Kiswahili kimeua lugha za asili za Watanzania kimya kimya

Na kwa kukumbushana tu ni kuwa
Lugha ni Nyenzo muhimu katika kuwaunganisha watu,
Biblia yangu hunikumbusha Failure ya Ujenzi wa Mnara wa Babeli ilikuja baada ya Mungu kuwapandikizia Lugha tofauti hatimaye disunity.
tunatakiwa kuongeza juhudi Kuhakikisha kiswahili kinasambaa ulimwengu mzima,
Hadi sasa Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo zote mbili, Zambia, Mozambique na Malawi lugha hii inasambaa kama UKIMWI,
Ni vizuri wana Africa mashariki kukomaa na kuhakikisha tunapenyeza Kiswahili Duniani kwa Nguvu zote,

Tunashukuru wasanii Kama diamond platinums na wasafi band yote kwa kutangaza kiswahili kupitia nyimbo zenu.
Juhudi zaidi zifanyike!!
 
Kaka sidhani kama upo sawa, naona kama unataka kuturudisha nyuma.
Dunia na inakati zinabadilika.
We call it Evolution, ambapo mazingira kiumbe anakuwa exposed ndio huamua kiumbe aweje,
Kama ukitaka hiyo dhana yako iwe practical ni pale maybe tuamue kila mtu arudi akaishi katika ardhi ya Kabila lake which is too awkward,
Mimi nawezasema haya mambo hutokea automatic kadiri nyakati zinavyoenda,

Familia huungana na kuwa ukoo- Kabila- Jamii -Taifa. Utaifa ni Mafanikio makubwa zaidi..

Kumbuka kuwa hakuna Mafanikio Makubwa zaidi katika Jamii zaidi ya Muungano,
Refer USA, RUSIA, UK, CHINA, INDIA,
Sasa kama Mungu alitujalia kiongozi wa kutuunganisha tena Kwa lugha Moja BOLD (Kiswahili) ambayo kwa sehemu kubwa ni Kibantu why not be proud of it?.

Hebu fikiria siku Moja Africa nzima iwe nchi moja inayozungumza Lugha Moja na Rais Mmoja na tuwe na Population Nusu ya Dunia,
Hatuwezi kuwa threat kwa Wazungu?
Narudia, we need to Unite, Unite and Unite to be powerful, Natumaini Kiswahili ndio Lugha pekee itakayoiungansha Africa hata kwa Miaka 100 ijayo.
Naunga mkono hoja, kama ulivyo sema, kila kitu kina kwenda na muda.... Hakuna mtu atazuwia mabadiliko ya jamii kwa njia yoyote ile. Sisi tupo hapa hivi sasa, hatujuwi miaka mia moja au mia mbili ijayo jamii ya wakati huo wata taka kutumia lugha gani au njia gani ya mawasiliano. Hata tusiende mbali, kiswahili tunacho kitumia hivi sasa kwa namna fulani kina tofauti na kiswahili cha miaka ya 1940-50.

Ukiwa na makabila mengi, na yote yana lugha zao binafsi, inakuwa chamgamoto kwa serikali kutowa huduma. Fikiria ofisi za wakuu wa wilaya inabidi wachapishe maelekezo kwa lugha 120 kukidhi haja ya kila kabila. Kampuni za dawa, inabidi wachapishe maelekezo ya hizo dawa kwa lugha 120. Watu hawajakatazwa kuongea lugha wanazo zipenda, lakini muda unawafanya watu wachaguwe lugha moja ndio waweze kuwa na wigo mpana wa mawasiliano hasa hasa kwa watu walio mbali na maeneo yao au utamaduni wao.
 
Kwanini unaweka UNESCO kama reference?
Who are they to you?
Wasingekuwa UNESCO mji mkongwe ungelikuwa umeshageuzwa 'mji mpya', au kaulize waliobomoa jengo la 'Salamander' ambalo lilikuwa limewekwa kwenye majengo yanayotakiwa kusalia kama yalivyo!
Wazungu sometime hatuwapendi lakini ndio wametengeneza hata hii mitandao tunakokutana na kubishana kwa lugha zetu, wangelikuwa na akili fupi wangesema tutumie Kiinglishi pekee kwenye mitandao.
 
