Kisa cha Sindbad baharia na safari saba

Kisa cha Sindbad baharia na safari saba

Moja ya hadithi zinazopatikana katika kitabu cha alfu lela u lela (siku elfu moja na moja). Vitabu vipo tisa,kisa hiki kinapatikana katika kitabu cha pili.
Wale wapenzi wa vitabu mnaweza mkajitafutia mkasome visa kwa urefu na kwa nafasi.
Vinapatikanaje na wapi? Je haiwezekani ukapata kwa soft copy?
 
KISA CHA SINDBAD BAHARIA
SEHEMU 12
Na baada ya kuwasha moto mkubwa kwenye lile tanuri, kwa taratibu lilianza kumchoma nahodha wetu mithili ya mtu achomavyo mishkaki.
Lilipohakikisha kuwa ameiva vizuri lilimpasua vipande vipande kwa makucha yake marefu, likaanza kumla huku likitupa mifupa pembeni kwenye ukuta, baada ya kushiba lilijinyoosha pale baoni likalala na kukoroma kama radi huku sisi usiku kucha tukijikunyata na kutetemeka kwa hofu pale pembeni.
Klipokucha lile jitu lilinyanyuka likatoka mle jumbani likatoweka likatuacha tukitetemeka kwa hofu, tulipohakikisha limetoweka, tulianza kuomboleza kwa yale masaibu yaliotufika.
"Bora tungekufa baharini au tungeuwawa na vile viumbe mbilikimo," tulilia,
"Kuliko kile kifo kilichompata nahodha wetu na ambacho bila shaka kinatusubiri site!"
Liandikwalo ndilo liwalo, basi tukatoka mle jumbani kutafuta pa kujificha, lakini pale kisiwani hatukuweza kupata mahali pengine popote pa kujificha.
Jioni tukawa hatuna budi kurudi mle jumbani kujiepusha na majoka na viumbe vingine vya kutisha vilivyotapakaa pale kisiwani, kulipokuchwa tena lile jitu likarudi likamnyakua mfanyabiashara mmoja likamtayarisha kama alivyomtayarish
a nahodha wetu, baada ya kushiba na kujinyoosha tena pale kwenye lile bao, lililala na kukoroma tena.
Asubuhi ya pili lilipotokomea nje tulianza kujadiliana, "wallah" aliapa mmoja wetu "ni bora kujitosa baharini kuliko kubaki humu kuchomwa na kuliwa kama mishkaki." Akatamka mwengine "sikilizeni jamani, tuliuwe hili dubwasha; kwani ni kwa kuliangamiza tu ndio tutakapoweza kuumaliza uovu wake na kuyaokoa maisha yetu, na ya waislamu wengine watakaofika hapa."
Pendekezo hili liliungwa mkono na wote, hapo na mm nilinyanyuka nikaongeza "kama tumeafikiana kuliuwa kwanza tutengeneze vyelezo vitakavyo tuwezesha kuokoka kutoka katika kisiwa hiki mara tu tutakapo liuwa. Labda vyombo hivyo vitatufikisha kisiwa kingine ambako labda tutaweza kupata merkeb itakayo tufikisha kwetu.
Tukifa Maji si kitu ni bora kuliko kufa kifo kile cha kuchomwa kama mishkaki
Itaendelea...

SEHEMU 13
Basi bila kuchelewa tukaanza kazi ya kukusanya magogo kutoka katika rundo la magogo yaliorundikwa na lile jitu karibu na lile tanuri lake, tukayabeba nje tukayafunga pamoja imara. Tulipovitayarisha vyelezo yetu tukaviacha ufukweni.
Jioni km kawaida ardhi ikatetemeka kwa kishindo cha kuja kwa lile jitu huku likilia kama jibwa. Kuingia tu, lilimnyakua mmoja wetu aliekua mnene kuliko sote, likamtayarisha kwa mlo wake wa jioni lilipokula na kushiba, lilijinyoosha baoni na kama kawaida yake lililala usingizi mzito.
Hapo tukanyata kwa hadhari kubwa tukachukua nondo yenye ncha moja kali tukaitia motoni, iliposhika moto sana tukaibeba pamoja mpaka pale lile jitu lilipokuwa likikoroma kwa nguvu moja, tulilichoma nalo kwenye lile jicho lake moja huku sote tukiisukuma ile nondo kwa nguvu zetu zote.
Lo masalale! Lile jitu likaruka toka pale baoni likapaza sauti ya kutisha likajaribu kututafuka kwa kupapasa huku na huko kwa majikono yake makubwa marefu, lakini sisi tuliweza kulikwepa, liliposhindwa kutukamata lilipapasa ukuta mpaka likafika kwenye lile lango likafungua na kutoka nje huku likipiga makelele kwa maumivu.
Haraka tukatoka mle tukaelekea ufukweni tukaviburuza vile vyelezo vyetu mpaka majini, tukapanda tukaanza kipiga makafi, kabla hatujafika mbali mara tukaliona lile jitu tulilolipofoa likiongozwa na kundi kubwa la wenzake.
Yalipofika ufukweni yalisimama huku yakitupigia makelele mara yakanyanyua mapande makubwa ya mawe pale ufukweni yakaingia majini, yakatuvurumishia nayo moja baada ya jengine, kwa kuwa yalikua na shabaha yakavizamisha vyelezo yote ispokua kile nilichokuwemo Mimi na wenzangu wawili, kwa bahati nzuri sisi tuliweza kupiga makafi kwa nguvu na kufika mbali baharini ambako Yale majitu hayakuweza kutufikia.
Basi mchana kutwa na usiku kucha tukawa tunaelea baharini tukichukuliwa na mawimbi mpaka yakatufikisha kwenye ufukwe wa kisiwa kingine, kwa kuwa tulikua tumechoka sana na kwa ajili ya njaa na kiu tuliokua nayo tulijibwaga pale pwani mchangani tukalala.
Asubuhi ya pili tilipoamka tukashtuka kuona joka kubwa ajabu limejikunja mbele yetu! La haulaa! Kabla hatujaweza kufanya lolote lilinyanyua kichwa likafunua kinywa likamnyakua mmoja wa wale wenzangu, likammeza mzima mzima huku tikisikia jinsi mbavu za mwenzetu zikivunjika tumboni mwa lile joka kwa kujibana kwake.
Halafu lilijinyoosha na bila kutijali lilitiririka mchangani likatoweka msituni, "mungu we!" Tukapiga mayowe, "tuliokoka kifo kibaya cha kuchomwa kama mshkaki na sasa tunakikabili kifo kibaya zaidi cha kuliwa tungali hai! Yaa rabby! Tutaliokoka vipi hili joka?!"
Asubuhi ya pili jua lilipochomoza, sisi wawili tuliobaki tulipata nguvu kidogo tukawa tunatafuta chakula na maji ya kunywa, na kabla hakuja kuchwa tulitafuta mti mrefu tukaupanda, tukakalia tawi la juu kabisa kujisalimisha na lile joka.
Giza lilipoingia tulisikia kupumua kwa lile joka, lilipofika pale mtini tulipokua, lilitambaa juu lilimnyakua mwenzangu aliekua chini yangu likammeza likimbana na kumvunja mbavu tomboni mwake kama mwenzetu. Baada ya kufanya hivyo likatambaa chini likatoweka msituni, kusema kweli usiku kucha sikupata usingizi kwa woga na wasi wasi niliokua nao.
Asubuhi nikashuka mtini, fikra yangu ya kwanza ikawa ni kukitosa baharini na kufa Maji ili kuyamaliza maisha yangu ambayo yalikua yameshapambana na maafa mengi. Lakini nikashindwa kufanya hivyo kwani kujitoa roho si mchezo na maisha ni matamu japokua ni mafupi.
Hapo nilifanya mpango wa kujihami dhidi ya lile joka. Basi nilikusanya mabiwi na magogo na majiti makubwa mazito yenye miba, nikayafunga vizuri pamoja kama sanduku, jioni nilijitia mle ndani nikajifungia vizuri, baada muda lile joka likaja likanizunguka huku likitoa harufu mbaya na sauti ya kutisha, lakini lilishindwa kunipata usiku kucha nikawa nasikia kupumua kwake na harufu yake mbaya.
Kulipo pambazuka lile joka lilitoweka nami nikatoka mle nilimo jificha nikaanza kukizunguka kile kisiwa kufafuta njia nyengine yoyote ya kujisalimisha,
Nilipofika pwani mara niliona merkebu moja ikipita si mbali sana na pale kisiwani nilipokua, bila kuchelewa nilikata tawi la mti nikapiga makelele huku nikiwapungia lile tawi, bila shaka mabaharia waliniona mara ile ile merkebu ikageuza njia ikaelekea kule kisiwani, furaha ilioje hiyo niliyokuanayo.
Nilipookolewa, nahodha alinipa nguo safi za kuvaa kwani nilikua uchi wa mnyama, baada ya muda nilipata nguvu, na siku chache zilipopita nilirudiwa tena na nguvu zangu nikawa mzima kabisa. Basi nilimshukuru mwenyezi mungu kwa kunisalimisha na yale maafa yaliowapata wenzangu.
Basi tulisafiri baharini kwa muda wa siku nyingi mpaka mwisho tuliwasili kwenye kisiwa kiitwacho Salabitab. Hapo tulitia nanga na wafanya biashara walishuka na bidhaa zao.
Wakati nilipokua kwenye deki nikiwaangalia wenzangu jinsi walivyokua wakijishughulisha na bidhaa zao, nahodha wa merkebu yetu alinijia na kuniambia: "skiliza rafiki yangu, kwa kua umasikini usiekua na chochote na uliyekabili masaibu mengi baharini, nitakufanyia hisani.
Itaendelea...
 
SEHEMU 14
"Miaka michache iliyopita katika merkebu yangu hii hii mlikia na mfanya biashara mmoja ambae kwa bahati mbaya tulimuacha kwenye kisiwa kimoja kisichokua na watu, toka siku hiyo hakuna yeyote aliewahi kusikia habari zake na hakuna hata mmoja anaejua kama alikufa ama yu hai, kwa kuwa nakuamini chukua bidhaa zake ukazifanyie biashara faida utakayopata uchukue nusu na nusu ya pili nitawapelekea jamaa zake huko Baghdad."
Baada ya kumshukuru sana, yule nahodha akatoa amri zile bidhaa ziteremshwe ziandikwe katika daftari la merkebu, karani aliepewa ile kazi aliuliza; "je hizi ni bidhaa za nani?" " Jina la mwenye bidhaa hizi lilikua Sindbad Baharia" alijibu nahodha
Niliposikia hivyo nilipaza sauti ya furaha na mastaajabu makubwa! Mara ile ile nilimtambua yule nahodha kama ni yule nahodha wa ile merkebu niliosafiria katika safari yangu ya pili.
"Mimi ndie Sindbad; yule mfanya biashara ambae miaka michache iliopita mlimuacha kwenye kisiwa cha madege ROK," nilimwambia "nilishikwa na usingizi karibu na chemchemi ya Maji nikalala, nilipoamka niliona merkebu imeshatoweka!"
Kwa bahati nzuri kwenye ile merkebu kulikua na mfanya biashara alieniona wakati nilipookoka kutoka katika lile bonde la almasi, yeye alijitokeza mbele akaniangalia kwa makini akanitambua kisha akasema, "wallahi hamuwezi kukisia jinsi bwana Huyu alivyookoka kutoka katika lile bonde la almasi! Mimi nathibitisha kabisa kuwa Huyu ndiye Sindbad Baharia; ni mtu yule yule alienipatia almasi."
Basi baada ya nahodha kunihoji kuhusu yaliyomo ndani ya mizigo yangu na mimi kumweleza yote, na baada ya kumweleza mambo muhimu yaliyotokea katika ile safari yetu, nahodha akanitambua na kunikumbatia akanipongeza, akisema "tumshukuru mwenyezi mungu kwa kutukutanisha tena."
Basi robota za bidhaa zangu zikashushwa, nikaziuza kwa bei nzuri na kupata faida kubwa sana baada ya muda tukang'oa nanga tukasafiri mpaka tukafika Sind ambako tulifanya biashara zaid.
Wakati tulipokua tukisafiri katika bahari ya hindi, nilishuhudia maajabu mengi kwa mfano baharini niliona mnyama aliefanana na ng'ombe lakini mwenye kichwa kama punda; na niliona ndege atagae mayai yake kwenye kombe na kuyatamia baharini mpaka yakangulika!
Basi baada ya kufanya biashara kwa muda tukang'oa nanga Sind tukaelekea Basrah ambako nilikaa kwa muda wa siku chache kabla sijaelekea kwetu Baghdad kupitia mto wa Tigris.
Nilipofika kwangu nilipokelewa mikono miwili na ndugu jamaa na marafiki zangu, ambao wote niliwatunukia zawadi nzuri nzuri, nilitoa misaada kwa maskini na mayatima kwani nilirejea na utajiri mkubwa kuliko ule wa safari zangu mbili.
******************************
Sindbad Baharia alipomaliza kusimulia yaliyompata katika safari yake ya tatu alimpa Hindbad Hamali mfuko wa Reale za dhahabu. Akamwambia "in sha Allah kesho nitawasimulia tena Yale yaliyonipata katika safari yangu ya nne"
Basi baada ya maakuli ya jioni, Hindbad Hamali na wale wageni wengine wakaaga wakaenda zao makwao wakitumaini kurudi tena kesho kuja kuskiliza kisa kingine cha ajabu kilimpata mwenyeji wao Sindbad Baharia.
SAFARI YA 4 YA SINDBAD
Mwanadamu haridhiki! Yale maisha ya raha na starehe niliokua nikiishi, baada ya safari yangu ya tatu hayakunisahaulisha furaha na faida ya kusafiri na kufika ughaibuni. Shauku yangu ya kuuona ulimwengu licha ya hatari nilizokabili ikanizidi nguvu ikanishawishi nisafiri tena baharini.
Basi baada ya kujitayarisha kwa safari ndefu nilijiunga na wafanya biashara, tulipanda merkebu kutoka basrah, tukang'oa nanga tukaelekea bahari kuu, tukawa tunafanya biashara kutoka kisiwa kimoja hadi kingine, na kutoka bahari moja hadi nyengine. Siku moja walakin, upepo mkali sana ukavuma kwa nguvu ukapandisha juu mawimbi makubwa kama mlima na kuangukia merkebuni metu na kuifanya ionekane kama kijiti kibebwacho juu ya bahari na kuteremshwa kasi bondeni.
Nahodha kuona vile akawaamrisha mabaharia kutosa nanga baharini sote tulianza kupiga magoti na kumuomba mungu huku tukiomboleza kwa ile hatari yiliokua tukiikabili. Ghafla tanga likakwanyuka kwanyuka likawa mithili ya kamba zivumazo upeponi kama bendera, na mlingoti ulikatika vipande viwili, kimoja kikatumbukia baharini.
Mara wimbi kubwa likatukumba kutoka juu likaiponda merkebu yetu na lilitutawanya sote baharini. Walakin kwa msaada wa mwenyezi mungu nikabahatika kama wenzangu wengine kushika sehemu ya ule mlingoti uliotumbukia baharini, niliung'ang'ania kwa nguvu zangu zote kama wenzangu huku tukipigwa na Yale mawimbi makubwa.
Ikawa tunapiga piga miguu kama makafi huku tukisukumwa na mawimbi na upepo mkali uliokua ukivuma mpaka usiku wa manane tukatupwa kwenye kisiwa kimoja tukiwa hoi kwa uchovu, kui na njaa tulivyokua navyo.
Tukalala pale ufukweni, tulipoamka siku ya pili tulianza kuzunguka zungika pale kisiwani na baada muda tulitokea kwenye jumba moja kubwa lililokua katikati ya miti, tulipolikaribia mara mlango ukafunguliwa wakatokea watu uchi wa mnyama waliokua na nyuso za kutisha, bila salamu walituvamia na kutuongoza mle jumbani moja kwa moja mpaka kwa mfalme wao alieketi kwenye kiti chake cha enzi.
Itaendelea...
 
