Kitabu cha Outliers na elimu yetu

Kitabu cha Outliers na elimu yetu

Kinachofundishwa shule bado hakina mahusiano na maisha halisi ya mtanzania.

Ship building in Japan
Fishing in Norway
Yaani mpaka kesho bado tunaulizana kuhusu mistari ya kontua iwapo ikikaribiana nini kinatokea
Wenzetu watoto wapo free sio kama kwetu mtoto akirudishuleni anaingia jikoni kupika,kwenda shambani,ngombe nk. Sidhani kama itawezekana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusoma masaa mengi bado sio ishu. Vipi kuhusu maarifa yanayotolewa katika hayo masomo. Mfumo wetu unahitaji marekebisho makubwa tena makubwa sana.

Lakini ndio tunazidi kudidimia siku baada ya siku. Ni janga kuu la taarifa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoa mada -- amemaanisha kuwa mfumo mzima wa elimu hauko sawa".. ikiwa pamoja na wanafunzi kuwa na muda mchache wa masomo .... Yaani huo muda anao uzungumzia kuwa uongezwe ni sehemu pia ya mfumo ambao unapaswa kubadilishwa kama ambavyo wewe umesema hapa"......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kinachofundishwa shule bado hakina mahusiano na maisha halisi ya mtanzania.

Ship building in Japan
Fishing in Norway
Yaani mpaka kesho bado tunaulizana kuhusu mistari ya kontua iwapo ikikaribiana nini kinatokea

Sent using Jamii Forums mobile app
Kweli mkuu,unajazwa makorokoro hayana faida yoyote katika maisha ndomana hata ukimaliza chuo huna unachojua zaidi ya kusubir kuajiliwa na ukiajiliwa unaweza kuajiriwa kitu ambacho hujasomea mradi we unataka pesa basi kanyaga twende njia ya chooni isiote nyasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Thanks mkuu kwa mada nzuri,,

Mimi naona mazingira Yao ni tofauti na ya kwetu...hivyo kuiga kila kitu itakua ngumu kidogo kwenye utelekezaji,,,

However,tumejua masaa mengi yakusoma kuna correlate na akili..ingawa (lifecoded ) atabisha...lol

Kwa mazingira yetu two hours extra ni possible

Hii haimaanishi iwe shuleni tu,

Wazazi wanaweza kuchukua active role kuhakikisha watoto wao wanapata kusoma two hours independent study...

Na shule za Government (boarding) watilie mkazo kwenye hii extra two hours …

Shule za Private kama Feza,Kifungilo,Marian etc..wana haya masaa ya kusoma jioni (Prepo)

Nadhani na shule za Government zingetilia mkazo,watoto wengi wangefaulu Zaidi..
 
Mkuu, wazo la kuongeza muda wa kusoma ni zuri, lakini halita tatua matatizo ya mfumo wa elimu yetu. Kuna mambo mengi ya kuangazia ili tupate wahitimu bora na wenye uwezo wa kushindana kimataifa, baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo;
Ubora wa walimu: hapa inabidi tubadili aina ya walimu watakao fundisha watoto wetu, vyuo vya ualimu vidahili wahitimu wa sekondari waliofaulu sana, mfano waliopata dvn I na II, yaani walimu wote, iwe msingi au sekondari tofauti na sasa, unakuta mwalimu hawezi kufundisha kabisa, mpaka yeye mwenyewe anajijua.
Elimu yetu itolewe kulingana na mazingira: kwa kiasi kikubwa mazingira yanaathiri uwezo wa kiakili wa mtu, mtazamo na tabia. Ifike mahali elimu yetu itolewe kulingana na mazingira husika, kwa mfano mikoa ambayo imepakana na mito, maziwa na bahari mtaala wao ubebe mafunzo ya uvuvi, kilimo cha umwagiliaji nk, sio saizi mwanafunzi aliyopo Morogoro unamuuliza, " why fishing industries failed in japan"?. Pia wanafunzi waliopo ktk miji ya kibiashara, mtaala wao uhimize mada zinazohusu biashara.
Mishahara: ni wazi kuwa kada ya elimu inadharaulika sana, kuna walimu mimi nawajua, wanaona aibu kuvaa yale mat-shirt yao ya CWT kwa sababu wanajua kuwa wanadharaulika. Mshahara haukidhi mahitaji, kila mtu ni bosi wako, mkuu anakutisha, mtendaji anadai hela ya dawati, diwani anataka hela ya Mwenge, kote huko ni vitisho mwanzo mwisho. Cha ajabu zaidi unamfundisha mwanafunzi anafaulu, baada ya miaka3, ana ajiriwa na kukuzidi mshahara! daaa.
Mfumo wa elimu: kama tuna hitaji mabadiliko makubwa kwenye elimu yetu, lazima tubadili aina ya mfumo wa elimu tulionao. Elimu yetu haimuandai mhitimu kujitegemea, "it is too bookish". Wanafunzi wanatakiwa wapate elimu kwa vitendo sio kukalili tu, kwa mfano standard seven leaver wa Japan na China anauwezo wa kutengeneza radio, lkn hapa kwetu kiwango cha ugunduzi/uvumbuzi hakilingani na cheti cha mtu.
Lugha ya kufundishia: hili ni tatizo kubwa ktk mfumo wetu wa elimu, yaani mwanafunzi anajifunza masomo yote kwa kiswahili, isipo kuwa somo la kiingereza akiwa shule ya msingi. Akianza sekondari anajifunza masomo yote kwa kiingereza, isipokuwa somo la kiswahili tu. Hapa wanafunzi huanza kukalili tu wanachofundishwa na sio kukielewa. Mbaya zaidi hicho kiingereza hata walimu hawawezi kukitumia vizuri kufundishia. Ushauri wangu serikali ichague lugha moja tu, kama ni kiswahili au kiingereza , basi kitumike tokea S/ msingi hadi Sekondari.
Tuache kupenyeza siasa kwenye elimu: mbali na ukweli kwamba falsafa ya elimu mpaka sasa haijulikani kwa walio wengi, siasa imetawala elimu ya Tz. Kila Rais na waziri wa elimu anakuja na kipaumbele chake mpaka tunapoteza dira. Hapa serikali iwaache wataalamu husika wapange na kushauri mambo mbali mbali kuhusu elimu, wanasiasa wabaki na kazi yao ya kudanganya.
Uwekezaji katika elimu: naipongeza serikali kwa kuwekeza katika elimu, lakini isifanye uwekezaji nusu nusu kwa mfano, unatoaje elimu bure wakati nusu ya wanafunzi wanakaa chini. Itenge bajeti ya kutosha ktk wizara ya elimu, vyuo mbali mbali vifanye tafiti za kutosha ilikutatua changamoto zilizopo ktk mfumo wa elimu yetu, miundo mbinu na masilahi ya walimu iboreshwe.
 
