Na ni ngumu sana kupata waaminifu siku hizi kwenye biashara kama akina Sinbad. Ni dhuluma na kuuana
AiseeeMimi nampenda Yule mwenzake kk
Umeshamaliza kusimulia?SEHEMU 13
Basi bila kuchelewa tukaanza kazi ya kukusanya magogo kutoka katika rundo la magogo yaliorundikwa na lile jitu karibu na lile tanuri lake, tukayabeba nje tukayafunga pamoja imara. Tulipovitayarisha vyelezo yetu tukaviacha ufukweni.
Jioni km kawaida ardhi ikatetemeka kwa kishindo cha kuja kwa lile jitu huku likilia kama jibwa. Kuingia tu, lilimnyakua mmoja wetu aliekua mnene kuliko sote, likamtayarisha kwa mlo wake wa jioni lilipokula na kushiba, lilijinyoosha baoni na kama kawaida yake lililala usingizi mzito.
Hapo tukanyata kwa hadhari kubwa tukachukua nondo yenye ncha moja kali tukaitia motoni, iliposhika moto sana tukaibeba pamoja mpaka pale lile jitu lilipokuwa likikoroma kwa nguvu moja, tulilichoma nalo kwenye lile jicho lake moja huku sote tukiisukuma ile nondo kwa nguvu zetu zote.
Lo masalale! Lile jitu likaruka toka pale baoni likapaza sauti ya kutisha likajaribu kututafuka kwa kupapasa huku na huko kwa majikono yake makubwa marefu, lakini sisi tuliweza kulikwepa, liliposhindwa kutukamata lilipapasa ukuta mpaka likafika kwenye lile lango likafungua na kutoka nje huku likipiga makelele kwa maumivu.
Haraka tukatoka mle tukaelekea ufukweni tukaviburuza vile vyelezo vyetu mpaka majini, tukapanda tukaanza kipiga makafi, kabla hatujafika mbali mara tukaliona lile jitu tulilolipofoa likiongozwa na kundi kubwa la wenzake.
Yalipofika ufukweni yalisimama huku yakitupigia makelele mara yakanyanyua mapande makubwa ya mawe pale ufukweni yakaingia majini, yakatuvurumishia nayo moja baada ya jengine, kwa kuwa yalikua na shabaha yakavizamisha vyelezo yote ispokua kile nilichokuwemo Mimi na wenzangu wawili, kwa bahati nzuri sisi tuliweza kupiga makafi kwa nguvu na kufika mbali baharini ambako Yale majitu hayakuweza kutufikia.
Basi mchana kutwa na usiku kucha tukawa tunaelea baharini tukichukuliwa na mawimbi mpaka yakatufikisha kwenye ufukwe wa kisiwa kingine, kwa kuwa tulikua tumechoka sana na kwa ajili ya njaa na kiu tuliokua nayo tulijibwaga pale pwani mchangani tukalala.
Asubuhi ya pili tilipoamka tukashtuka kuona joka kubwa ajabu limejikunja mbele yetu! La haulaa! Kabla hatujaweza kufanya lolote lilinyanyua kichwa likafunua kinywa likamnyakua mmoja wa wale wenzangu, likammeza mzima mzima huku tikisikia jinsi mbavu za mwenzetu zikivunjika tumboni mwa lile joka kwa kujibana kwake.
Halafu lilijinyoosha na bila kutijali lilitiririka mchangani likatoweka msituni, "mungu we!" Tukapiga mayowe, "tuliokoka kifo kibaya cha kuchomwa kama mshkaki na sasa tunakikabili kifo kibaya zaidi cha kuliwa tungali hai! Yaa rabby! Tutaliokoka vipi hili joka?!"
Asubuhi ya pili jua lilipochomoza, sisi wawili tuliobaki tulipata nguvu kidogo tukawa tunatafuta chakula na maji ya kunywa, na kabla hakuja kuchwa tulitafuta mti mrefu tukaupanda, tukakalia tawi la juu kabisa kujisalimisha na lile joka.
