Kisirani kwa wa dada wenye 30 and above

Kisirani kwa wa dada wenye 30 and above

mutant gene

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
876
Reaction score
326
Habari zenu wakuu.

natumai mtakuwa mnaendelea vyema na majukumu ya kulipeleka mbele gurudumu la Tanzania.

Kuna hiki kitu huwa najiuliza lakini sipati jibu, hivi kwanini wadada ambao wana 30 na kuendelea wanakuwa visirani sana, unakuta dada ananuna bila ya sababu muda wote, maana hata kazi haziendi, ukimuambia hivi kosa, ukimuambia vile kosa. Mtu unabaki unajiuliza me ndio niliokufanya usiolewe au nilikutia mikosi.

Basi sawa hata kama ndio mna stress zenu, msije nazo mpaka sehemu za kazi mziache nyumbani kwenu.

Kitu kingine ambacho kinashangaza, nyie huwa mnasema "kuolewa ni bahati", sasa mpaka umri uliokuwa nao kwanini usikubali matokeo kuwa hauna bahati ya kuolewa, kina dada msifanye hivyo bhana kama umeamua kuja kazini njoo stress zenu kwenu.

Natumai wahusika mtakuwa mmeupokea ujumbe na kuufanyia kazi, mnatukwaza wenzenu bana, wengine hatupendi kuona mwanamke ananuna hana furaha.

Ni hayo tu.
 
nisamehe buree
eti nimeusoma uzi wako nikapata picha eti wewe ni subordinate wa mdada ofcn kwenu
af mdada amekuwa mkali so ukaamua kumjengea hioja kwamba ni mkali kisa hajaaolewa
kumbe sio kweli, mzembe ni wewe na anakugombeza kisa uzembe wako
jiongeze na wewe ili usiwe subordinate.

af sjui kwann hili ni kwazo sana kwa wakaka yaan bosi akiwa mdada tu ataandamwa hadi akome, mara oooh ana mastress ya kutoolewa, akiolewa mara ooh ana stress za ndoa, hakunaga jema jaman mdada akiwa bosi
 
nimewahi kuwa na boss wa aina hiyo mahala fulani..yani alikuwa anajinunisha mpaka kero!!

jaman wanawake tuna tabu.......
so kama hajazaa akinuna kisa ni hana mtt
kama hajaolewa akinuna kisa ni hana mume
sasa kama kaolewa na ana mtt akinuna kisa huwa ni nini?

mbona vitu vingine ni tabia tu na wala havina uhusiano na status za watu?
 
jaman wanawake tuna tabu.......
so kama hajazaa akinuna kisa ni hana mtt
kama hajaolewa akinuna kisa ni hana mume
sasa kama kaolewa na ana mtt akinuna kisa huwa ni nini?

mbona vitu vingine ni tabia tu na wala havina uhusiano na status za watu?

uhusiano upo sana mkuu, mjirekebishe basi.
 
Stress mbaya sana, na hii inawaathiri wanawake zaidi. Hata performance Yao makazini inapungua. Wengine wala sio mabosi lakini unaona wanavyoumia rohoni, ukimgusa tu hata kwa utani umeharibu.

Sio stress za ndoa tu, hata tamu. Kama mdada amekaa mda mrefu sana bila kupewa dozi anakuwa restless na mistress, mawazo na performance kazini huwa sio nzuri.
 
Si uwaambie live hao unaofanya nao kazi wenye hizo Tabia?
Watu kuja na stress kazini haina jinsia wala status best,wapo Me wanaokuja na stress zao Sema wengi hawana kaba za ulimi ukimuuliza tu atasimulia mpaka ya chumbani. Wanawake wana vifua yao hawayatoi hovyo ndio mnajimaliza tu kwa kuwadhania,Mara Kisa hana mtoto,Mara hana mume,Mara kaolewa na mzee hapati dose ya uhakika!!!!
 
ila kweli jamani nna mam angu mdodo ana38 hana mtoto han ndoa jamani utamuonea huruma anastress,vitu vidogo vidogo kwake bonge la ishu
uyamuonea huruma hata mchumba hana
 
"""tu unabaki unajiuliza me ndio niliokufanya usiolewe/ nilikutia mikosi!"""


Kwa hiyo walioolewa ndio wanafuraha !!! are you serious ?? acheni kunyanyapaa wanawake na kuwatafutia visababu kisa kutoolewa , kwa Taarifa yako huyo angekuwa kaolewa ingekuwa x2 ! hiyo ni tabia Binafsi



 
Pia muda mwingine menopause inachangia, na at 30's kwa wengine ndo dalili zinaanza kujitokeza....hata kama kaolewa anaweza kuwa kisirani hatari....!
 
Back
Top Bottom