Kiswahili kimeua lugha za asili za Watanzania kimya kimya

dah! huwa nakupaga tano mara zote lakini kwa hili NO!

hatuitaji makabila ya aina yoyote na bora yafe tu. kinachoitajika ni Utanzania

Wewe ndio huhitaji, mimi kabila langu ndio utambulisho wangu wa kwanza. Naweza kubadili uraia lakini sio kabila.
 
lukindo

Utakuwa umechanganya kati ya kabila na ukabila! Hivi ni vitu viwili tofauti! Kuongea lugha ya kabila lako hadharani sio ukabila, ila kumbagua mtu kwa sababu ya kabila lake huo ndo ukabila!

Tukiwaambia wakenya kuhusu ukabila hatumaanishi kuwa wanaongea vilugha hadharani, La hasha!

Labda hauna exposure na ukabila wa Kenya! Kwa mfano, sio rshisi kwa mkikuyu kenya kuoa/kuolewa na mjaluo! Huu ndio unaguzi,

Pia wakikuyu wengi hawapendi samaki na ukiuliza sababu eti samaki wanaliwa na wajaluo

Ubaguzi wa hawa watu ni mkubwa kweli kweli na ndo unawaathiri hadi kwenye uchaguzi, hawataki kabila jingine litawale

Hata mtu kutotaka kuoa mtu wa kabila tofauti na lake sio ubaguzi pia, kuna watu wanataka kutunza utambulisho wao na sio dhambi hii. Sio Waafrika wote wanajichukia kama nyie.

Mbona hapa Tanzania Muislamu anaoa Muislamu mwenzake na Mkristo anaoa Mkristo mwenzake hamuiti ubaguzi? Au ubaguzi wa kidini unaruhusiwa?
 
Eti vilugha?Watz mnatisha.Mnadharau asili zenu,sijui mnajidai waarabu?Lugha ya MAMA mnaita vilugha?Nakienzi kiswahili lakini ikiekwa kwenye ratili na lugha nilofunzwa na mama,haitoshi mboga bana.Kwanza ni lugha ya mama Kikuyu afu kimaasai kiswahili,kiingereza na kimeru zinavuta mkia kwa pamoja.
 
Kwa mtu ambaye kiswahili ni lugha yake ya kwanza kuna haja gani ya kuitukuza lugha jamii yake asiyoijua.

Na unakuta huyo mtu anaishi sehemu isiyozungumzwa hiyo lugha na haitumii katika shughuli yeyote.
 
Tayari mnavuna mlichopanda aisee najaribu kufikiria ni sehemu gani ya Kenya ambapo Kikuyu hakitumiki sipati.Hehe.Utajivuniaje kuwa mwafrika wa kweli wakati hufahamu hata walivoamkuana babu zako?
 
Wewe ndio huhitaji, mimi kabila langu ndio utambulisho wangu wa kwanza. Naweza kubadili uraia lakini sio kabila.

Wengi tulikuwa na makini kama hiyo. Lakini sasa utakuta ukiwa town baada ya kumaliza shule au ukiwa katika mishe za mjini unakutana na binti wa kirangi au kinyaturu au kinyamwezi au kisukuma au kihehe au kisambaa nk. Bila ya kufanya hiyana unajitwalia binti na kuanza kupata watoto. Kuanzia hapo ukabila wetu unaanza kuyeyuka hatua kwa hatua hatimae utaisha.
 
Tayari mnavuna mlichopanda aisee najaribu kufikiria ni sehemu gani ya Kenya ambapo Kikuyu hakitumiki sipati.Hehe.Utajivuniaje kuwa mwafrika wa kweli wakati hufahamu hata walivoamkuana babu zako?
Sio kuvuna lugha lengo lake kuu ni mawasiliano na kama yanaenda sioni tatizo.

Kuna lugha nyingi saana duniani zimekufa.
 
Wewe utajihisi sawa ukiambia watu lugha yako ya asili imekufa,na bado wewe mwenyewe uko hai eti!Acha mzaha wewe!
 
Wewe ndio huhitaji, mimi kabila langu ndio utambulisho wangu wa kwanza. Naweza kubadili uraia lakini sio kabila.
maskini kilam watanzania wenzako watakuponda wakumalize. Wao wanafuata mkondo uliowekwa kitambo ambapo asili yenu ni kitu cha kuchekwa na kudharauliwa. Umenikumbusha jinsi watu wa msumbiji pia wana hilo kasumba ya kuua na kucheka asili yao hasa ukipatikana ukiongea hizo "vijilugha". Hivi unadhani ni vyema kuyaangamiza historia/tamaduni/lugha za mababu zetu kisa mipaka ya wakoloni?
 
Hapa unapinga mipaka eti ni ya wakoloni, wakati likija suala la kiingereza, unajivunia lugha ya hao wakoloni!
 
Back
Top Bottom