Kitabu cha Outliers na elimu yetu

Kitabu cha Outliers na elimu yetu

Watanzania hapo tuna mengi ya kufanya, dar es salaam nzima tuna maktaba ngapi ambazo watu wanaweza kwenda kujisomea baada ya masomo au siku za weekend?,,hiyo moja tu pale posta hata kujaa haijai.
Swala la muda wa masomo kuongezwa mashuleni si lazima ila ni jukumu la wazazi, walimu ,serikali, na jamii kwa ujumla kuwafanya watoto wapende hali ya kusoma ,,ebu angalia wilaya ya kinondoni nzima haina maktaba ya kujisomea na kuazima vitabu, ubungo ,temeke kote maktaba hadimu sijui kwa mikoani tutafika kwa mtindo huu?
 
Mkuu Red Giant mimi mpaka sasa nimeshajisemea moyoni kabisa sitahangaika na chochote cha Tanzania. Ukiiwaza sana Tanzania utaishia kuumia tu, na kupoteza muda.Haya mambo uliyoyasema ni kweli kabisa yana umuhimu mkubwa, kwa mustakabali wa taifa letu.

Lakini ukweli mchungu ni kwamba Tanzania haiji kubadilika hata siku moja na wala hakuna atayekusikiliza: Kama tungekuwa ni watu wa kubadilika basi tungeshabadilikaga muda mrefu sanaaaa na hata huku tusingekuwa tumefika.

Tunapenda sana siasa na uchawi kuliko maarifa na hekima. Laana aliyoiacha Nyerere kwenye hii nchi ni mbaya sana.
 
Hiki kitabu Outliers kimeandikwa na Malcom Gladwell. Kinaelezea kwanini watu hufanikiwa. Kuna sehemu kinazungumzia kuhusu mafanikio ya kielimu. Anasema Waasia wanaonekana wana akili sana sababu wana muda mwingi wa kusoma kuliko watu wengine.

Anasema kwa mwaka mwanafunzi wa Marekani anasoma siku 180. Mwanafunzi wa Korea kusini anasoma siku 220 kwa mwaka wakati mwanafunzi wa Japan anasoma siku 243 kwa mwaka.

sasa nikajiuliza mwanafunzi wa Tanzania anasomaje, kuna siku 60 za likizo ya mwezi wa sita na kumi na mbili. jumamosi na jumapili kwa mwaka ni siku 106. kuna wiki moja ya pasaka na wiki moja ya mwezi wa 9 jumla siku kama 10 ukitoa jmosi na jpili. kuna sikukuuu tufanye siku 5 hivi. jumla ni siku 171. ukichukua siku 365-171 unapata siku 194 kwa mwaka. tofauti ya siku 49 na japan. Huu ni muda mwingi sana wa kujifunza.

Aliendelea kuandika kuwa huko bronx New York. Ni asilimia 16 tu ya wanafunzi wanaweza kufanya hesabu vizuri. Wakaanzisha shule za majaribio. Shule hizi huanza saa moja na nusu hadi saa kumi na moja jioni. Hapo unapewa na Homework za kutosha. Jumamosi darasa linaanza saa 3 asubuhi ha saa 7 mchana. Likizo ilipunguzwa kwa wiki tatu na siku za likizo darasa lilianza saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Matokea yalikuwa asilimia 84 ya wanafunzi waliweza kufanya hesabu vizuri na 80% walifanikiwa kufika chuo kikuu. Ila hili linahitaji kupata chakula shuleni.

Kwa hiyo niliona kwamba Tanzania watoto hawasomi vya kutosha. Kwanza kuna upungufu wa waalimu na muda mchache wa kusoma unaongezeka juu. Mwanafunzi anaanza saa mbili asubuhi mpaka nane mchana. Masaa sita tu ya kusoma.

Naonelea tuongeze muda wa kusoma labda toka moja na nusu hadi saa kumi jioni. masaa kama 8 na nusu. Tuongeze siku za kusoma walau zifike 230 kwa mwaka. Pia tujitahidi hata uji upatikane shuleni.

Malcom Lumumba , Rebeca 83 Nalendwa James Comey Wick mitale na midimu
Walimu mshahara wao uongezwe kiduchu
 
Tatizo sio unatumia muda gani kusoma
Swali ni
Je unasoma nini?
Hata usome siku zote 365
Bado huwezi kuwazidi hao wajapan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bonge La Mada! Sema Hujanitagi Labda Kwa Sababu Ni Ingizo Jipya Jf , Hahaha, Kwanza Kabisa Muda Wa Kukaa Shuleni Hupangwa Kulingana Na Mtaala Wa Elimu, Kwamba Muda Gani Utatosha Kumaliza ,pia Mtaala Hupangwa Kutegemea Na Mahitaji Ya Jamii Husika ,ndio Maana Kuna Masomo Hufutwa Na Mengine Kuzaliwa, Nije Kwenye Mada Sasa, Kuongeza Muda Haiwezekani, Bali Ni Kufumua Mtaala Mzima Wa Elimu Ili Uweze Kukizi Mahitaji Ya Sasa Ambao Ni Kujitegemea Zaidi Na Si Kutegemea Ajira Tena,, Elimu Ya Kujitemea Haipo Tena ,kutokea Hapo Muda Nao Utabadirika, Ili Kukamilisha Mtaala, Mbona Zamani Ilikuwa Mpaka Sakumi Jioni, Na Ndio Elimu Ilikuwa Hot, Shida Ni Kwamba Hatujajua Shida Yetu Ni Nini Katika Elimu, Utakuta Wengine Wanakimbilia Kusema Lugha, ,
 
