Kiswahili kimeua lugha za asili za Watanzania kimya kimya

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
21,065
2,000
1-300x250.jpg

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe

Benjamin Sawe, Dar es Salaam

LICHA ya Tanzania kuwa na utajiri wa makabila zaidi ya 120, lakini watu wake wapo katika hatari ya kuzika lugha zao za asili kwa kuwa idadi kubwa ya wazazi wanazipuuza na hivyo kuwafundisha watoto lugha ya Kiswahili pekee.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), lugha za asili ni utambulisho wa makabila mbalimbali duniani na zina umuhimu mkubwa katika jamii.

Hivyo, Watanzania wanapaswa kuweka mikakati ya kuwarithisha watoto wao lugha na tamaduni zao kwa kuwa ipo tofauti kubwa kati ya ukabila na makabila. Lugha na utamaduni wa asili ni urithi usioshikika na una thamani kubwa kwa Taifa hivyo wazazi wasizipuuze kwa kisingizio cha kuepuka ukabila.

Wakati wa kupigania Uhuru wa Tanganyika, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere alihimiza matumizi ya Kiswahili ili kuimarisha mfumo wa mawasiliano na kujenga Taifa lenye nguvu.

Hata hivyo alisema jambo hilo haliwazuii Watanzania kuendeleza makabila yao.

Baba wa Taifa alikuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya ukabila ili kudumisha amani, upendo na mshikamano miongoni mwa Watanzania, jambo lililochangia kuishi kama ndugu bila kujali tofauti za rangi, kabila wala itikadi za kidini.

Hata hivyo, Kiswahili hakipaswi kuchukuliwa kama tishio kwa lugha za asili kutokana na ukweli kwamba binadamu ana uwezo wa kujifunza na kuzungumza lugha zaidi ya tatu.

Taarifa za tafiti zinazofanywa na wataalamu mbalimbali wa masuala ya lugha na utamaduni, zinabainisha sababu zinazowafanya wazazi kutowafundisha watoto lugha za asili.

Sababu ya kwanza ni dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii kuwa lugha za asili zinajenga ukabila. Sababu ya pili ni elimu na mwingiliano wa watu katika makabila ambapo hata watoto wanaozaliwa vijijini wanalazimika kuzungumza Kiswahili wakati wote kama lugha ya mawasiliano shuleni na wanapokuwa nyumbani.

Mfumo wa maisha ya kisasa unaleta changamoto kubwa katika jitihada za kukuza lugha za asili pamoja na kudumisha mila na desturi za makabila mbalimbali nchini Tanzania. Pia mwingiliano wa makabila katika ndoa, kukua kwa miji, maisha ya kuhamahama na kukua kwa mfumo wa elimu ni miongoni mwa sababu kubwa zinazodidimiza maendeleo ya lugha za asili, mila na desturi za makabila mbalimbali.

Tofauti na miaka ya nyuma ambapo ilikuwa ni nadra kuona watu wa makabila tofauti wakioana, hivi sasa asilimia kubwa ya wanandoa ni watu wa makabila tofauti jambo linalosababisha watoto kuzungumza lugha ya Kiswahili kama lugha ya asili.

Maisha ya kuhamahama yanasababisha watoto kutojifunza lugha ya asili hata kama wazazi wao wametoka kabila moja. Pia gharama za usafiri zinakwamisha maendeleo ya lugha ya asili kwa kuwa wazazi waliokuwa na desturi za kuwapeleka watoto wao vijijini wakati wa likizo hivi sasa wameacha kufanya hivyo kitendo kinachowanyima watoto fursa ya kujifunza mambo ya asili.

Kukua kwa miji na mabadiliko ya mfumo wa kiuchumi kunasababishwa na watu wa makabila tofauti kuacha kutumia lugha zao za asili na kuzungumza lugha inayoeleweka na watu wote. Pia wanapohamia eneo fulani wanaacha mila na desturi za makabila yao na kufuata mfumo mpya wa maisha kulingana na eneo walilohamia.

Watanzania wanapaswa kuweka mikakati ya kufungua benki za kuhifadhi taarifa mbalimbali kuhusu mila na desturi za kila kabila nchini, ikiwa ni pamoja na kuwafundisha watoto lugha za asili na kuwasimulia hadithi mbalimbali juu ya mambo ya kale hususani juu ya mila na desturi ambazo hazina madhara kwa jamii.

Kwa kuwa maendeleo ya sayansi na teknolojia yanaathiri tamaduni, mila na desturi za makabila mbalimbali, wazee wanapaswa kutumiwa kikamilifu ili kukusanya taarifa muhimu na kuziweka katika maandishi.

Watu na viongozi wa makabila hayo wanapaswa kuweka mikakati ya kutangaza mila na desturi zao ili Watanzania kudumisha utajiri wa mila na desturi za makabila ya Tanzania.

Lugha za asili zimebeba maarifa mengi yaliyolimbikizwa na jamii ambapo kama jitihada za makusudi hazitachukuliwa sasa kuzidumisha,kuzififisha na kuzibeza zitakufa taratibu katika kipindi cha miaka 20 ijayo.

Ni wazi kwamba lugha zetu za asili zimeanza kukosa mvuto mbele ya kizazi hiki kipya ambacho sehemu kubwa ya maisha yao toka kuzaliwa na kukulia kwenye mazingira yanayotumia lugha za mataifa ya Magharibi.

Lugha hizi, lazima zifunguliwe milango katika sekta ya habari na mawasiliano, katika elimu na katika siasa. Kuthamini lugha zetu kutatupa msukumo mkubwa katika kujiletea maendeleo, kujenga demokrasia na kuhifadhi utamaduni wetu.
KISWAHILI KIMEUA LUGHA ZA ASILI KIMYA KIMYA
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,024
2,000
Katika vitu vichache nilivyompinga Mwalimu Kambarage ni mpango wake wa kuua makabila Tanzania. Makabila yetu ndio utambulisho wetu halisi, tukumbuke kuwa hizi nchi sijui Tanzania, Kenya n.k ni mzungu ndiye aliyezitengeneza.

Kukubali kuua kabila lako na lugha yako ya asili ni upunguani wa hali ya juu.
 
Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,154

Kila taifa lingekuwa na mtazamo kama wako unafikiri hali ingekuaje?
 
kashinje juma

JF-Expert Member
Apr 20, 2017
707
1,000

Na kabila lingine linaloua makabila madogo madogo ni WASUKUMA. Huku kanda ya ziwa makabila mdogo madogo yanaolewa na kubadilishwa kila kitu.
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,024
2,000
Kila taifa lingekuwa na mtazamo kama wako unafikiri hali ingekuaje?

Haina shida yoyote, ni upuuzi kulazimisha watu wapoteze asili yao kisa utambulisho ulioletwa na mzungu. Mtu akiwa mzalendo kwa kabila lake shida ipo wapi?

Upuuzi wa Tanzania hata redio za makabila haziruhusiwi wakati redio za dini za kigeni zinaruhusiwa.
 
kilam

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
2,024
2,000
Na kabila lingine linaloua makabila madogo madogo ni WASUKUMA. Huku kanda ya ziwa makabila mdogo madogo yanaolewa na kubadilishwa kila kitu.

Tatizo hilo tena kubwa, vijana wa siku hizi kupotezea makabila yao ndio wanaona ujanja kumbe ujuha.
 
