KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

KISWAHILI: Naomba maana ya maneno haya...

Huja acknowledge kuwa hata Kiswahili cha kuandika hatukijui.We are talking about a vast population of Swahili speakers.Au uta settle for that mish mash produced in the bible?

Nina acknowledge mkuu. Lakini mwanzo wa zeze ni lele au mpaka niseme mwanzo wa ngoma?! 🙂
 
Nina acknowledge mkuu. Lakini mwanzo wa zeze ni lele au mpaka niseme mwanzo wa ngoma?! 🙂

I admire your vision, it is visionaries like you who make important changes in this world.I on the other hand am more practical.

Let's send a man to the outer wanderers while we are at tit.
 
Mgekuwa mnachangia kwa kiswahili ingeleta maana zaidi.
 
Mi naomba kufahamishwa jambo moja, hivi inakuwaje watu wanaopiga kelele au kuongea kwa sauti kubwa yenye kukera, wakitakiwa kunyamazishwa utamsikia mtu anasema... mf: Jamani eeh! "Keleleni" au "kelelee"

Wakati mwingine utawasikia watu wanabishana na mmoja anamwambia mwenzie kwa sauti kubwa... "Kelelee...!"

Hii inamaanisha nini wakuu.

Naomba kuwakilisha...!
 
Wakati mwingine lugha haina mantiki ('logic'). Ni sauti za nasibu ambazo watu (jamii) 'inakubaliana' kutumia katika kuwasiliana. Maneno hayo pengine kimantiki hayakubaliki lakini jamii ya waswahili tumekubaliana kuyatumia kama yalivyo - na kwa kweli tunaelewana!. Mtu akikwambia kwa sauti 'kelelee'! unajua fika ana maana acha kelele. Ni kama vile neno 'acha' kwa makusudi linaachwa silent kwa sababu msemaji ana-assume msikilizaji (anaepiga kelele!)ataelewa.

Kiswahili kina maneno/misemo mingi tu ya jinsi hii. Kwa mfano mtu anaweza kusema:

- 'Mambo'? (akiwa na maana ya 'mambo vipi'?)
- 'Za saa hizi? (akiwa na maana ya 'habari za saa hizi'?)
- 'Za kwako?(akiwa na maana ya 'habari za (nyumbani) kwako'?)
- 'Nakuja!' - wakati in reality mtu anondoka' (akiwa na maana ya 'nitarudi punde' au 'nitakuja tena baada ya muda mfupi')
 
Hongera sana MAXENCE kwa kuuliza Maswali, na SHUKRANI SANA kwa Mzee M/Kijiji kwa majibu yake sahihi na yenye maelezo yanayojitosheleza. ama kweli JF ni Darasa la kutosha. Hebu tuendelee kujifunza na kuwa wazi kama kawaida badala ya Malumbano.
 
Heshima mbele wakuu..Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakiitwa 'Vihiyo' na pia baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikilitumia neno hili,,utakuta gazeti fulani limeandika(kwa mfano) "Kiongozi kihiyo aumbuka" ama utakuta mtu anasema "Balantanda ni kihiyo"...Hivi wakuu asili ya neno hili ni nini hasa??,,je,neno hili ni rasmi kwa sasa katika lugha yetu adhimu ya Kiswahili??,,na mwisho je,ni zipi sifa hasa za mtu kuitwa 'Kihiyo'...Naombeni msaada wakuu
 
Kihiyo alikuwa mbunge (Nadhani wa Temeke) alifoji vyeti kuwa alisoma Dar Technical college(siku hizi DIT).
Kihiyo huyo baada ya kuonekana kafoji vyeti akapigwa chini ubunge (Nadhani ndio kipindi Mrema akagombea na kuwa mbuge wa Temeke)
Kuanzia hapo watu waliokuwa wakionekana kama wamefoji vyeti au hawana utaalamu ktk field zao huitwa Kihiyo.Kwa viongozi utasikia viongozi Vihiyo.

Ni surname ya mtu hiyo ahaaaaaaaaaaaaaa,ila ndio imeingia katika kiswahili cha bongo ,ukizingatia kuwa moja ya sifa ya lugha ni kuwa lugha hukuwa na pia ni mpangilio wa sauti za nasibu zilizo kubalika na kutumika na jamii ya sehemu fulani.
 
Mkuu Mutu,,je neno hili kwa sasa ni rasmi ama bado ni la 'mtaani'???
 
Heshima mbele wakuu..Kwa muda mrefu nimekuwa nikisikia baadhi ya watu wakiitwa 'Vihiyo' na pia baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikilitumia neno hili,,utakuta gazeti fulani limeandika(kwa mfano) "Kiongozi kihiyo aumbuka" ama utakuta mtu anasema "Balantanda ni kihiyo"...Hivi wakuu asili ya neno hili ni nini hasa??,,je,neno hili ni rasmi kwa sasa katika lugha yetu adhimu ya Kiswahili??,,na mwisho je,ni zipi sifa hasa za mtu kuitwa 'Kihiyo'...Naombeni msaada wakuu