Giza lilipoingia tulisikia kupumua kwa lile joka, lilipofika pale mtini tulipokua, lilitambaa juu lilimnyakua mwenzangu aliekua chini yangu likammeza likimbana na kumvunja mbavu tomboni mwake kama mwenzetu. Baada ya kufanya hivyo likatambaa chini likatoweka msituni, kusema kweli usiku kucha sikupata usingizi kwa woga na wasi wasi niliokua nao.
Asubuhi nikashuka mtini, fikra yangu ya kwanza ikawa ni kukitosa baharini na kufa Maji ili kuyamaliza maisha yangu ambayo yalikua yameshapambana na maafa mengi. Lakini nikashindwa kufanya hivyo kwani kujitoa roho si mchezo na maisha ni matamu japokua ni mafupi.
Hapo nilifanya mpango wa kujihami dhidi ya lile joka. Basi nilikusanya mabiwi na magogo na majiti makubwa mazito yenye miba, nikayafunga vizuri pamoja kama sanduku, jioni nilijitia mle ndani nikajifungia vizuri, baada muda lile joka likaja likanizunguka huku likitoa harufu mbaya na sauti ya kutisha, lakini lilishindwa kunipata usiku kucha nikawa nasikia kupumua kwake na harufu yake mbaya.
Kulipo pambazuka lile joka lilitoweka nami nikatoka mle nilimo jificha nikaanza kukizunguka kile kisiwa kufafuta njia nyengine yoyote ya kujisalimisha,
Nilipofika pwani mara niliona merkebu moja ikipita si mbali sana na pale kisiwani nilipokua, bila kuchelewa nilikata tawi la mti nikapiga makelele huku nikiwapungia lile tawi, bila shaka mabaharia waliniona mara ile ile merkebu ikageuza njia ikaelekea kule kisiwani, furaha ilioje hiyo niliyokuanayo.
Nilipookolewa, nahodha alinipa nguo safi za kuvaa kwani nilikua uchi wa mnyama, baada ya muda nilipata nguvu, na siku chache zilipopita nilirudiwa tena na nguvu zangu nikawa mzima kabisa. Basi nilimshukuru mwenyezi mungu kwa kunisalimisha na yale maafa yaliowapata wenzangu.
Basi tulisafiri baharini kwa muda wa siku nyingi mpaka mwisho tuliwasili kwenye kisiwa kiitwacho Salabitab. Hapo tulitia nanga na wafanya biashara walishuka na bidhaa zao.
Wakati nilipokua kwenye deki nikiwaangalia wenzangu jinsi walivyokua wakijishughulisha na bidhaa zao, nahodha wa merkebu yetu alinijia na kuniambia: "skiliza rafiki yangu, kwa kua umasikini usiekua na chochote na uliyekabili masaibu mengi baharini, nitakufanyia hisani.
Itaendelea...
Nadhani ameiruka!uaminifu wa hawa baharia unanikumbusha uaminifu wa vijana wakat utawala wa mwinyi,ilikuwa ukipiga pesa unatafuta wenzako mkatumie sio sasa hivi mtu akipiga hela anakimbia wenzake na kuenda kutumia pesa peke yake!
NB:nisaidieni sehem ya 12(ni post # ngapi)
Hata anayekileta hapa anafanya hisani,vinauzwa maduka ya vitabu,wachapishaji ni mkuki na nyota,ni vitabu vizuri sana.Vinapatikanaje na wapi? Je haiwezekani ukapata kwa soft copy?
Sehemu ya 12 vipiSEHEMU 13

😆😆😆😆😆😆😆😆😆Dada mwenyewe ukimsifia anakuchamba ukimkosoa napo anakuchamba zaidi tena na msumeno.
Hakukua na tamthilia za kideoniDah ninachowapendea hawa Mabaharia akina Sinbad walikuwa waaminifu sana hakuna kudhuliana. Halafu enzi hizo inaonekana watu walipenda kusimuliana na kusikiliza story