Kesi Pauline Gekul tutafute Mahakama ya Kiroho hii ni "Dawa ya Wanasiasa wa Tanzania kushughulika nao kiroho tu, utawala hakuna

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara imefuta shauri la jinai lililofunguliwa na Wakili Peter Madeleka dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Paulina Gekul la kumfanyia shambulio la mwili Hashim Ally.

Uamuzi huo umetolewa leo December 27,2023 na Hakimu Mkazi wilaya ya Babati Victor Kimario baada ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali kuona hana nia ya kuendelea na kesi hiyo na ameiondoa kwa mujibu wa kifungu cha 91 (1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai sura ya 20 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2022 ambayo inamoa DPP Mamlaka ya kuondoa kesi yoyote ya jinai Mahakamani kabla haijafikia hukumu.

Nje ya Mahakama, Wakili wa upande wa Mlalamikaji, Peter Madeleka amesema wanakusudia kukata rufaa kwa kuwa hawajaridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama.

Madeleka akiwa na Mawakili wengine Thadei Lister na Peter Masanja walifungua kesi dhidi ya Mbunge Paulina Gekul wakidai alimfanyia kitendo hicho Hashim Ali kwa kumuingizia chupa sehemu ya haja kubwa, upande wa Mshtakiwa uliwakilishwa na Wakili Ephraim Kisanga.

Take!!!
Mambo kama haya ndio yanafanyaga nione wachawi wana msaada muda mwingine.

Piga kirogo kimoja kitakatifu kiasi wanasiasa wengine watajifikiria mara 2 kabla hawajafanya upuuzi
 
Back
Top Bottom