chuoni aanze kujifunza kozi za programming na hacking na nyinginezo ngumu ngumu??

Utakuta kuwa tatizo sio tu masaa na wingi wa masiku ya kukaa darasani, tatizo elimu yetu imejaa makoro koro mengi ambayo hayamsaidii kijana zaidi ya kuchosha tu ubongo wake.
 
Hapa naona kuna hatari ya kurudia kosa lile lile ambalo tumekua tukilifanya kila siku. Kusema kwamba marekani au Japan wamefanya hivi wakafanikiwa, kwahiyo na sisi tukifanya kama wao tutafanikiwa! Hii sio sawa.
Kinachotakiwa kufanya ni kujifunza kutoka kwa wenzetu kisha tuangalie sisi tufanyeje kwa mazingira na hali halisi ya hapa kwetu ili tuweze angalau kupiga hatua.
 
Mada nzuri sana hii.
Lakini nadhani kabla ya kuongeza siku na masaa katika elimu yetu, cha kwanza ni kufumua mfumo wa elimu ili ubebe maana hasa ya elimu.

Elimu maana yake ni kufuta ujinga na kujenga nuru fulani kwenye akili lakini pia kuuwezesha uwezo wa ndani alioumbwa nao mtu ukae kwenye shape uweze kumnufaisha yeye alio nao lakini pia wale wanaomzunguka.

Mtu kazaliwa kwa mfano na kipaji cha muziki, anakwenda kusoma anapelekwa kusoma O level shule ya ufundi Tanga Tech, anasoma kozi za umeme, mabomba, kujenga matofali, magari mpaka kupiga randa.

Baadaye kijana huyo anafaulu kwa division one ya points 14 anakwenda kusoma PCM shule labda Milambo pale kwa miaka 2 tena.
Baada ya hapo anafaulu kwenda chuo kikuu anachukua kozi za Computer Science.

Sasa jiulize.
1.Kipaji chake cha muziki elimu yake ya miaka zaidi ya 19 mbona hakijawahi kuguswa na mfumo wa elimu??
2.Kama mwisho ulikuwa ni computer Science kwa nini kumsumbua kwa miaka yote hiyo anapiga randa na ufundi mabomba??, kwa nini asingemaliza tu darasa la saba pale pale anaanza kupiga kozi ndogo ndogo za computer huku anaendelea na masomo mengine ya msingi kama Civics, Basic Maths, History, Geography na Biology??

3.Kwa nini alienda high school kukariri ma-formula ya Organics Chemistry kumchosha tu ubongo??, kwa nini miaka hiyo miwili asingepiga diploma ya Computer Science ili akifika chuo kikuu awe ameiva vya kutosha??, badala ya kuanza kusoma what is a computer chuoni aanze kujifunza kozi za programming na hacking na nyinginezo ngumu ngumu??

Utakuta kuwa tatizo sio tu masaa na wingi wa masiku ya kukaa darasani, tatizo elimu yetu imejaa makoro koro mengi ambayo hayamsaidii kijana zaidi ya kuchosha tu ubongo wake.

Na kiukweli hapa ndio wenzetu wanapotupiga gap. Ukikaa darasa moja mfano na wazungu, utagundua kua hawa jamaa sio kwamba wana akili sana la hasha! Ila wao ni perfectionists kwenye kila wanachokifanya kwa maana ya kwamba mtu anaanza ku specialize kwenye ka eneo kamoja tu tangu akiwa mdogo. Ndio maana unakuta kijana wa miaka 16 aliebobea kwenye computer huwezi kumlinganisha na PhD holder wa hapa Tz. Ila ukimuuliza mambo nje ya taaluma yake ni sifuri. Hapa kwetu unadonoa donoa kila kitu mwisho wa siku hakuna unachokijua.
 
Ni kweli mkuu.
Nafikiri mfumo wetu wa elimu ulijengwa na serikali ya Nyerere enzi hizo kwa sababu ya uhaba wa wataalamu kwenye kila sekta.
Kwa hiyo Mwalimu alichofanya ni kuhakikisha mtu anafahamu mambo mengi kwa wakati mmoja hata kama ni kwa rasha rasha ili kupata angalau watu watakaoisaidia nchi kwa wakati wake.
Maana hata kujua kusoma na kuandika tu lilikuwa ni tatizo kwa karibu 80% ya population nzima.

Sasa kwa kuwa kizingiti hicho tulishakivuka, inabidi tuanze kujenga msingi mwingine mpya utakaosisitiza quality inayotokana na elimu zaidi ya quantity.

Kwamba , kwa kuwa nchi imeshakuwa na watu wengi ni bora kufahamu mambo machache unayoyamudu kwa efficiency kubwa kuliko kuwa na rundo la mambo unayoyafahamu nusu nusu.
 
Si ungi mkono hoja kwahyo kwa maelezo yako kukaa sans class ndo kufaulu na kuongeza maarfa? Usfananishe marekani na bongo br,,mifumo Ni tofauti Sana hslaf kichwa kinajilazimisha kuelewa kutokana na Hali inayojitokeza mda huo..tuliowahi kusoma tunajuaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom