Kisa: Nini hutokea pale muoaji au muolewaji anapotokomea kusikojulikana baada ya kukusanya michango?

Monosex

JF-Expert Member
Jun 10, 2017
892
1,618
Salam Wakuu,

Ndani ya mada kabisa, Nataka kujua ni hali gani anakuwa na mtu kama huyu. Mapema January mwaka huu nilipata kadi ya kuchangia send-off kutoka kwa rafiki yangu, ambapo aliainisha mapema mwezi huu ata-agwa kutoka nyumbani kwao.

Kwa tamaduni za send-off, japo siyo mdau huwa naona baada ya send-off haichukui mwezi, harusi hiyo hapo.
Sasa kilichotokea kwa huyu rafiki yangu ambaye ni Mama wa mtoto wa kike, Ameleta mrejesho kuwa hilo tukio halitokuwepo hadi mwezi wa saba mwaka huu. Hivyo anayehitaji hela yake ya mchango atapatiwa kwa sasa au akihitaji kuibakiza hadi mwezi wa saba ni sawa pia.

Kwakuwa hapo kibaruani kuna majirani wa huyo rafiki yangu, inasemekana jamaa aliyetaka kuoa huyo mrembo wa rafiki yangu huyo ametokomea kusiko julikana.

Nahitaji kufahamu mambo haya..

1. Wewe muoaji nini huwa kinatokea katikati ukala kona au ulitumia mbinu za kuopoa utelezi wa pisi kali kwa gia ya ndoa feki?

2. Wewe unayeolewa ni hali gani unayopitia ili ku-recover kutoka katika hali kama hii?

3. Familia na kamati ya maandalizi ya send-off au harusi huwa mnapitia hali gani pia?

4. Kama imewahi kukutokea, send-off au harusi ilifanyika baada ya kusogezwa mbele au iliyeyuka? Mambo gani ya kisaikolojia ulipitia kwa kipindi hicho cha subira?

20230302_222122.jpg

Naomba kuwasilisha
 
Mbona kadi ya mchango wa vigodoro hii? Aliyekimbia yupo sahihi amejiokowa na kifo.

Sijawahi kuona mchango wa sherehe chini ya 50,000/= single.

Unless uniambie huyo alikuwa anakusanya pesa za kulipia mkopo wa kausha damu kwa kisingizio cha sendoff.
Mchango feki, hata vijijini haupo!😁😁😁
 
Mbona kadi ya mchango wa vigodoro hii? Aliyekimbia yupo sahihi amejiokowa na kifo.

Sijawahi kuona mchango wa sherehe chini ya 50,000/= single.

Unless uniambie huyo alikuwa anakusanya pesa za kulipia mkopo wa kausha damu kwa kisingizio cha sendoff.
Hahahahaha, ila hii issue ni serious, hiyo alitaka fanya kulingana na uwezo wake wa kiuchumi, nawaza hivyo.
 
huo mchango 😂😂huku kwetu uswahilini ni mchango wa kitchen party hapo unapata kijora/kitambaa na kadi .🤣🤣🤣🤣
Turudi kwenye mada sijawahi pitia hiyo hali..ngoja waje wenye walipitiamo humo
 
Hii mbona kawaida! Kuna jamaa mmoja alikusanya michango ya harusi yake. Alipokusanya fedha za kufanya sherehe ilipofika siku ya harusi akaenda bomani kufunga ndoa badala ya kanisani, na hela za kufanyia sherehe akazigeuza mtaji wa biashara akaanzisha duka
 
Back
Top Bottom