Kisa cha kweli: Jinsi nilivyosengenywa na "kubaguliwa" na Watanzania wenzangu nchi ya ugenini

Hii imeshawahi kunikuta sikumoja tupo na shogaangu kituo cha dalala tunasubiria daladala ije tupande tumesubiri sana kama lisaa limoja hamna gari pembeni yetu yupo mzee mmoja amebeba mkoba wake umechakachakaa tukaanza kumsema kipare mimi na huyo shogaangu tukamsema sana mara daladala ikaja tunashangaa yule mzee anatuambia kwa kipare twendeni watoto wangu ..aiseee tuliona aibu hata kupanda ile gari tulishindwa mzee akapanda

Sent using Jamii Forums mobile app
😀😀😀😀mheiwe.
 
Hiyo tabia tunayo sana waswahili tukiona mtu huelewi kiswaz,siku moja tumetoka ubalozini tushapiga vyombo vya bure mara ndani ya metro na wazungu wamekaa ikatokea harufu kali ya ushuzi nahisi mmoja wetu pale alijamba,ushuzi wa maharage kabisa.
Basi bana tunaanza "mmh mmmmh,duh e bana kuna jamaa kaachia ushuzi"
Mwingine anajibu si huyo nguruwe hapo"mzungu"
Kadakia mwingine "sijui kala nini kumabake"
Mwingine "aah mayai visa hayo du e bana unanuka kishenzi"
Basi bana tunaendelea kumteta kumbe jamaa anajua kiswahili fasta akatujibu.
Mzungu"mmh SIJAJAMBA jamani usinisingizie sio mimi"
Dah ile noma tulishuka kituo kinachofata kwa aibu tunasubiri treni ingine 30 min bila kupenda.
mwisho mkaanza kunusana nyie wenyewe haaa haa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hii umenikumbusha mbali saaana.

Mimi haikuwa kwa mweusi mwenzangu bali ilikuwa ni kwa wazungu. Tulikuwa ufukweni tunapunga upepo na tulikuwa watanzania watatu na wakenya wawili. Kati yetu wanamme tulikuwa watatu na wanawake wawili. Lakini hatukuwa na mahusiano ya kimapenzi kati yetu wote.

Walikuja mwanamme na mwanamke na watoto wawili nao wakakaa jirani na sisi. Tuligundua kuwa huyo mke na mme ni mtu na mmewe kutokana na maongezi. Kiss kwa wingi. Lakini mme alikuwa ni kijana mdogo nae mke umri ilikuwa umeende.

Kama kawaida wamama tuliyokuwa nao wakaanza kuwakogoa wanandoa hao kuwa mme kamuoa dada yake. Wanamme ikawa tunasema kuwa ni kawaida kwa wazungu lkn kina mama waliendelea kuwasemea mbovu za kutosha. Kilichowaudhi ni pale mwanamama wa kizungu aliposimama mimi nikasema "kweli huyu mama kazeeka hadi matako yake yamepolomoka"

Kauli hiyo iliwaudhi kumbe wanaelewa kiswahili vizuri sana wote mke na mme. Walitutolea mbovu tukawa kimya kama tumemwagiwa maji ya baridi. Huku wakisema "tena wote hawa ni watanzania wenzetu"

Tuliwaomba msamaha na kwa kweli walitusamehe kumbe wote wamezaliwa na kukulia palokia moja huko makete iringa. Tulijiona choo sana nchi ya watu.
Leo nimekumbuka hiki kisa, nikaona weekend hii ni-share na Wanajamvi wenzangu,sijajua kama hapa ni jukwaa sahihi au la!

Miaka mingi iliyopita nilikuwa nchi za watu kimasomo, wakati huo nikiwa bado kijana mdogo. Nilipata nafasi hiyo kwa sababu ya kufahamiana na mwalimu mmoja aliyekuja Tanzania kufundisha kwa kujitolea. Alinipenda sana na akahaidi kunitafutia scholarship ili nikasome huko.

Kweli baada ya yeye kurudi kwao,tuliendelea kuwasiliana kwa njia ya barua,maana simu zilikuwa shida sana kwa wakati ule. Hatimaye siku zilienda na nilibahatika kwenda kusoma.

Maisha ya ugenini yalikuwa magumu sana,upweke,utamaduni tofauti na vyakula viliniathiri.Ni wakati ambao tulikuwa tunaondokana na mambo ya ujamaa na kuingia kwenye sera za soko huria.Hivyo ulikuwa ni wakati ambao Watanzania wengi pia walitoka nje ya nchi kuchukua mizigo kwa ajili ya biashara.

Katika likizo za majira ya joto na majira ya baridi mimi sikurudi nyumbani,nilibaki kufanya kazi katika mashamba ya kuvuna matunda na wakati mwingine katika migahawa ya wageni (Foreign Restaurants) ,hii ni migahawa ambayo ilikuwa inauza vyakula vya kigeni tofauti na vyakula vya nchi niliyokuwepo. Na kulikuwa na mtaa kabisa wa migahawa ambayo wanauza vyakula vya kigeni.

Kwa hiyo wateja wake wengi walikuwa ni wageni toka nje ya hiyo nchi,na pia kulikuwa na migahawa ya Waafrika kama Tunisia,Misri na Algeria ambao walikuwa wanauza "halal food" kwa jamii ya Waislam.Karibu yake kulikuwa pia na Mgahawa wa Mzimbabwe ambaye alikuwa anapika vyakula vya Kiafrika, wao wakiuta ugali kama "Sadza"(wanatamka Saza).

