Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,672
SEHEMU KWANZA
Hapo kale katika enzi za Khalifa haarun al-rashid, paliishi wanaume wawili katika jiji la Baghdad. Mmoja aliitwa Sindbad baharia na wa pili aliitwa Hindbad hamali.
Hindbad mahali alikua mtu fukara alielisha mke na watoto wake kwa shida sana wakati Sindbad Baharia alikua mfanya biashara tajiri mkubwa asiejua hata wingi wa utajiri wake.
Yeye alikua mtu wa fahari aliejulikana na kuheshimiwa sana katika jiji la baghdad. Utajiri wake ulimuezesha kuwa na watumwa na vijakazi wengi katika kasri lake la fahari ambalo lilishinda hata la sultani,
Kwani kuta za kasri hilo zilinakshiwa kwa taswira nzuri nzuri za dhahabu na mawe ya tunu, na kila chumba kilinyunyiziwa kwa Maji ya marashi na kufukizwa kwa udi na ambari.
Hali kadhalika, kila chumba kilipambwa kwa maua ya nargis, waridi na yasmini yanukiayo yaliochumwa katika bustani take, katika kasri hilo siku zote vijakazi wazurizuri waliwatumikia na kuwatumbuiza wageni kwa sauti zao nzuri zilizofuatana na zana mbali mbali za muziki walizozipiga kwa ufundi mkubwa. Zana kama udi na zumari.
Huko jikoni nako siku zote kulitoka harufu nzuri ya maakuli mbalimbali yaliopikwa na yaliomtoa mtu mate kinywani.
Siku moja, wakati Hindbad mahali alipokua akiubeba kwa shida mzigo mzito uliomwelemea katika jua Kali la kiangazi lililowaka kupita kiasi, Hindbad mahali alifika kwenye kasri hilo la Sindbad Baharia ambako, kwa uchovu mwingi aliutua mzigo wake mzito ili apumue, apumzike kidogo.
Alipoutua na kufuta jasho lililomtiririka mwili mzima, Hindbad mahali alianza kupepewa na upepo mwanana uliomletea zile harufu nzuri za kunukia zilizotoka katika lile kasri huku akisikia sauti za furaha, muziki na nyimbo za kuburudisha roho.
Hapo Hindbad mahali akanyanyua macho yake juu, akatamka kwa kukata tamaa: "ah, yaa Rabby, muumba wa viumbe vyote, tofauti kubwa ilioje hii baina ya maisha yangu na maisha aishio mwenye kasri hili! Wakati Mimi nahangaika kutwa kucha kutafuta rizki kidogo ya kilisha kwa shida familia yangu, mwenye kasri hili anaishi katika maisha ya anasa na kifahari!
Nimekosa nini, yaa tabby, hata nikastahili maisha haya niishiyo?"
Baada ya kutamka maneno hayo ya kukata tamaa, Hindbad mahali akainamisha kichwa chake chini kwa huzuni. Baada ya muda mfupi, alitokea mjakazi kutoka mle ndani akamshika mkono Hindbad mahali, akamwambia:
"Bwana wangu mwenye kasri hili ameniagiza; anataka kusema nawe." Hindbad mahali kuskia maneno Yale, alisita kidogo lakini akaona hana sababu yoyote ya kutomfuata yule mjakazi; kwani kakosa nini? Hapo akanyanyuka, akanyanyua ule mzigo wake akauweka barazani palipokua na bawabu,
Akamfuata ndani yule mjakazi wa kike mpaka wailipofika katika chumba kikubwa. Humo Hindbad mahali akaona kila upande wa kile chumba kumepambwa kwa mabusati mazuri nadhifu na katikati pana chemchemi ya maji yarukayo juu na kushuka chini kutoka katika mdomo wa ndege aliesimama kwenye dimbwi la marumaru.
Chumba kizima kilijaa masheikh, madiwani na waungwana maarufu wa jiji la baghdad. Katikati yao alikaa mwenye kasri.
Hindbad mahali alipoingia aliwaamkia kwa kuwapigia magoti kwa heshima akaibusu sakafu akifikiri,
"bila shaka hiyo pepo isemwayo ni kama hii hapa nilipo mimi"
Baada ya kunyanyuka, akasimama wima kama mlingoti.
Ndipo Sindbad Baharia akamkariibisha kwa ukarimu akimwambia akae karibu take. Alipokaa, Sindbad Baharia akamuuliza jina lake.
ITAENDELEA KESHO MUNGU AKIPENDA