Je, asilimia ngapi ya Watanzania wanaelewa ama wanazungumza lugha ya kiingereza?

nasrimgambo

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
1,858
2,348
Japokuwa watu wa sensa huuliza lugha za watu, inaonekana ni moja ya takwimu ambazo huwa hawajisumbui kuzitaja.

Pengine huonekana si muhimu, ama pengine watu huwa hawaiulizii hiyo takwimu.

Ila, binafsi, naamini kingereza hadi sasa kipo kwenye tano bora ya lugha zinazoongelewa zaidi nchini, ama, basi tuseme walau zinazoeleweka zaidi na watanzania

Hadi sasa wazungumzaji wa kingereza kwa ujumla wao wanazidi idadi ya wazungumzaji wa lugha nyingi za makabila.

Siamini wazungumzaji wa Kiingereza wamepitwa kiidadi na wazungumzaji wa lugha kama Kizaramo, kihehe, Kimasai, au kichaga na kadhalika, zingatia sio wazungumzaji wa hizo lugha kwa ujumla wao, bali kama lugha moja moja na wazungumzaji wake kivyake, kisha linganisha na kingereza na wazungumzaji wake kama lugha moja pia

Hivi kwa mijini tunamoishi, unadhani wangapi kiidadi baada ya Kiswahili wanaweza kuzungumza lugha zao zile za asili kwa uzuri kabisa, haya, je, wangapi kiidadi baada ya Kiswahili wanaweza kuelewa ama kuzungumza kingereza? Unadhani wepi ni wengi, je, ni watanzania wawezao lugha zao za asili ama wale ambao kingereza ndio lugha yao ya pili?

Haya ni maoni yangu, wewe unaonaje?
 
Badala ya kufanya tafiti wewe unaleta mambo ya imani, kwahiyo usipoamini wewe basi inakuwa hivyo?
 
Hizo takwimu zinatumika wap?, nimekuwa nikiwasikia viongozi wa juu wa serikali wakisema kwa mujibu wa sensa za 2012 tupo watu zaidi ya million 60, cha ajabu hawatumii takwimu za sensa ya 2022.
 
Unataka kugundua Nini!??
Mimi nataka kubaini tu ukweli wa mambo,
Je, ni kweli uzungumzaji wa lugha ya kingereza upo chini humu nchini kama watu wanavyodhania?
Kwa sisi tunaoishi na kule twitter ni kawaida sana watu hasa wakenya kudai kuwa kingereza hakizungumzwi Tanzania.

Kwa uzoefu wangu nimekuwa nikifikiri kuwa, pengine wanaodhani kingereza kinaongelewa kwa udogo wanakuza udogo huo, pengine ndio, kingereza kinaongelewa na wachache, ila huwa nahisi huenda si wachache kihivyo kama inavyodhaniwa
 
Kiswahili, kidogo kiarabu na kisukuma nimeridhika.

Kiingereza ❌ na wala sina time nayo
 
Tuanze na huyo aliyesema tupewe elimu ya katiba. Je anaiweza kuiongea vizuri lugha ya kuzungu kwa ufasaha, au ndio kama mtangulizi mwenzake
 
Japokuwa watu wa sensa huuliza lugha za watu, inaonekana ni moja ya takwimu ambazo huwa hawajisumbui kuzitaja.

Pengine huonekana si muhimu, ama pengine watu huwa hawaiulizii hiyo takwimu.

Ila, binafsi, naamini kingereza hadi sasa kipo kwenye tano bora ya lugha zinazoongelewa zaidi nchini, ama, basi tuseme walau zinazoeleweka zaidi na watanzania

Hadi sasa wazungumzaji wa kingereza kwa ujumla wao wanazidi idadi ya wazungumzaji wa lugha nyingi za makabila.

Siamini wazungumzaji wa Kiingereza wamepitwa kiidadi na wazungumzaji wa lugha kama Kizaramo, kihehe, Kimasai, au kichaga na kadhalika, zingatia sio wazungumzaji wa hizo lugha kwa ujumla wao, bali kama lugha moja moja na wazungumzaji wake kivyake, kisha linganisha na kingereza na wazungumzaji wake kama lugha moja pia

Hivi kwa mijini tunamoishi, unadhani wangapi kiidadi baada ya Kiswahili wanaweza kuzungumza lugha zao zile za asili kwa uzuri kabisa, haya, je, wangapi kiidadi baada ya Kiswahili wanaweza kuelewa ama kuzungumza kingereza? Unadhani wepi ni wengi, je, ni watanzania wawezao lugha zao za asili ama wale ambao kingereza ndio lugha yao ya pili?

Haya ni maoni yangu, wewe unaonaje?
kijijini kweli kiswahili na kiingereza si muhimu sana.

tunakijua zaidi kile cha kwenye mamuvi ya kivita na ngumi kali ya akina anold shuzniga, Jetlii, cheknorisi, vandame, au silvesta Rambo kiingereza za humu hata ukimute sauti nikicheki muvi hadi mwisho baadae nakutafsria movi nzima kwa lugha yangu.

una far nchezo nn
 
Tuanze na huyo aliyesema tupewe elimu ya katiba. Je anaiweza kuiongea vizuri lugha ya kuzungu kwa ufasaha, au ndio kama mtangulizi mwenzake
Anaweza kuongea, mara nyingi mbona tunauon anatoa speech za kingereza kila akutanapo na wageni wa nje. Tena anacho kile cha kuremba kabisa, sio adoado cha form four
 
Back
Top Bottom