Kisa cha kweli: Jinsi nilivyosengenywa na "kubaguliwa" na Watanzania wenzangu nchi ya ugenini

Nakumbuka jamaa yangu alikuwa SWEDEN na rafiki yake! Wakawa ndani ya street train mara wakamkamuona mama mnene sana. Si wakaropoka kuwa mimama kama hii ikijamba inatoa ushuzi unaonuka ajabu, wakacheka. Yule mama alipofika kituo alichokuwa anashuka akawaeleza ‘do you know the meaning of kumamayo’ akasepa. Jamaa walijisikia wapuuzi sana! Ni kuwa usimseme mtu ambaye humjui anaweza kuwa anakuthale tu anasubiri kithibiti
Hahahahahaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahha... umenikumbusha mbali sana mkuu, 2014 nipo zangu ontario canada na wanangu kama wawili hivi mtaani tunazurura huku tunatafuta mambo ya clubs na sehemu za kupiga vyombo hapo tuna kama wiki mbili hivi (mambo ya chuo chuo) sasa tunajifanya hatutaki kuuliza yaan tukomae tuu kusoma mabango mpk tupate hizo sehem..
Mwisho wa siku tukachoka mwana mmoja akasema tuache ufala hebu tuulizeni nyie na kwa urahis zaidi tuwaulize wazee manake ndo wanaonekana kama hawana noma, mara tukamuona mtu wa makamo kiasi kama 50s hivi anashona viatu kny kona hivi tukamwendea....
Tukamsalimia vizuri kwa kizungu naye akatujibu fresh tu, tukampa shida yetu kwamba tunataka kufaham sehem zenye migahawa na mahoteli ya watu wa kati na chini hasa clubs za mziki, yey akatuuliza "hamna ramani maana wageni wote ugenini hutumia raman au gugo map" tukamwambia "sisi ni wageni sana hata hii mitaa hatutaijua vizuri tukiisoma kwenye ramani" yey akasema basi na mimi siwezi kuwaelekeza kama hamjui hata mitaa tukajiona wajinga kweli, sasa mimi huwa mkimya hivi sio muongeaji ko hapo sikuchangia chochote katika hayo mazungumzo yote isipokua alivokataa huyu mzungu kutuelekeza nikajikuta naropoka kwa kiswahili "..daah hawa wazungu wasenge kweli .." mudy akadakia "...hasa ukiwajia huku kwao.." hamaadi yule mbabu akajibu banaaa🤣🤣 akasema "... wasenge wenyewe mnaotembea miji ya watu bila ramani tena wajinga sana..." tulistuck kama dakika mzima hivi tunashangaaana tuu kuja kugutuka hivi ikabidi tuondoke kwa aibu bila kuaga huko mbele tukacheka balaa
Yule babu ni mzungu pure huwezi imagine hata kama kawahi kufika Afrika! Tuwe makini sana jamani ugenini hasa kwa wenyeji manake yule mzee alitutafuta ili kutushtaki ila msala uliisha alikua mtu wa dini kumbe na aliwahi kuja kuishi huku kwetu vinginevyo moto ungewaka!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Miaka ile British Airways inakuja Dsm,una muda katika mwaka walikuwa na msimu wa bei cheee sana kuvutia wateja.Nikaamua kusomba vijana wangu kwenda kutembea.

Nimepanda hapo Dar es Salaam,basi tupo juu huko,wife akawa ameomba Air hostess amletee juice ya Apple,yule dada akusikia vizuri akaleta juice ya chungwa.Wife akapiga fundo moja...Then akaropoka!Hawa nao unamuagiza hiki analeta hiki...Utafikiri hatulipii!Yule mzungu akajibu kwa Kiswahili safi kabisa,samahani dada,nitakuwa nilipitiwe ulitaka juice ya nini?Wewe mteja ni mfalme...

Loooh...Mwanamke wa Kingazinja sura ikamshuka kama paka shume...nikamwambia ndio uache kuropoka hovyo.Wakati wa kushuka yule dada akawa mlangoni,tumefika akasema mnisamehe kwa huduma isiyoridhisha,siku nyingine ntakuwa makini...
 
Nakumbuka jamaa yangu alikuwa SWEDEN na rafiki yake! Wakawa ndani ya street train mara wakamkamuona mama mnene sana. Si wakaropoka kuwa mimama kama hii ikijamba inatoa ushuzi unaonuka ajabu, wakacheka. Yule mama alipofika kituo alichokuwa anashuka akawaeleza ‘do you know the meaning of kumamayo’ akasepa. Jamaa walijisikia wapuuzi sana! Ni kuwa usimseme mtu ambaye humjui anaweza kuwa anakuthale tu anasubiri kithibiti
HahahHahaha nimecheka kama chizi
 
Miaka ile British Airways inakuja Dsm,una muda katika mwaka walikuwa na msimu wa bei cheee sana kuvutia wateja.Nikaamua kusomba vijana wangu kwenda kutembea.

Nimepanda hapo Dar es Salaam,basi tupo juu huko,wife akawa ameomba Air hostess amletee juice ya Apple,yule dada akusikia vizuri akaleta juice ya chungwa.Wife akapiga fundo moja...Then akaropoka!Hawa nao unamuagiza hiki analeta hiki...Utafikiri hatulipii!Yule mzungu akajibu kwa Kiswahili safi kabisa,samahani dada,nitakuwa nilipitiwe ulitaka juice ya nini?Wewe mteja ni mfalme...

Loooh...Mwanamke wa Kingazinja sura ikamshuka kama paka shume...nikamwambia ndio uache kuropoka hovyo.Wakati wa kushuka yule dada akawa mlangoni,tumefika akasema mnisamehe kwa huduma isiyoridhisha,siku nyingine ntakuwa makini...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu na hongera kwa kuwa na kifua!!

Me nisibgevumilia mpaka mwisho yan pale pale ningewapa mitusi na kuwajazia nzi, sipendag dharau za kiboya....na kwene vitu nisingewapeleka, dawa ya moto ni moto....mtoa mada mvumilivu sana aisee

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom