Tanesco Iringa mjini hali ni mbaya

moe junior

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
894
856
Nikiri kufahamu uwepo wa mgao wa umeme nchi nzima kutokana na sababu hizi au zile kwa namna wanavyozielezea wahusika (TANESCO) na waziri mwenye dhamana.ILA KUNA HII KUBWA KULIKO.

Nipo Iringa mjini kwa likizo yangu ya mwaka, nimefika hapa nyumbani kata ya Igumbilo hali niliyoikuta kiukweli sijawahi kuiona popote nilipopita kuanzia DSM ninapoishi na mikoani ninapokwenda kikazi.

Nina wiki ya tatu hapa mjini, kila siku saa moja kamili asubuhi umeme unakatwa na kurudishwa saa kumi na mbili na nusu jioni.

Utakaporudi sio guarantee kuwa nao, baada ya nusu saa unaweza kukatwa tena ukarudishwa usiku sana na ikifika saa moja kamili asubuhi unakatwa tena. So kwa hesabu zangu za haraka ni wastani wa masaa sita (06 hrs) ya kuwa na umeme katika masaa 24 ya siku.

Ni mara yangu ya pili kutoa malalamiko juu ya uongozi wa TANESCO hapa Iringa mjini hasa kwa kata hii ninayoishi.

Nadhani tatizo la TANESCO halikuwa maharage Chande, ila wapo watendaji huku mikoani wanaofanya kazi kwa matakwa yao na sio kitaalamu au kwa maelekezo wanayopewa.

TANESCO

Sent from my Nokia C1 using JamiiForums mobile app
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tupatie namba ya simu tuweze kufungua taarifa kuhusu changamoto hiyo.^OK
 
Kuna mgao mkali maeneo mengi ya miji midogo, sema kwakuwa wanaharakati na vyombo vya habari vingi vipo majijini ambako wamefumbwa macho kwa kutokatiwa umeme husikii kelele. ingawa wao wanakanusha kwa nguvu zote kwamba hakuna mgao!
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa wetu na pole kwa changamoto hiyo, tafadhali tupatie namba ya simu tuweze kufungua taarifa kuhusu changamoto hiyo.^OK
Ehhh

Ova
 
Back
Top Bottom