Hoshea

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
4,988
2,000
[quote uid=142457 name="MK254" post=21727271]Nimesema Watanzania waliopakana na mataifa majirani bado hawajawa watumwa, wamefaulu kudumisha asili zao, Wahaya, Wanyakyusa, Wasukuma, Wamaasai n.k. Lakini wengine wote walishamezwa, wengi hata hawajui salamu kwa lugha zao.[/QUOTE]<br />Kwa hiyo kujua kiswahili kuliko kikabila tumekuwa watumwa, ha haa, Jamaa baada ya kukubaliana na utumwa wenu mmetafuta pa kutuita watumwa ili mfanane, ukaona uje na kiswahili, mkuu unapaswa ujue kiswahili kina asilimia kubwa ya misamiati ya lugha za kikabila za hili eneo la Tanganyika na Zanzibar. Kiarabu kireno na kiingereza vina mchango sumni sana. Najua umeshangaa neno sumni, sumni na kidogo vyote vina maana moja tu, kuna ya kibantu na arabu hapo. So it was agreed that all these tribes in order to unite, tuunge nguvu kwenye kiswahili ambacho kilikuwa kimesambaa zaidi. Hakuna utumwa hapo mkuu, sababu hata kikikuyu kina lugha ambazo zilikuwepo kabla ya current Kikuyu language, likewise kuna ancient Chinese and current one. So muingiliano wa watu huwezi kuucontrol buda, na muingiliano wa watu hukuza na kudiversify lugha, hence lugha hazitabaki the same, ww mwenyewe umejifunza zaidi kiswahili humu jamvini, na sasa unabonga zaidi na wanao kiswahili, na wanao wanajikuta wana baba mzungumzaji mzuri wa Swahili na wao wamezungukwa na jamii inabonga Swahili muda mwingi wakiwa home, skuli ndio kiingereza kwa sana, likizo kwa bibi na babu Kikuyu, ww kwa akili yako mwanao atakuwa bora kwenye lugha gani? Muda mwingi atatumia wapi na akiwa na watu wanasema lugha gani. Let's be analytical and burry this topic for good.<br /><br />Sasa hapo kama una akili sawasawa utaona muda mwingi atakuwa around Swahili language, hence Swahili growth ma niga, ww unadhani ni kwann Swahili ni second most spoken language in Africa, ni tokana na social political factors which you as an individual ma Frnd can't stop it. Ndio maana unaona serikali ya Tz inataka kuiweka kwenye mtaala wa elimu, sababu no way out English speakers will surpass Swahili ones. <br />Kwa iyo hata Swahili kuingizwa kwenye mtaala wenyu wa elimu, hauepukiki, eti mnajaribu kupunguza kuenea kwa kuleta sheng, itabaki kuwa kama lugha ya kikabila cha watu wa Nairobee ambacho kitamezwa na Swahili. <br />Sababu inaongelewa Congo mshariki, Burundi, Rwanda, Ug, SA wameomba walimu, Zambia kaskazini, Msumbiji kaskazini, visiwa vyote bahari ya Hindi, Bongo enyewe kubwa kushinda Naija, imagine tukija kuwa MTU nyomi kama Naija, wote waswahili. <br /><br />Swahili will become the first most spoken language, nations are making decisions, Zimbabwe, Ethiopia etc are cracking their minds on how to teach their people Swahili so that they are not left behind in the near future. Wewe baki hapo na utumwa wakati mtumwa anakuja kuwa mfalme like Joseph.
 
CAMARADERIE

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
4,428
2,000
Katika vitu vichache nilivyompinga Mwalimu Kambarage ni mpango wake wa kuua makabila Tanzania. Makabila yetu ndio utambulisho wetu halisi, tukumbuke kuwa hizi nchi sijui Tanzania, Kenya n.k ni mzungu ndiye aliyezitengeneza.

Kukubali kuua kabila lako na lugha yako ya asili ni upunguani wa hali ya juu.Kabila hutokana na mazingira pia. Muhaya yuko jinsi alivyo kwa kuwa mazingira ya Bukoba yalimfanya awe hivyo. Sasa kahamia Darisalama na amezaa watoto unadhani watoto wale watakuwa watu wazima wa Kihaya kamilifu? Hata ulaya walikuwa na makabila kama sisi lakini nyakati haziko tena kama zama hizo walipokuwa na makabila.
 
Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
8,154
2,000
Haina shida yoyote, ni upuuzi kulazimisha watu wapoteze asili yao kisa utambulisho ulioletwa na mzungu. Mtu akiwa mzalendo kwa kabila lake shida ipo wapi?

Upuuzi wa Tanzania hata redio za makabila haziruhusiwi wakati redio za dini za kigeni zinaruhusiwa.
Kwani hicho unachokitaka wewe faida zake ni zipi?
 
Mdumange

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
714
1,000
Katika vitu vichache nilivyompinga Mwalimu Kambarage ni mpango wake wa kuua makabila Tanzania. Makabila yetu ndio utambulisho wetu halisi, tukumbuke kuwa hizi nchi sijui Tanzania, Kenya n.k ni mzungu ndiye aliyezitengeneza.