uaminifu wa hawa baharia unanikumbusha uaminifu wa vijana wakat utawala wa mwinyi,ilikuwa ukipiga pesa unatafuta wenzako mkatumie sio sasa hivi mtu akipiga hela anakimbia wenzake na kuenda kutumia pesa peke yake!

NB:nisaidieni sehem ya 12(ni post # ngapi)

Kinondoni Sweetheart kairuka hiyo, au kaipest kwingine.
 
SEHEMU 13
Basi bila kuchelewa tukaanza kazi ya kukusanya magogo kutoka katika rundo la magogo yaliorundikwa na lile jitu karibu na lile tanuri lake, tukayabeba nje tukayafunga pamoja imara. Tulipovitayarisha vyelezo yetu tukaviacha ufukweni.
Jioni km kawaida ardhi ikatetemeka kwa kishindo cha kuja kwa lile jitu huku likilia kama jibwa. Kuingia tu, lilimnyakua mmoja wetu aliekua mnene kuliko sote, likamtayarisha kwa mlo wake wa jioni lilipokula na kushiba, lilijinyoosha baoni na kama kawaida yake lililala usingizi mzito.
Hapo tukanyata kwa hadhari kubwa tukachukua nondo yenye ncha moja kali tukaitia motoni, iliposhika moto sana tukaibeba pamoja mpaka pale lile jitu lilipokuwa likikoroma kwa nguvu moja, tulilichoma nalo kwenye lile jicho lake moja huku sote tukiisukuma ile nondo kwa nguvu zetu zote.
Lo masalale! Lile jitu likaruka toka pale baoni likapaza sauti ya kutisha likajaribu kututafuka kwa kupapasa huku na huko kwa majikono yake makubwa marefu, lakini sisi tuliweza kulikwepa, liliposhindwa kutukamata lilipapasa ukuta mpaka likafika kwenye lile lango likafungua na kutoka nje huku likipiga makelele kwa maumivu.
Haraka tukatoka mle tukaelekea ufukweni tukaviburuza vile vyelezo vyetu mpaka majini, tukapanda tukaanza kipiga makafi, kabla hatujafika mbali mara tukaliona lile jitu tulilolipofoa likiongozwa na kundi kubwa la wenzake.
Yalipofika ufukweni yalisimama huku yakitupigia makelele mara yakanyanyua mapande makubwa ya mawe pale ufukweni yakaingia majini, yakatuvurumishia nayo moja baada ya jengine, kwa kuwa yalikua na shabaha yakavizamisha vyelezo yote ispokua kile nilichokuwemo Mimi na wenzangu wawili, kwa bahati nzuri sisi tuliweza kupiga makafi kwa nguvu na kufika mbali baharini ambako Yale majitu hayakuweza kutufikia.
Basi mchana kutwa na usiku kucha tukawa tunaelea baharini tukichukuliwa na mawimbi mpaka yakatufikisha kwenye ufukwe wa kisiwa kingine, kwa kuwa tulikua tumechoka sana na kwa ajili ya njaa na kiu tuliokua nayo tulijibwaga pale pwani mchangani tukalala.
Asubuhi ya pili tilipoamka tukashtuka kuona joka kubwa ajabu limejikunja mbele yetu! La haulaa! Kabla hatujaweza kufanya lolote lilinyanyua kichwa likafunua kinywa likamnyakua mmoja wa wale wenzangu, likammeza mzima mzima huku tikisikia jinsi mbavu za mwenzetu zikivunjika tumboni mwa lile joka kwa kujibana kwake.
Halafu lilijinyoosha na bila kutijali lilitiririka mchangani likatoweka msituni, "mungu we!" Tukapiga mayowe, "tuliokoka kifo kibaya cha kuchomwa kama mshkaki na sasa tunakikabili kifo kibaya zaidi cha kuliwa tungali hai! Yaa rabby! Tutaliokoka vipi hili joka?!"