Kama alivyojibu Mtanguliza wangu, KIHIYO - Asili yake ni Jina la Mtu/Mbunge wa Zamani wa Temeke(sikumbuki majina yake ya mwanzo- ila Kihiyo ndilo jina maarufu japo kuna watu wengi nawafahamu wanatumia jina hilo, ni kama Jina Mrema, ukisema Mrema basi fikra ya Mwanzo utawaza Augustino Lyatonga japo ni jina la ukoo mkubwa tu).Mbunge Huyu katika Forms zake za ugombea alionesha kwamba ana FTC - Full Technician Certificate ya DIT(zamani Dar Tech) kumbe yote hiyo haikuwa kweli bali alighushi Cheti, walioshindwa katika uchaguzi ule walipinga matokeo na kesi iliposikilizwa ndipo mambo yote yakabainika pale aliposhindwa hata kumtaja aliyekuwa mkuu wake wa chuo wakati huo, hivyo matokea yalitenguliwa na jimbo likatangazwa nafasi wazi ya ubunge na uchaguzi mpya kuitishwa ambapo baadae alichaguliwa Mbunge mwingine(Lyatonga).
Sasa ikawa kila ambaye anaonekana kuto mudu nafasi yake ya kazi kitaalamu basi alihisiwa kwamba huenda mambo ni yale yale ya Kihiyo ndio mwanzo wa kuibuka neno kihiyo kwa asiye na elimu ya kutosha. nikama ambavyo imekuwa kawaida kwa watu kutumia maneno kutoka na matukio, mfano utasikia mtu akisema "we endelea tu kunichokoza... nitakuangushia KOSOVO, akimaanisha fujo/vurugu ama kipigo atakachokupa ni kama ilivyokuwa zile vita maarufu ya mapigano kule KOSOVO-URUSI.
 
Mkuu Mutu,,je neno hili kwa sasa ni rasmi ama bado ni la 'mtaani'???

Si kiswahili rasmi ni la mitaani,ila usilaumu kutumika na media maana tafsiri ya lugha ina uwanja mpana ya kuruhusu maneno hayo kutumika japo si rasmi.
 
Mkuu Mutu,,je neno hili kwa sasa ni rasmi ama bado ni la 'mtaani'???

Neno likijulikana na wengi, na jamii ikilikubali, huwa tayari ni neno rasmi. Tunaweza kusema, kwa mfano, ..... ni Mandela wa Tz, au .... ni Shakespeare/Shaaban Robert wa zama hizi.

Hivyo, tunaweza kusema pia: "Walimu vihiyo lazima ...."

Labda tuchukue mfano hai. Mabasi ya abiria ya jijini Dar, na sasa hadi ktk mikoa mingine ya Tz, yanaitwa daladala kutokana na historia ya neno hilo. Ktk miaka ya 70 mwishoni, watu binafsi walianza kujiingiza ktk biashara ya usafiri wa abiria baada ya shirika la umma la UDA, wkt huo, kuwa muekezaji pekee ktk biashara hiyo. Wkt huo nauli ilikuwa ni sh. 5, ambayo ilikuwa sawa na dola 1 ya kimarekani. K/hiyo, makonda walikuwa wakipiga debe: "Temeke-Posta! Temeke-
Posta! (kwa mfano), nauli dala!; dala dala! dala dala! Temeke-Posta!
". Neno hili (daladala) likaanza kuwa ni jina lililotumika kutofautisha mabasi ya UDA na yale ya binafsi. Jamii ikalikubali, na ndipo likawa neno rasmi.
 
Wakuu Lusajo na Mwanjelwa,kwa muda mrefu nimekuwa nikiambiwa kuwa mengi kati ya majina ya mwanzo(first names) ya ndugu zetu wanyakyusa hubeba maana fulani,naomba mnisaidie kunipatia maana ya majina haya:- Atuganile,,Atupele,,Atupokigwe,,Tupeligwe,,Atupakisye,,Ambisile,,Tuntufye,,Atufikwege,,Ambele,,Anganile,,Andendekisye,,Gwamaka,Ambonisye,Andombwisye...Kwa leo ni hayo wakuu ntajaribu kuyatafuta na mengine
 
mimi siyo mnyakyusa lakini najua maana ya baadhi wanyakyusa wanaweza nikosoa lakini maana haitakuwa mbali sana

Tuntufye- Tumsifu

Gwamaka-Mungu
 
Pia kuna majina kama Sekela,Tusajigwe,Tusekeleni,Tutindaga na Nsajigwa
 
Most of those names have their root in praising the lord, although the name of the lord is not explicitly mentioned, you are supposed to know that he is the subject. For example Atupele literally means he has given us. implicit to that is that the God lord has given us ( I tend to think he has given us his son) Gwamaka literrally means the one who has the power, implicitily it means the lord who has the power. Atuganile means he loves us , Sekela (Furahia).

There is no Atufikwege, perhaps you meant Atufigwege (kutufya means kusifu ) so Atufigwege means asifiwe atufigwege means asifiwe daima, Tuntufye means tumsifu. To the best of my knowledge there is no Ambisile I can not help you there, nyakyusa is my tenth langauge that I rarely use I learned it while a student at TKY.
Ndigwako -I am yours, again do not get excited it just means oh lord I am yours. Tutindaga = lets give thanks or lets be thankful

Ndaga means thanks, Ambele =He has given me,

Tupokigwe =Tumeokolewa,
Tusajigwe means tumebarikiwa.
Lusajo Means Baraka
 
Back
Top Bottom