Kukubali kuua kabila lako na lugha yako ya asili ni upunguani wa hali ya juu.
Nyerere alifanya vizuri sana nchi inahitaji lugha moja tu...ukitaka lugha ya kwenu rudi ukaishi kijijini..mjini ni kiswahili tu.nchi zote zilizoendelea wana lugha moja tu.
 
Victor wa happy

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
11,675
2,000
Duuuu sidhani hata km unaelewa

Nyerere aliua makabila?

Unatia aibu we huoni Kenya wanavyouana kwa ukabila baada ya kukosa lugha moja iliyowaunganisha toka uhuru?

Katika vitu vichache nilivyompinga Mwalimu Kambarage ni mpango wake wa kuua makabila Tanzania. Makabila yetu ndio utambulisho wetu halisi, tukumbuke kuwa hizi nchi sijui Tanzania, Kenya n.k ni mzungu ndiye aliyezitengeneza.

Kukubali kuua kabila lako na lugha yako ya asili ni upunguani wa hali ya juu.
 
Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,681
2,000
Ndio safi, ukabila unakufa kimya kimya! Hata Kenya Kiswahili kimewasaidia kupunguza ukabila kwa kiwango kikubwa... Ukimsikia Kenyata akiongea, basi ni Kiswahili ama Kizungu... Kikikuyu kapuni!
 
game over

JF-Expert Member
Jan 1, 2016
7,441
2,000
Katika vitu vichache nilivyompinga Mwalimu Kambarage ni mpango wake wa kuua makabila Tanzania. Makabila yetu ndio utambulisho wetu halisi, tukumbuke kuwa hizi nchi sijui Tanzania, Kenya n.k ni mzungu ndiye aliyezitengeneza.

Kukubali kuua kabila lako na lugha yako ya asili ni upunguani wa hali ya juu.
Kaka sidhani kama upo sawa, naona kama unataka kuturudisha nyuma.
Dunia na inakati zinabadilika.
We call it Evolution, ambapo mazingira kiumbe anakuwa exposed ndio huamua kiumbe aweje,
Kama ukitaka hiyo dhana yako iwe practical ni pale maybe tuamue kila mtu arudi akaishi katika ardhi ya Kabila lake which is too awkward,
Mimi nawezasema haya mambo hutokea automatic kadiri nyakati zinavyoenda,

Familia huungana na kuwa ukoo- Kabila- Jamii -Taifa. Utaifa ni Mafanikio makubwa zaidi..

Kumbuka kuwa hakuna Mafanikio Makubwa zaidi katika Jamii zaidi ya Muungano,
Refer USA, RUSIA, UK, CHINA, INDIA,
Sasa kama Mungu alitujalia kiongozi wa kutuunganisha tena Kwa lugha Moja BOLD (Kiswahili) ambayo kwa sehemu kubwa ni Kibantu why not be proud of it?.

Hebu fikiria siku Moja Africa nzima iwe nchi moja inayozungumza Lugha Moja na Rais Mmoja na tuwe na Population Nusu ya Dunia,
Hatuwezi kuwa threat kwa Wazungu?
Narudia, we need to Unite, Unite and Unite to be powerful, Natumaini Kiswahili ndio Lugha pekee itakayoiungansha Africa hata kwa Miaka 100 ijayo.
 
ECONOMY

JF-Expert Member
Apr 10, 2017
509
500
Katika vitu vichache nilivyompinga Mwalimu Kambarage ni mpango wake wa kuua makabila Tanzania. Makabila yetu ndio utambulisho wetu halisi, tukumbuke kuwa hizi nchi sijui Tanzania, Kenya n.k ni mzungu ndiye aliyezitengeneza.

Kukubali kuua kabila lako na lugha yako ya asili ni upunguani wa hali ya juu.
Makabila yatakusaidia nini wewe?
 
ECONOMY

JF-Expert Member
Apr 10, 2017
509
500
Safi sana vijulugha vyenu huko huko vijijini kwenu .mkija town ongeeni kiswahili la sivyo tutawarudisha kwenu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom