Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,672
- Thread starter
- #61
SEHEMU 11
Baada ya maakuli ya jioni, Sindbad Baharia akampa Hindbad Hamali Reale mia za dhahabu ambazo Hindbad Hamali alizipokea kwa shukran na dua nyingi; akatoka, akaelekea kwake huku akizidi kustaajabu kwa yale alioyasikia kutoka kwa Sindbad.
Siku ya tatu, Hindbad Hamali, baada ya swala ya adhuhuri alielekea tena kwa mkarimu wake aliempokea tena mikono miwili, akataka aketi karibu yake wageni wengine walipofika Sindbad Baharia alianza kuwasimulia yaliompata katika safari yake ya tatu.
SAFARI YAKE YA TATU
Mjue, sahibu zangu, alianza Sindbad Baharia, kwamba baada ya kurejea kwetu kutoka katika ile safari yangu ya pili, nikawa kama nilivyowasimulia, naishi katika maisha furaha, raha na starehe nyingi. Lakini baada ya muda nikachoshwa tena na yale maisha ya kukaa katika jiji LA Baghdad nikila na kulala tu bila kufanya kazi yoyote.
Basi kwa mara nyengine tena niliingiwa na hamu ya kusafiri kufanya biashara na kuuona ulimwengu.
Bila kujali yale yalionikuata awali, nilianza kujitayarisha tena kwa safari yangu ya tatu. Basi nikanunua bidhaa nyingi mbali mbali nikasafiri kwenye mto Tigris mpaka basrah ambako nilijiunga na wafanya biashara wengine. Tupanda merkeb kuelekea baharini.
Safari yetu ilianza vizuri kwani tulisafiri kwa upepeo mzuri bila matatizo yoyote, tukawasili katika bandari tofauti za kigeni, tukifanya biashara ya kununua na kuuza bidhaa zetu kwa faida kubwa bila tatizo lolote.
Siki kuja, walakin, wakati tulipokua tukisafiri katikati ya bahari kuu, mara dhoruba kali ikavuma na upepo wenye nguvu ulituchukua kutoka katika mkondo wetu, ukatupeleka mbali kusikojulikana.
Baada ya muda tukamsikia nadhodha wetu ambae alikua kwenye omo akiangalia upeo wa macho, akapiga mayowe! Alikua akijipiga ngumi za usoni na kifuani huku akinyofoa ndevu na kuzichana nguo zake.
"Tumeangamia" alikua akipiga makelele, "upepo umetuchukua mbali na kutuelekeza kwenye kile kisiwa kwenye upeo wa macho, hicho ni kisiwa kinachojulikana kwa kina la Zughb ambako wanaishi viumbe mbilikimo waliofanana zaid na amanyani kuliko wanadadu, ma ambako hakuna msafiri yeyote aliewahi kufika huko na akaokoka Salama!"
Upepo ulipotufikisha karibu na like kisiwa, mara vile viumbe alivyovitaja nahodha wetu vikajazana pwani, vikaanza kuogelea kutuelekea. Baada ya muda mfupi, kwa wingi wa nzige vikapanda merkebuni mwetu vilikua vifupi vyenye sura mbaya ya kutisha.
Na vyenye macho madogo yenye rangi ya manjano na mwili uliojaa manyoya. Vilika vingi kama utitiri! Hapo nahodha akatuhadharisha na kutuonya tusijaribu kuvishambulia wala kuviudhi, visije vikatuvamia na kutuangamiza!
Vilipojazana merkebuni mwetu vilipanda kwenye mlingoti, vikashusha tanga halafu vikashika usukani na kuiongoza merkebu yetu mpaka kisiwani ambako vilituteremsha mmoja mmoja, halafu vikarejea merkebuni vikatweka tanga vikatoweka na merkebu yetu.
Basi tukawa hatuna la kufanya ispokua kumshukuru mungu kwa kuokoka kwetu, pale kisiwani tukaanza kusaka kitu cha kula na Maji ya kunywa. Kwa bahati nzuri tuliona mito mingi na miti iliojaa matunda ya kutosha, hapo tukaoga tukapumzika tukila matunda tulioyachuma.
Tulipopumua tilianza kutembea tembea pale kisiwani mpaka katikati ya miti mikubwa, mbali na pale tulipokua tiliona jumba moja kubwa sana ambako tulitumaini kuupitisha Salama ule usiku.
Walakini, tulipokaribia tulistaajabu kuona ukubwa wa lango lake lililikua wazi. Bila kisita sita tukaingia ndani-lakini kwa hadhari kubwa - tukitumaini kukitana na watu, lakini tulistaajabu kuona hamna hata mtu mmoja.
Uwani kwenye pembe moja tukaona rundo la mifupa na kwa upande wa pili tukaona bao kubwa refu kupita kiasi. Karibu yake palikua na tanuri kubwa, masufuria, vikaangio vikubwa na nondo ndefu sana zenye ncha kali.
Kwa kua tulikua tumechoka kupita kiasi tukajibwaga pale ukumbini bila kujali tukalala kidogo. Kulipokuchwa mara tuliamshwa na kishindo kikubwa kama ngurumo, ardhi ilianza kutetemeka na ghafla lilelango lilianza kufunguka likaingia jitu kubwa, refu kama mnazi tena jeusi kama makaa, lenye jicho moja jeupe utosini! Domo lake kubwa la chini lilikua likining'inia mithili ya la ngamia, na maskio yake mapana yaliofika mabegani yalifanana na ya tembo, na kucha zake kali kama za simba zilijitokeza.
Kuliona tu, sote tukazimia kwa woga tukabaki pale kama wafu. Tulipopata fahamu tukalikodolea macho kwa khofu, wakati lenyewe likiranda randa huko na huko mle uani, mwisho lilikaa kwenye lile bao, likatuangalia kwa muda bila kutoa sauti yoyote, ghafla lilinyanyuka likaelekea kwangu, likanishika shingoni likaninyanyua juu likaanza kunikagua mwili mzima kwa kunitomasa tomasa na kunibonyeza bonyeza kwa dole lake kama mtu amkaguavyo kondoo atakae mchinja.
Lilipoona nimekonda kijiti na ni mifupa tu, lilinibwaga chini likaanza kuwakagua wenzangu mmoja mmoja mpaka likamfikia nahodha wetu ambae alikua mrefu tena mnene mwenye mabega mapana. Lile jitu likavutiwa naye likamshika kama mchinjaji amshikavyo kondoo atakae Mchinja,
Likamvunja shingo kwa guu lake; halafu likachukua moja ya zile nondo zilizokua na ncha kali likamchoma nalo kutoka nyuma hadi kinyani.
Itaendelea.