Hiki kitabu Outliers kimeandikwa na Malcom Gladwell. Kinaelezea kwanini watu hufanikiwa. Kuna sehemu kinazungumzia kuhusu mafanikio ya kielimu. Anasema Waasia wanaonekana wana akili sana sababu wana muda mwingi wa kusoma kuliko watu wengine.


Anasema kwa mwaka mwanafunzi wa Marekani anasoma siku 180. Mwanafunzi wa Korea kusini anasoma siku 220 kwa mwaka wakati mwanafunzi wa Japan anasoma siku 243 kwa mwaka.

sasa nikajiuliza mwanafunzi wa Tanzania anasomaje, kuna siku 60 za likizo ya mwezi wa sita na kumi na mbili. jumamosi na jumapili kwa mwaka ni siku 106. kuna wiki moja ya pasaka na wiki moja ya mwezi wa 9 jumla siku kama 10 ukitoa jmosi na jpili. kuna sikukuuu tufanye siku 5 hivi. jumla ni siku 171. ukichukua siku 365-171 unapata siku 194 kwa mwaka. tofauti ya siku 49 na japan. Huu ni muda mwingi sana wa kujifunza.

Aliendelea kuandika kuwa huko bronx New York. Ni asilimia 16 tu ya wanafunzi wanaweza kufanya hesabu vizuri. Wakaanzisha shule za majaribio. Shule hizi huanza saa moja na nusu hadi saa kumi na moja jioni. Hapo unapewa na Homework za kutosha. Jumamosi darasa linaanza saa 3 asubuhi ha saa 7 mchana. Likizo ilipunguzwa kwa wiki tatu na siku za likizo darasa lilianza saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Matokea yalikuwa asilimia 84 ya wanafunzi waliweza kufanya hesabu vizuri na 80% walifanikiwa kufika chuo kikuu. Ila hili linahitaji kupata chakula shuleni.

Kwa hiyo niliona kwamba Tanzania watoto hawasomi vya kutosha. Kwanza kuna upungufu wa waalimu na muda mchache wa kusoma unaongezeka juu. Mwanafunzi anaanza saa mbili asubuhi mpaka nane mchana. Masaa sita tu ya kusoma.

Naonelea tuongeze muda wa kusoma labda toka moja na nusu hadi saa kumi jioni. masaa kama 8 na nusu. Tuongeze siku za kusoma walau zifike 230 kwa mwaka. Pia tujitahidi hata uji upatikane shuleni.

Malcom Lumumba , Rebeca 83 Nalendwa James Comey Wick mitale na midimu
Ni kitabu kizuri jamaa anatema cheche za ukweli...
 
Tatizo ni viongozi tulionao hawalitakii mema taifa letu
 
Back
Top Bottom