Hizi hapa sababu za Kitilya na wenzake kupinga makubaliano ya 'Plea Bargain' na DPP

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,098
Aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wawili wamekimbilia Mahakama ya Rufani kuomba kuruhusiwa kupinga makubaliano baina yao na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), yaliyowatia hatiani katika kesi ya uhujumu uchumi iliyokuwa ikiwakabili.

Kitilya, Shose Sinare na Sioi Solomon wamekata rufaa mahakamani hapo wakipinga uamuzi wa Mahakama Kuu iliyotupilia mbali maombi yao ya kuongezewa muda kufungua shauri la maombi ya kutengua hukumu iliyowatia hatiani.

Kwa mujibu wa wakili wao, Zaharani Sinare, hukumu hiyo ilitokana na makubalino yasiyo halali baina yao na DPP wakidai yalifikiwa bila hiyari yao.

Watatu hao na wenzao wengine wawili--Bedason Shallanda na Alfred Misana walitiwa hatiani na Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Agosti 25, 2020 kutokana na makubaliano na DPP katika kesi ya uhujumu uchumi namba 4 ya mwaka 2019 iliyokuwa ikiwakabili.

Walihukumiwa kulipa faini ya Sh1 milioni kila mmoja na fidia ya Sh1.5 bilioni kama walivyokubaliana baada ya majadiliano baina yao na DPP.

Lakini mwaka 2022, takribani miaka miwili baada ya hukumu hiyo, Kitilya, Shose na Solomon walifungua shauri la maombi ya kuongezewa muda wafungue shauri la maombi ya kutengeua hukumu hiyo.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo walidai walichelewa kufungua shauri la kutengua hukumu hiyo kwa kuwa walikuwa wanasubiri kupatiwa nakala za mwenendo wa kesi hiyo walizoziomba tangu Oktoba 5, 2020.

Mahakama Kuu katika uamuzi wake ulioutoa Agosti 19, 2022, ilikubaliana na hoja za Serikali na ikayatupilia mbali maombi hayo ya kuongezewa muda ikieleza pamoja na mambo mengine watoa maombi hawakutoa sababu za kuchelewa kuishawishi mahakama kuwaongezea muda.

Mahakama hiyo katika uamuzi huo uliotolewa na Jaji Immaculata Banzi ilikubaliana na hoja za Serikali kupitia kwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Christopher Msigwa kuwa namna majadiliano yalivyofanyika si sehemu ya mwenendo wa mahakama isipokuwa makubaliano yaliyowasilishwa mahakamani.

Alisema kwa kuwa tayari walikuwa na nakala ya makubaliano hayo waliyoyasaini, hapakuwa na haya ya kusubiri kupata mwenendo wote wa kesi.

Katika rufaa hiyo, kina Kitilya wamewasilisha sababu sita kuonyesha mahakama hiyo ilikosea kutupilia mbali maombi yao.

Pamoja na sababu nyingine wanadai mahakama ilikosea kuamua kuwa kutokuhiyari kwao (katika majadiliano na makubaliano) hakuwezi kuonekana katika mwenendo wake na kwamba kukataa kuwa mwenendo wa majadiliano si sehemu ya mwenendo wa kesi wa mahakama.

Pia wanadai mahakama hiyo ilikosea kuamua kwamba wangeweza kufungua shauri la maombi ya kutengua hukumu hiyo bila hata kuwa na mwenendo wa wa kesi na kwamba ilikosea kulichukulia shauri hilo la maombi ya kuongezewa muda kama shauri la maombi ya kutengua hukumu.

Katika kesi ya msingi walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 58 ya kuongoza uhalifu wa kupangwa, kughushi, kuwasilisha nyaraka za uongo, kumdanganya mwajiri kwa kutumia nyaraka, kujipatia fedha Dola za Marekani milioni sita kwa udanganyifu, utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara kiasi hicho cha fedha.

Walidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Februari 2012 na Juni 2015 katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na nje ya nchi wakati wa mchakato kuiwezesha Serikali kupata mkopo wa Dola za Marekeni 550milioni kutoka Benki ya Standard ya nchini Uingireza.

Wakati huo Kitilya alikuwa Mkurugenzi kampuni ya Enterprise Growth Market Advisors Limited (EGMA) iliyojishughulisha na ushauri wa uwekezaji na huduma za uwezeshaji na upatikanaji wa fedha, ambayo ndio ilikuwa ikidaiwa ilitumika kujipatia fedha hizo. Shose alikuwa alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wakubwa na Uwekezaji wa Stanbic Bank Tanzania Ltd na Solomon alikuwa Mkuu wa Idara ya Sheria na Katibu wa kampuni wa benki hiyo.

Shallanda na Missana walikuwa watumishi wa Wizara ya Fedha waliokuwa wanahusika na masuala ya mikopo ya Serikali. Shallanda alikuwa Kamishna wa Uchambuzi wa Sera na Misana alikuwa Kamishna Msaidizi wa Usimamizi wa Madeni.

Hali ilivyo

Mbali na kina Kitilya ambao wamechukua hatua hizo za kisheria, pia kuna baadhi ya mawakili wa washtakiwa waliomaliza kesi zao kwa utaratibu huo ambao nao wameshaibua malalamiko kama hayo.

Wakili Gaspar Nyika alikuwa akimtetea aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom, Hisham Hendi na wenzake katika kesi ya uhujumu uchumi wakidaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh5.8 bilioni.

Alisema ingawa wao walikuwa wanaona hakuna ushahidi wa kuwatia hatiani, lakini wakati wanafuatilia hatima ya kesi hiyo DPP alidai kama wanataka kesi hiyo iishe wateja wake walipe fidia ya fedha walizokuwa wanadaiwa na kama hawako tayari waendelee na kesi mahakamani.

Wengine waliozungumzia na kukosoa utaratibu huo wa majadiliano katika mitandao ya kijamii ni mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera aliyekuwa mmoja wa waathirika.

Kabendera ambaye pia alikuwa akikabiliwa na kesi iliyomalizika kwa utaratibu huo aliwahi kuandika katika ukrasa wake wa twitter akitoa tuhuma kuwa kuna washtakiwa waliolazimishwa kutoa fedha, ili wakubaliwe kufanya majadiliano.

Pia aliwataka wafanyabiashara waliotishwa na maofisa wa Serikali kutoa fedha wajitokeze, akisema uchunguzi kama huo ulishawahi kufanyika wakati wa uongozi wa awamu ya pili, waliohusishwa na uhujumu uchumi na baadhi wakarudishiwa mali zao.

MWANANCHI
 
Cha kushangaza utakuta hizo hela watakazo rejeshewa, zinatoka kwenye hizi kodi na tozo tunazokatwa kila siku na akina Lameck!

Maana hizo hela walizolipa baada ya kuingia makubaliano na huyo DPP, unaweza kukuta hazijulikani zilipo!! Nchi ngumu sana hii!
 
Cha kushangaza utakuta hizo hela watakazo rejeshewa, zinatoka kwenye hizi kodi na tozo tunazokatwa kila siku na akina Lameck!

Maana hizo hela walizolipa baada ya kuingia makubaliano na huyo DPP, unaweza kukuta hazijulikani zilipo!! Nchi ngumu sana hii!
409A2B2E-1883-4204-9A07-832071C77C97.png
 
Wenye bank wenyewe walikiri huko kwao na wakapigwa fidia ya kutosha ila huku walio facilitate wanataka kukata rufaa...hii issue ni km ile ya rada ambayo waingereza waliturudishia mpunga waliotupiga ila wabongo waliofacilitate hawakuwahi kufikishwa Mahakamani...pathetic
 
Back
Top Bottom