Kisingizio: Daftari la Wapiga Kura, vyombo vya dola. Sababu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Daftari la wapiga kura na vyombo vya dola vitabebeshwa lawama na labda vinastahili. Lakini katika hili CHADEMA inapaswa kutoa sababu zinazoeleweka zaidi ya visingizio.

Wanachama, wapenzi, na mashabiki wa CHADEMA wanapaswa kuwa wakali kidogo (au sana) ili chama kiweze kutoa maelezo yanayoeleweka ya kwanini matokeo haya hayakuwa mazuri kama watu walivyokuwa wanaaminishwa au kutarajia. Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 CHADEMA ilitakiwa iwe inasukumwa na upepo wa ushindi lakini hali sivyo ilivyo.

Kama majibu ya kueleweka hayapo ipo haja ya haraka ya kuanza kudai watu wawajibike au wawajibishwe.

To be continued....
 
Mnapoteza muda wenu bure, Chadema haiwezi kushindwa pale anaposimamishwa mtu anayekubalika katika eneo husika, bado Chadema ina tatizo kwenye eneo hili, inao watu wengi sana wanaoiunga mkono lakini hawako tayari kusimama kwenye majukwaa ya siasa. hata mimi binafsi siwezi kupimgia kura mgombea mbovu eti kisa ni wa Chadema.
 
Sioni mtu wa kuwajibishwa ila naona haja ya watu kupongezwa na kutiwa moyo na kuambiwa songa mbele.kata zilizoongezeka ni kura za watu waloipigia kura ccm 2010...Watu waelimishwe na kuhamasishwa wakajiandikishe.
 
muhimu cdm iwe inashawishi watu makini wanaokubalika ktk jamii kugombea,kwa ujumla wananchi wameichoka ccm
 
Mm lawama katika daftari la wapiga kura haikwepeki ni moja ya udhalimu ccm inatumia kushinda. Utakuta kituo kina wapiga kura km 400 lakini watakao piga kura ni km 80 wengine mara majina yao hayapo,yamekosewa na hasa vijana ambao ni wafuasi wakubwa wa chadema. Kwanini daftari la kura halifanyiwi mabadiliko tokea 2010 mpaka sasa kuna mabadiliko makubwa. Hongera chadema toka ziro hadi moja ni hatua nzuri.
 
Mzee Mwanakijiji

Mkuu,

Tathimini yako na wengine kwa haraka haraka ni rahisi kukurupuka kuwa Chadema kimeshindwa...

Hatuna sababu ya kuwa wakali wala kutafuta sababu, uzuri wanachadema tunazijua sababu,


Kwa hili ungewashauri CCM, wajitadhimini na waje na sababu kwa nini wanazidi kuporomoka...uchaguzi huu wamepoteza viti 3 vya udiwani...Chadema tumeongeza, sasa sijui nani aje na hizo sababu...

Mkuu MMK, kama Tanzania tungekuwa na Democrasia ya Kweli...Nami ningeungana nawe, kuwakosoa na kuwaponda viongozi wetu, lakini kwa jinsi uwanja wa demokrasia ulivyo, CDM wamejitahidi sana,, nikuulize kidogo tu...
1. Unafahamu kuna kesi ngapi zinazowakabili viongozi wakuu wa CDM mpaka sasa?
2. Kesi ngapi kwa mashabiki na wapenz wa Cdm mpaka sasa?
3.Kuna mashabiki wangapi wa CDM wamekufa mpaka sasa?
4.Kuna walemavu, wagonjwa, walioteswa wa CDM mpaka sasa?

MzeeMwanakijiji, Tanzania ni zaidi ya ujiavyoo..., Chadema tunawapongeza sana tena sana, endeleeni viongozi wetu tupo nyuma yenu.
 
Last edited by a moderator:
Suala la kuwawajibisha viongozi wa CHADEMA sikubaliani nalo kabisa kwa sababu kazi wanazozifanya zinaonekana na zinakubalika kwa wananchi. Kushindwa kwa CHADEMA kufanya vizuri zaidi ni kutokana na mambo makuu mawili.

Kutokuboreshwa kwa daftari la wapiga kura na pia rushwa kutawala sana katika chaguzi. Ninaamini kwa dhati kabisa ya kwamba endapo daftari la wapiga kura litaboreshwa basi CHADEMA itafanya vizuri zaidi. Ni jukumu la CHADEMA kwa sasa kupigania kwa nguvu zote daftari la wapiga kura kuboreshwa.

