Kisutu: Mahakama yawafutia Mashtaka Harry Kitilya na wenzake, Polisi yawakamata tena

Dunia hii, yani binadamu mwenzako anaweza kuamua tu kukuweka ndani miaka minne halafu anakuja kusema hana haja ya kuendelea na kesi..kisha unashikwa tena pengine wakufungulie kesi iendelee miaka mingine minne ukiwa ndani tena... Very Unfair!
 
Mahakama ya Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya na maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, hata hivyo wamekamatwa tena na kurudishwa mahabusu.

-----------
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya na mwenzake wawili ambao ni maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon.

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo ya kutakatisha fedha.

Wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Uamuzi huo imefikiwa leo Januari 11 na Hakimu Mkazi, Salum Ally baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kueleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole akisaidia na wenzake Pendo Mangole na Patrick Mwida, amedai mahakamani hapo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

"Taarifa hii ya kutokuendelea na shauri hili mbele ya mahakama yako, imeletwa chini kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002," amesema Ngole.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Ally alisema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kuwekwa mahabusu.

Chanzo Mwananchi

Habari zaidi, soma=>Harry Kitilya, Sioi Sumari na Shose Sinare wafikishwa mahakamani - JamiiForums
Magu anataka hela.tu anajua kuwatia hatiani hawezi kilichobaki in kuwatisha watoe hela
 
Duuh aisee, labda wanataka waanze upya kutafuta ushaihidi,ila nikwanini huwa wanafungua kesi na kutesa watu wakati ushahidi haupo?
 
Wamehenya sana hawa jamaa! Mimi si mwanasheria lakini nafikiri kuna kitu hakiko sawa hapa. Yawezekana wanataka kuwafungulia mashitaka mengine baada ya kuona kuwa yale uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha hayana mashiko kisheria. Wamedhamiria kuwatesa watu na sijui wanafaidikaje! Anyway, yana mwisho haya!

kwa hiyo wewe ni hakimu kabisa

una majibu yote
 
Pole sana kwa hawa watu yani hata kama umeiba mabilioni lkn kwa misukosuko hii ya miaka 3 unaona hata bora usingechukua hiyo pesa
 
Mahakama ya Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishna wa TRA, Harry Kitilya na maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon, hata hivyo wamekamatwa tena na kurudishwa mahabusu.

-----------
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka aliyekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya na mwenzake wawili ambao ni maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon.

Washtakiwa hao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka nane yakiwemo ya kutakatisha fedha.

Wamefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Uamuzi huo imefikiwa leo Januari 11 na Hakimu Mkazi, Salum Ally baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kueleza mahakama hiyo kuwa hana nia ya kuendelea na shauri hilo.

Wakili Mkuu wa Serikali, Hashimu Ngole akisaidia na wenzake Pendo Mangole na Patrick Mwida, amedai mahakamani hapo kuwa DPP hana nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

"Taarifa hii ya kutokuendelea na shauri hili mbele ya mahakama yako, imeletwa chini kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002," amesema Ngole.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Ally alisema kutokana na maombi hayo, mahakama hiyo imeifuta kesi hiyo.

Hata hivyo, washtakiwa hao baada ya kufutiwa kesi hiyo, wamekamatwa tena na kuwekwa mahabusu.

Chanzo Mwananchi

Habari zaidi, soma=>Harry Kitilya, Sioi Sumari na Shose Sinare wafikishwa mahakamani - JamiiForums
Ni mtindo wa kubadirisha mashitaka.
 
Naona matumizi mabaya ya kifungu cha 91(1),
Hizo fedha wamezirudisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamehenya sana hawa jamaa! Mimi si mwanasheria lakini nafikiri kuna kitu hakiko sawa hapa. Yawezekana wanataka kuwafungulia mashitaka mengine baada ya kuona kuwa yale uhujumu uchumi na utakatishaji wa fedha hayana mashiko kisheria. Wamedhamiria kuwatesa watu na sijui wanafaidikaje! Anyway, yana mwisho haya!
Wanatafuta makosa ya kudhaminika na kupata Mtonyo....
 
Back
Top Bottom