Na kiukweli hapa ndio wenzetu wanapotupiga gap. Ukikaa darasa moja mfano na wazungu, utagundua kua hawa jamaa sio kwamba wana akili sana la hasha! Ila wao ni perfectionists kwenye kila wanachokifanya kwa maana ya kwamba mtu anaanza ku specialize kwenye ka eneo kamoja tu tangu akiwa mdogo. Ndio maana unakuta kijana wa miaka 16 aliebobea kwenye computer huwezi kumlinganisha na PhD holder wa hapa Tz. Ila ukimuuliza mambo nje ya taaluma yake ni sifuri. Hapa kwetu unadonoa donoa kila kitu mwisho wa siku hakuna unachokijua.
Exactly kabisa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania hapo tuna mengi ya kufanya, dar es salaam nzima tuna maktaba ngapi ambazo watu wanaweza kwenda kujisomea baada ya masomo au siku za weekend?,,hiyo moja tu pale posta hata kujaa haijai.
Swala la muda wa masomo kuongezwa mashuleni si lazima ila ni jukumu la wazazi, walimu ,serikali, na jamii kwa ujumla kuwafanya watoto wapende hali ya kusoma ,,ebu angalia wilaya ya kinondoni nzima haina maktaba ya kujisomea na kuazima vitabu, ubungo ,temeke kote maktaba hadimu sijui kwa mikoani tutafika kwa mtindo huu?
Hii comment imejaa ukweli mtupu " kwa muktadha huu .. nakubaliana na wewe kwamba tuna jamii ya watu wasioipenda elimu ".... tunapaswa kufanya juhudi kubwa ili tuweze kuwafanya watoto wetu waipende elimu kama ambavyo wanavyopenda kucheza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Red Giant bora umeleta hiki kitabu humu.

Kwa kuongezea muda wa watoto kujifunza mashuleni, huwa wanajali sana muda waliojipangia kiasi kwamba wakipoteza masaa fulani,(bila kukusudia) huwa wanatafuta njia ya kuyarudisha hata kama ikabidi kupunguza likizo.
Ila kwetu ni ngumu, kama tuna walimu wachache tayari.

Kitu kingine nilijifunza from Asians, parents&kids na jinsi walivyo makini na elimu. Linapokuja suala la masomo, licha ya kutumia muda mwingi kujifunza, mtoto kupata A's na B's darasani is not an option.
That's the aim. Hakuna kuremba.
Wameifanya kama custom to the point watoto that's all they know, na kwa wazazi kuelekeza watoto wao to that direction is their first and foremost job. Sisemi wazazi wengine hawako hivyo, lakini hawa wenzetu go extra na kuleta faida kwa watoto with their Tiger Parenting.

Tiger parenting - Wikipedia

http://time.com
 
Mkuu Red Giant mimi mpaka sasa nimeshajisemea moyoni kabisa sitahangaika na chochote cha Tanzania. Ukiiwaza sana Tanzania utaishia kuumia tu, na kupoteza muda.Haya mambo uliyoyasema ni kweli kabisa yana umuhimu mkubwa, kwa mustakabali wa taifa letu.

Lakini ukweli mchungu ni kwamba Tanzania haiji kubadilika hata siku moja na wala hakuna atayekusikiliza: Kama tungekuwa ni watu wa kubadilika basi tungeshabadilikaga muda mrefu sanaaaa na hata huku tusingekuwa tumefika.

Tunapenda sana siasa na uchawi kuliko maarifa na hekima. Laana aliyoiacha Nyerere kwenye hii nchi ni mbaya sana.

Nimecheka kama mazuri kwa huu ukweli unao uma..
 
Hii comment imejaa ukweli mtupu " kwa muktadha huu .. nakubaliana na wewe kwamba tuna jamii ya watu wasioipenda elimu ".... tunapaswa kufanya juhudi kubwa ili tuweze kuwafanya watoto wetu waipende elimu kama ambavyo wanavyopenda kucheza..

...And this's the Key. Watoto.
Tunavyohangaika sasa na jamii ya watu wasiopenda elimu/vitabu, ni matokeo ya siku za nyuma. Hatukulelewa in that atmosphere ya kupenda vitabu na matokeo yake ndo haya.
Kwa watoto wa sasa ndio pa kuanzia, kubadilisha hali for the future.
...And that's the Key. Watoto.
 
Kusoma masaa mengi bado sio ishu. Vipi kuhusu maarifa yanayotolewa katika hayo masomo. Mfumo wetu unahitaji marekebisho makubwa tena makubwa sana.

Lakini ndio tunazidi kudidimia siku baada ya siku. Ni janga kuu la taarifa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante Mkuu -- maoni yako ni mbegu ya mafanikio katika elimu endapo yakitumika vyema

Back
Top Bottom