Tuungane katika hili.
 
Mzee mwanakijiji, naona kama uko comfotable na hili swala la kulinda kura yako kama unalinda kipusa, kana kwamba tishio la kupotezwa kwa kura stahiki pamoja na maamuzi yake unali downplay kama si kulikubali, ni kama hujathamini michango ya hali na mali waliyojitolea wananchi kwa cdm pamoja na madhara waliyoyapata wakiwa njiani.

Watu wamevunjiwa magari kwenye harakati, wengine wameumizwa vibaya sana wakikipigania chama na haki kupiga kura. enewei tunasubiri continuation yako.
 
Ningetamani kuona mchanganuo wa kura kwa maana ya kila chama kilipata nini ktk uchaguzi uliopita kwa maana ya idadi ya kura kulinganisha na jana ili kuona swing ikoje...

Wakati mwingine kushinda isimaanishe kuchukua kiti peke yake......ingawa lengo ni kuchukua kiti.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hivi ni mpaka lini tutaendelea kuamin kuwa mashinikizo ya kisiasa yatatupa matokeo
tunayoyakusudia? Tulishashuhudia namna CDM walivyoshinikiza hili tangu kule igunga lakin bado matokeo yake hayakuwa chanya, sasa ni kwa ni bado mnataka tuwashinikize washinikize? Je ingewafaa nin kwa sasa kama wangeamua kususia uchaguzi huu?

Mimi nadhan wakati wa mashinikizo ya kisiasa umepita sasa tuanze mapambano ya kisheria. Kama suala la kupiga kura ni HAKI kwa kila Mtanzania mwenye miaka 18+, ni kwa nini mpaka sasa hawa watanzania wanaonyimwa haki zao hawajaiburuza tume ya uchaguzi mahakaman? Katika hili watu wa LHRC na CHRGG wako wapi?

Na hapa tulitegemea kitengo cha sheria na haki za binadamu ndan ya CDM kitoe msaada zaidi kama kwel waliopokwa haki hizo ni wafuasi wao.
 
Daftari la wapiga kura na vyombo vya dola vitabebeshwa lawama na labda vinastahili. Lakini katika hili CDM inapaswa kutoa sababu zinazoeleweka zaidi ya visingizio.

Hapo kwenye red sio jambo dogo hilo, Lina nguvu kubwa yakubadilisha matokeo!

Wakati CDM inajijenga kwa kasi majukwaani,Tusisahau ccm nayo ilikuwa bize kuratibu mbinu chafu za uchaguzi.CDM bado inayo miezi 36 ya kuendelea kujijenga na kufanya marekebisho makubwa.Wajaribu kuutathmini matokeo haya kwa kina zaidi,then waje na very contractives strategies kuimaliza ccm.
 
Mzee Mwanakijiji hapo siungani na wewe, kwa nini???

Watu wanapigwa wanaumizwa na wapiga kura kurubuniwa kuuza shahada za kupigia kura halafu bado unalalama mkuu.

CDM wamejitahidi sana hata sehemu walizoshindwa ni kwa idadi ya kura ndogo tofauti na sehemu ambazo CDM inakubalika!!!

Watu hawana meno, wanauawa ili kujenga mirrage ja vurugu juu ya CDM.

Daftari ni lile la wapiga kura, yaani saizi tunatumia mtaji wa CCM kuchagua CDM, ngoja ifike 2015 tuongeze nguvu ya mtaji kwa kuongeza watu ambao ndiyo wanaoiaminisha CDM kushinda lakini hawana shahada.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji

Hapa kidogo utakuwa umekosea. Kuanza kuleta mada ya kuaandalia uongozi wa CDM uwe na mazingira ya kuonekana kufail wakati hakuna failure hapo.

Kumbuka CDM ilikuwa na kata chache tu nadhani kufanikiwa kupata kata nyingine 3 ni maendeleo makubwa sana. Kumbuka jitihada hizi zinafanywa na watu wanaofikiria pia. Na hata kufika katika kiwango hiko cha kupata hizo kata pia ni juhudi kubwa zimetumika.

Unaposema unasubiria upate maelekezo ya nini kimetokea yanaweza yasikunufaishe wewe, zaidi ya kuwanufaisha wenyewe CDM kwenye kutambua ni wapi walipoteleza.

Hili sio anguko kwa CDM. Ni anguko kwa CCM kwa kupoteza kata. Hakuna wa kulaumiwa zaidi ya kupongezwa ingawa matarajio yamekuwa hasi kidogo. Kutafuta ukombozi sio kukaa ofisini watakufa watu wengi mpaka kufikia ukombozi kamili.
 
Last edited by a moderator:
Sina taarifa yoyote kama chama kimetoa taarifa ya tathmini ya chaguzi hizi za jana. Nadhani wakitoa tathmini ndipo tutajua wapi palikwenda vibaya, nani alisababisha tushindwe kuibuka na ushindi mkubwa kama tulivyotarajia na ni mambo gani tunapaswa kufanya ili wakati mwingine tupate ushindi mkubwa zaidi ya huu wa jana.

Hata hivyo kwa kupata kata tano si ushindi mkubwa sana wa kujivunia bali pia hiyo inaonyesha mafanikio madogo yapo kwakuwa tulikuwa tumepoteza madiwani wawili, ambao tumeweza kutetea viti hivyo na pia tumefanikiwa kupata viti vingine vitatu vya ziada vilivyokuwa vimeshikiliwa na ccm hapo awali.

Nadhani tusubiri taarifa rasmi ya chama ili tuweze kuijadili kwa kina na kutoa mapendekezo yatakayotusaidia kuboresha namna tunavyoshiriki chaguzi. Kwa sasa tuwapongeze wanachama na viongozi wote walioshiriki kwa namna mbalimbali katika chaguzi hizi ndogo zilizokamilika jana.
 
Mzee Mwanakijiji

Kimsingi mie sikuwa na matarajio makubwa sana na nilimwambia rafiki yangu kuwa chadema wakipata japo kata Tano kwenye hizi chaguzi basi watakuwa wamefanya vizuri kwani nimekulia kijijini najua wapiga kura wa kijijini walivyo. Rafiki yangu yeye alitegemea kupata hata kata ishirini kutokana na upepo wa mikutano ya kampeni. CCM bado inakamtandao kule kijijini na bila CDM kupenyeza mtandao wake huko kijijini bado itakuwa ngumu kwa CDM kushinda vijijini. Kitu cha msingi ambacho CDM ni lazima ikifanye ni kuhakikisha kila kijiji wanauongozi(commited leadership) ambao pia kazi yake iwe ni kufungua machina ndani ya kijiji ili kuanza kuvunja mtandao wa CCM. Wananchi wa vijijini bado wanawasilkiliza viongozi wanachowaambia kufanya ndicho wanachofanya.

Pia tukumbuke viongozi hawa wa chini kabisa yaani mabalozi wa machina ndiyo hutumiwa na CCM kupeleka ahadi za rushwa na kuaandaa vikundi vya akina mama vya kuwahamasisha mama zetu ili wawe tayari kupokea chumvi na vitambaa vya CCM. Ni lazima CHADEMA wajuwe kuwa kura nyingi za kijijini ni za akina mama ambao ni wapokeaji wa rushwa wazuri na ni wagumu sana kuwabadilisha mpaka labda azuiwe na mme wake. Chama cha wanawake wa Chadema kinatakiwa kuliona hili lakini sidhani kama wanaliona na kama wanamkakati wowote wa kukisaidia chama kwa hili. Ukweli ni kwamba M4C inavuna vijana zaidi lakini si akina mama ambao ni wapiga kura wazuri na wanaohongeka kiurahisi sana huko vijijini. Chadema wanahitaji kukabiliana na hili la akina mama huko vijijini kwa kuanzisha operasheni special kwa ajili ya mama zetu huko vijijini la sivyo kupata mafaniakio kule vijijini itachukua muda sana!

Kuhusu suala kuboresha daftari nadhani kunahaja ya kuangalia kwa undani ni kipengele kipi katika sheria kinachowapa upenyo tume ya uchaguzi wasiboreshe daftari la wapiga kura! Mimi sijaisoma sheria hiyo vizuri lakini nadhani inataka tume ya uchaguzi iwe inaboresha daftari muda wote. Na ndhani pia kama sikosei inaruhusu mtu kwenda kwenye tume kujiandikisha na siyo lazima kusubiri tume itangaze kipindi cha kuandikisha. kama kuna mtu anayokaribu hiyo sheria aiweke hapa tuiangalia kwa mapana na kuona ni hatua gani za kisheria CHADEMA wanaweza kuchukua dhidi ya jambo hili.

Kama CHADEMA wanataka kuona matunda ya kampeni zao ni lazima watumie kila fursa za kisheria zilizopo kuhakikisha TUME ina comply na haki inatendeka. Nadhani CHADEMA wanahitaji kuchukua hatua kali pale wanapoona haki haitendeki na sikuishia kulalamika tu.
 
Last edited by a moderator:
Hv ni lini? katika harakati hizi za CDM tulisikia chombo cha dola au kiongozi aliyetumia madaraka yake vibaya ameburuzwa kortini kwa kesi za madai (civil) au madhara (tort), hizo za jinai tumuachie Jamhuri. Labda tuingie ndan zaidi.

Hivi ni kweli kwamba Mjane wa Mwangosi hawezi kuishtaki serikali na kudai fidia? Hv ni kweli kwamba RPC Kamuhanda hawezi kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka kama alitenda kinyume na taratibu za ofisi yake?

Tuache utani hivi vyombo vya Dola vinaendelea kupata kiburi kutokana na ukimya wetu, kutokana na ukimya wa wanaharakati wetu na kutokana na ukimya wa wanasheria wetu.
UKIMYA WETU NDIO SILAHA YAO
 
Ina maana hawa waliojiandikisha kwenye daftari la kudumu huwa hawa shawishiki kupigia kura upinzani?Mpaka wapatikane wapika kura wapya?
Kwa maaana hiyo Chadema katika movement zake imeshindwa kushawishi wapiga kura waliopo sasa kukipa kura?Wameweza kata 3?Harakati na operaion kibao za miaka miwili wamefanikiwa kata 3 mpya?Je miaka 3 ijayo mpaka kufikia uchaguzi ujao kata ngapi zitaongezeka?Ubunge je?Urais?
Ikumbukwe walizungusha makamanda wao wote kwenye maeneo yote yaliofanyika uchaguzi!Dr.Slaa na viongozi wote !
Chadema watulie wajipange,wajitulize kusonga mbele!
 
Daftari la wapiga kura na vyombo vya dola vitabebeshwa lawama na labda vinastahili. Lakini katika hili CHADEMA inapaswa kutoa sababu zinazoeleweka zaidi ya visingizio.

Wanachama, wapenzi, na mashabiki wa CHADEMA wanapaswa kuwa wakali kidogo (au sana) ili chama kiweze kutoa maelezo yanayoeleweka ya kwanini matokeo haya hayakuwa mazuri kama watu walivyokuwa wanaaminishwa au kutarajia. Kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 CHADEMA ilitakiwa iwe inasukumwa na upepo wa ushindi lakini hali sivyo ilivyo.

Kama majibu ya kueleweka hayapo ipo haja ya haraka ya kuanza kudai watu wawajibike au wawajibishwe.

To be continued....

Mzee wa kijiji naomba kuchangia wazo kidogo juu ya hoja yako ambayokwa kiwango fulani inaonesha huna furaha juu ya matokeo haya! hakika hata mimi sijafurahia.
Pamoja na kutaka viongozi wetu watoe sababu za kupata matokeo hayo, basi kabla yao naomba na mimi nitoe sababu moja ya msingi.
Kwa ujumla naomba kuwakumbusha wapenzi wa cdm kuwa chama kama chama kimejiongezea wanachama siku chache kabla ya uchaguzi wa 2010 na baada ya hapo namba imeendelea kuongezeka siku hadi siku. lakini kati ya wapenzi wengi wa cdm wa sasa kumbuka walikuja kuipenda cdm wakati maboresho ya daftari la wapiga kura yakiwa yameishafanyika, hivyo hadi sasa wengi wao ni wanachama wa moyoni lakini hawawezi kupiga kura kwani sheria haiwaruhusu.
USHAURI: Kwakuwa 2014 kutakuwa na uandikishaji upya wa daftari la wapiga kura, cdm ijipange kutoa elimu ya uraia ili kila mtu aone kuwa kupiga kura ni haki yake na ili upige kura lazima ujiandikishe. NI MAONI YANGU TU.
The BOSS, POMPOO, MWITA MALANYA, MCHAMBUZI mpo hapo? karibuni
 
Back
Top Bottom