A common language is an integrating force in social cohesion. Ubaguzi like i-dont-want-these-four-rats-in-uasin Gishu is unheard of Tanzania.
 
Kiswahili stressed as PM launches new dictionary
MASATO MASATO in Dodoma
20 June 2017


PRIME Minister Kassim Majaliwa yesterday challenged Kiswahili students to embrace the language as a money minting opportunity, saying the government is committed to promote it as a major medium of communication in its national and international activities.

0 Comments
“We have resolved to have firm infrastructure to support availability of Kiswahili interpreters and teachers for increasing demand, as we have recently experienced emerging demand of Kiswahili teachers from the neighbouring countries,” Mr Majaliwa stated during the launch of the General Kiswahili Dictionary here.

He stated further that the government appreciated the role of Kiswahili in the promotion and protection of national unity, stressing: “It is Kiswahili that makes us Tanzanians”.

The premier specifically commended President John Magufuli for his dedicated efforts to use the national language in all national events like conferences, debates, seminars and teaching in schools.

“President Magufuli has spearheaded the use of Kiswahili in meetings and other important events he hosts for visitors from outside the country,” said Mr Majaliwa, imploring all Tanzanians—parents, parliamentarians, journalists, interpreters, translators, authors and communicators—to get and use the dictionary.

Speaking at the launch, the Tanzania Kiswahili Council (BAKITA) Executive Secretary, Dr Seleman Sewangi, said the Kiswahili word list was prepared to address the shortage of vocabulary in the language, hinting that 100m/- was spent on the project.

He said the council executed the project in partnership with Longhorn Publishers Limited of Kenya. The dictionary has 45,500 root words, special cultural labels, illustrative sentences and many new words, said the council chief, describing the glossary as unique and the first of its kind to have been published in the world.

Information, Culture, Arts and Sports Minister Dr Harrison Mwakyembe said the dictionary had come at an opportune time when Kiswahili language was gaining prominence in the world.

He said currently Kiswahili is the tenth widely spoken language globally and second In Africa. “… and soon Kiswahili will be the most spoken language in Africa. As Tanzanians we have to be proud of our language,” Dr Mwakyembe emphasized.

Chairman of Longhorn Publishers in Tanzania Khatibu Senkoro said Kiswahili was a tradable product, saying Tanzania should come up with articulate strategies to reap maximum benefits.

Kiswahili stressed as PM launches new dictionary
 
Katika mipango ya UNESCO nasikia hata engendered languages and cultures vinapewa kipaumbele. Hapa Tz tunawacheka wenzetu eti wana ukabila kwa kutumia kigezo cha kuongea vernaculars zao hadharani tena kwa kuzipenda wakati sisi tukiamini kuwa ni wamoja sababu sote tunaongea Kiswahili. Tulichosahau ni kwamba Mungu muumba nchi na mbingu ni mwenye mapenzi na anapenda viumbe vyote alivyoviumba ikiwa ni pamoja na lugha zao, right kama Mungu angelijua lugha ni mbaya basi asingeziumba! Patamu hapo.

lukindo

Utakuwa umechanganya kati ya kabila na ukabila! Hivi ni vitu viwili tofauti! Kuongea lugha ya kabila lako hadharani sio ukabila, ila kumbagua mtu kwa sababu ya kabila lake huo ndo ukabila!

Tukiwaambia wakenya kuhusu ukabila hatumaanishi kuwa wanaongea vilugha hadharani, La hasha!

Labda hauna exposure na ukabila wa Kenya! Kwa mfano, sio rshisi kwa mkikuyu kenya kuoa/kuolewa na mjaluo! Huu ndio unaguzi,

Pia wakikuyu wengi hawapendi samaki na ukiuliza sababu eti samaki wanaliwa na wajaluo


Ubaguzi wa hawa watu ni mkubwa kweli kweli na ndo unawaathiri hadi kwenye uchaguzi, hawataki kabila jingine litawale
 
Katika vitu vichache nilivyompinga Mwalimu Kambarage ni mpango wake wa kuua makabila Tanzania. Makabila yetu ndio utambulisho wetu halisi, tukumbuke kuwa hizi nchi sijui Tanzania, Kenya n.k ni mzungu ndiye aliyezitengeneza.

Kukubali kuua kabila lako na lugha yako ya asili ni upunguani wa hali ya juu.

dah! huwa nakupaga tano mara zote lakini kwa hili NO!

hatuitaji makabila ya aina yoyote na bora yafe tu. kinachoitajika ni Utanzania
 
lukindo
Utakuwa umechanganya kati ya kabila na ukabila! Hivi ni vitu viwili tofauti! Kuongea lugha ya kabila lako hadharani sio ukabila, ila kumbagua mtu kwa sababu ya kabila lake huo ndo ukabila!
Tukiwaambia wakenya kuhusu ukabila hatumaanishi kuwa wanaongea vilugha hadharani, La hasha!
Labda hauna exposure na ukabila wa Kenya! Kwa mfano, sio rshisi kwa mkikuyu kenya kuoa/kuolewa na mjaluo! Huu ndio unaguzi,
Pia wakikuyu wengi hawapendi samaki na ukiuliza sababu eti samaki wanaliwa na wajaluo
Ubaguzi wa hawa watu ni mkubwa kweli kweli na ndo unawaathiri hadi kwenye uchaguzi, hawataki kabila jingine litawale
Hapa ni kuimpose hoja mkuu Toyota escudo, mfano ni kusema wamasai hawapendi samaki kama wamanda! Pia kuoleana hata hapa Tanzania tunaoana lakini kuna pia watu ambao wanakuwa reluctant kuwaoa wengine. Mfano wa karibuni hauusiani hata na makabila bali utasikia mtu anasema ukioa aliyesoma umekwisha ...huu sio ubaguzi!?
Alafu ubaguzi mwingine unategemea aina ya siasa na kwa sasa unaona hata Tanzania mfano Wachaga, wanyakyusa au Wahaya wao kwa wao wanaweza kubaguana sababu ya vyama wanavyotokea ..refer mikutano ya siasa watu wanapigwa hadi mabomu wakati lengo lao ni moja na wote ni masikini. Nakuhakikishia hata jamii moja mnaweza kubaguana sababu ya koo zenu.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba 'disagreement' ni kitu kilichomo kwenye aslili ya uumbaji na hakiwezi kuisha mpaka labda binadamu atakapoacha kuishi duniani. Kwa hiyo suluhisho sio elimination (kuua lugha asili) ya kimojawapo bali to face the challenges of living together then mnagundua ule ukweli kwamba kila mmoja anamtegemea mwingine.
 
Umewahi kujiuliza maneno mapya ya Kiswahili yanatoka wapi ...si ni kwenye hivi vilugha!?
Je, unajua kuwa kamusi mpya ya Longman (sijui Oxford?) imetambua neno 'bodaboda' kama jipya kwenye English!?
Vilugha vyenu hukooooo mkija town lugha moja tu
 
Ni ukweli ulio wazi na usioonekana sasa miaka mingi ijayo makabila yetu yatakuwa duni sana, maana sasa hata ukienda Vijijini uwezi kuona tena ngoma zetu za asili, uwezi pata watu waliobobea katika kuelezea historia ya makabila au kabila husika na kama wapo ndio wanaishiria, ukiuliza baada ya wewe nani meingine ana hazina ya kabila hili jibu ni hakuna.

Makabila yetu ni fahari yetu, inapendeza unapoongea lugha ya asili, leo tuna vijana wengi tumesoma, tunasali, tunaishi nao ulimuuliza kabila atakwambia,mie mluo,mie mchaga, mie mnyakyusa,mie mmakuwa au mgogo au muha nk nk lkn ukitaka kuongea atakwambia sijui? Aliejitahdi sana atakwambia najua salam tu, nenda mbali umuulize kwenu ni mkoa flan sehemu gani asiposema sipajui atakwambia tunaendaga tu December sijui.

Hii ni mbaya sana kwa historia yetu. Na Msatakabali wa taifa letu, hatuwezi kuishia kujiita waswahili basi, inapendeza tunapoonesha na asili yetu.

Ndio maana kuna TOFAUTI kati ya mzanzibari na mjita, hawa wote wanaongea kiswahili lakini mmoja anaongea na lugha asili, tukikutana kwenye maharusi, radha inakuja unapoona watu wanacheza nyimbo za kwao. Wanakumbuka Nyumbani.

Tukipoteza kabisa makabila ya asili, tutapoteza mila zetu, tamaduni, miiko na desturi,maana hakuna mila za mswahili, wala miiko aghalabu mambo ya wazalamo ndio uhitwa ya kiswahili, sasa Je wote tunataka kubaki na mila na tamaduni za watu wa pwani? Ambazo ndio sana zinatambulisha uswahili.

Hoja hii ni muhimu, tuwekeze tena katika mila na lugha za asili, wala haitatufanya tuwe wakabila
Makabile fahari ya ujinga tu.Mtu ambaye anataka maendeleo hawezi endekeza ukabila.ukimuona MTU anaendekeza ukabila mtazame maisha yake yalivyo utajua
 
Vilugha vyenu hukooooo mkija town lugha moja tu
Ndio maana hizo tauni zimejaa vibao vya 'usikojoe hapa', kielelezo cha ustaarabu mdogo!
Wenye vilugha vyao ni aibu kubwa na fedheha kukojoa sehemu ya wazi na hadharani.
 
Hapa ni kuimpose hoja mkuu Toyota escudo, mfano ni kusema wamasai hawapendi samaki kama wamanda! Pia kuoleana hata hapa Tanzania tunaoana lakini kuna pia watu ambao wanakuwa reluctant kuwaoa wengine. Mfano wa karibuni hauusiani hata na makabila bali utasikia mtu anasema ukioa aliyesoma umekwisha ...huu sio ubaguzi!?
Alafu ubaguzi mwingine unategemea aina ya siasa na kwa sasa unaona hata Tanzania mfano Wachaga, wanyakyusa au Wahaya wao kwa wao wanaweza kubaguana sababu ya vyama wanavyotokea ..refer mikutano ya siasa watu wanapigwa hadi mabomu wakati lengo lao ni moja na wote ni masikini. Nakuhakikishia hata jamii moja mnaweza kubaguana sababu ya koo zenu.
Ninachotaka kusema hapa ni kwamba 'disagreement' ni kitu kilichomo kwenye aslili ya uumbaji na hakiwezi kuisha mpaka labda binadamu atakapoacha kuishi duniani. Kwa hiyo suluhisho sio elimination (kuua lugha asili) ya kimojawapo bali to face the challenges of living together then mnagundua ule ukweli kwamba kila mmoja anamtegemea mwingine.
Ndio, suala la ubaguzi limejikita kwenye vitu vingi kweli kweli! Mifano uliyotoa ni dhahili, ni baadhi ya hivyo!

Umetoa mfano wa watu kubagua kuoa wasomi, ni kweli! Lakini utakubaliana na mimi kuwa vyuoni watu hubaguana kwa masomo wanayosoma!

Yaani ni vurugu tupu!

Anyway, hii ni off topic kidogo! I apologize
 
Can you tell me one, (only one) TANGIBLE thing I'll get after promoting my Beautiful Kihehe in Public ?
We don't need them as a Nation. Trust me.
Mimi naongea sana kilugha nikiwa home kijijini always. Lakini Kiswahili ni Muhimu zaidi.

Can you tell me one, (only one) TANGIBLE thing I'll get after promoting Kiswahili in Public ?
 
Back
Top Bottom