Asubuhi ya pili jua lilipochomoza, sisi wawili tuliobaki tulipata nguvu kidogo tukawa tunatafuta chakula na maji ya kunywa, na kabla hakuja kuchwa tulitafuta mti mrefu tukaupanda, tukakalia tawi la juu kabisa kujisalimisha na lile joka.
Giza lilipoingia tulisikia kupumua kwa lile joka, lilipofika pale mtini tulipokua, lilitambaa juu lilimnyakua mwenzangu aliekua chini yangu likammeza likimbana na kumvunja mbavu tomboni mwake kama mwenzetu. Baada ya kufanya hivyo likatambaa chini likatoweka msituni, kusema kweli usiku kucha sikupata usingizi kwa woga na wasi wasi niliokua nao.
Asubuhi nikashuka mtini, fikra yangu ya kwanza ikawa ni kukitosa baharini na kufa Maji ili kuyamaliza maisha yangu ambayo yalikua yameshapambana na maafa mengi. Lakini nikashindwa kufanya hivyo kwani kujitoa roho si mchezo na maisha ni matamu japokua ni mafupi.
Hapo nilifanya mpango wa kujihami dhidi ya lile joka. Basi nilikusanya mabiwi na magogo na majiti makubwa mazito yenye miba, nikayafunga vizuri pamoja kama sanduku, jioni nilijitia mle ndani nikajifungia vizuri, baada muda lile joka likaja likanizunguka huku likitoa harufu mbaya na sauti ya kutisha, lakini lilishindwa kunipata usiku kucha nikawa nasikia kupumua kwake na harufu yake mbaya.
Kulipo pambazuka lile joka lilitoweka nami nikatoka mle nilimo jificha nikaanza kukizunguka kile kisiwa kufafuta njia nyengine yoyote ya kujisalimisha,
Nilipofika pwani mara niliona merkebu moja ikipita si mbali sana na pale kisiwani nilipokua, bila kuchelewa nilikata tawi la mti nikapiga makelele huku nikiwapungia lile tawi, bila shaka mabaharia waliniona mara ile ile merkebu ikageuza njia ikaelekea kule kisiwani, furaha ilioje hiyo niliyokuanayo.
Nilipookolewa, nahodha alinipa nguo safi za kuvaa kwani nilikua uchi wa mnyama, baada ya muda nilipata nguvu, na siku chache zilipopita nilirudiwa tena na nguvu zangu nikawa mzima kabisa. Basi nilimshukuru mwenyezi mungu kwa kunisalimisha na yale maafa yaliowapata wenzangu.
Basi tulisafiri baharini kwa muda wa siku nyingi mpaka mwisho tuliwasili kwenye kisiwa kiitwacho Salabitab. Hapo tulitia nanga na wafanya biashara walishuka na bidhaa zao.
Wakati nilipokua kwenye deki nikiwaangalia wenzangu jinsi walivyokua wakijishughulisha na bidhaa zao, nahodha wa merkebu yetu alinijia na kuniambia: "skiliza rafiki yangu, kwa kua umasikini usiekua na chochote na uliyekabili masaibu mengi baharini, nitakufanyia hisani.
Itaendelea...
#12 mzee umechemka mbona hujaiweka
 
Let story tu! Nmeipennda sana

Mabaharia wanakuwaga na sifa ya kuwaamberuth watu.mbona uku wanasimulia mazuri tu au ilikuwaga bado mduara haujaanza?nawasilisha tu ndugu mwandishi
 
Back
Top Bottom