Mgahawa mwingine ulikuwa ni wa Muhindi,ambaye baadae nilikuja kujua alizaliwa Bukene-Tabora,na fimilia yake ilikimbia Tanzania baada ya Azimio la Arusha. Hapa ilikuwa nikitaka biriani, chicken Massala, Lamb Steck, pilau,sambusa, bajia na kababu, basi napata...na tulikuwa tunabonga Kiswahili vizuri na habari za Tanganyika na Nyerere.Alikuwa Muhindi Mnyamwezi anayeijua Tanganyika vizuri.

Kwenye huu mtaa nilizunguka usiku mgahawa kwa mgahawa kuosha vyombo baada ya muda wa watu kula kuisha,pia baadhi ya migahawa weekend nilikuwa napata kazi ya muda ya kuhudumia sababu niliweza Kingereza na pia kidogo lugha ya hiyo nchi,wengi wa wateja wa migahawa hii ni wale waliokuwa wanasumbuka kuongea lugha ya hii nchi ila wanaongea walau Kingereza cha mawasiliano.

Niliosha sana vyombo hii mitaa,mpaka nikazoeleka.Na pengine walinipenda sababu hawakuwa wananilipa kiasi kikubwa kutokana na aina ya viza niliyokuwa nayo, ila kazi niliyokuwa nafanya ni kubwa.Japo bia kwa kiasi nilichopata kibongo ilikuwa pesa nzuri niliyo-save sana.

Mara moja nipo katika Mgahawa ninahudumia,ilikuwa weekend,wakaja watu weusi wanne.Ilikuwa ni nadra kuona mtu mweusi mitaa ile,na mara unapomuona basi unamchangamkia sababu unahisi kuwa ni mwenzako, hata kama hamtoki nchi moja.Na kwa sababu hujui nchi anayotoka utaanza na kingereza.

Wale walikuwa ni watumishi wa umma toka Wizara ya Kilimo,ambapo waliletwa kuja kupata mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya kutoa ukufunzi katika chuo cha Kilimo Ukiliguru(nilijua baadae). Niliwachangamkia sana

Baadae kuwauliza wanachotaka,wakasema niwape muda wachague MENU, then mmoja akaniuliza nafanya kazi pale?nikamwambia just part time, naosha vyombo na weekend kama ile napata nafasi ya kuhudumu, basi wakanieleza wanachotaka kula,nikiwa bado naendelea kuandika "order" yao, mmoja akabadili lugha akaongea kwa Kiswahili "Waafrika bhana, sasa huyu kaacha nchi yake anakuja huku kuosha vyombo na kuuza migahawani". Nilistuka kidogo.

Mmoja akahisi kustuka kwangu,akaniuliza kwa Kingereza unatokea nchi gani Afrika?haraka nikasema Namibia...ooh sasa hapa unaishije?nikasema nafanya tu kazi hizihizi za kuosha vyombo nk.

Basi pale nikawa nimefungulia bomba la majungu, wacha waniseme...sengenya sana.Wakawa wanajiona na wao wanajua sana maisha, nikikatiza karibu na meza yao basi nasikia wanavyong'onga.Nikaomba wenzangu kuwa mie mnipe meza kadhaa nizihudumie, iliwepo ya wale watz,so nikawa nimejitega karibu ili wakihitaji kitu iwe rahisi kuwapelekea.

Basi wale jamaa walining'ong'a sana mie kuosha vyombo na kuuza mgahawani.Sasa katika maongezi yao,ilikuwa wanataka kwenda madukani kununua zawadi za kurudi nazo home,maana walibakiza siku chache kurudi. Walikuwa hawana mtu wa kuwapeleka, hotel waliyofikia maduka ya jirani ni gharama sana sababu ni eneo katikati ya mji.Mmoja alitaka radio ya kanda mbili, mwingine saa na nguo na viatu kwa ajili ya mkewe.

Niliwasikia,na nilikuwa najua sehemu za bei rahisi wanaweza kupata na hata maduka ya used ambazo zina viwango tu kama mpya.Lakini nikakaa tu kimya.Baadae mmoja akashauri tumuulize "Mnamibia" atakuwa mwenyeji.

Baadae wakashauriana,wakati napeleka bills,wakaomba kama nina muda na ninajua niwasaidie,nikawaambia nitafanya hivyo sababu wao ni waafrika wenzangu,nimefurahi kuwaona.Wasivyo na haya wakabadili Kiswahili kuwa "hawezi kukataa ana njaa huyu,tutampa hela kidogo akitusaidia".Halafu akanigeukia akasema "Thank you very much Sam Nujoma,we are at this Hotel...(akanionyesha kadi ya hotel),come to take us there"

Kesho mie nikaenda kuwasomba,nikawatia kwenye sub-way mpaka madukani,njia nzima wanang'ong'a tu.Mie kimyaa,wakiulizana wakashindwana wananiuliza kwa Kingereza,nawajibu,na sababu nakuwa naelewa msingi wa mabishano yao,nawajibu kiufasaha.

Tumefika madukani wakazuzuka na vitu, kila wanachoona wanatamani.Wakanunua vitu vingi mpaka hata "mgawo" wangu wakakosa,wakawa wanajishauri kuwa tukifika hotelini tutampa shukurani yetu huyu jamaa. Wakawa wamepanga wote wachangie "flat rate" wanipe.

Lakini pia pale hotelini walikuwa wanapewa pombe kali vyumbani kila siku,wakapanga wanisombee wanipe baada ya kujua natumia kinywaji. Niliwasikia na kuelewa.

Tulimaliza shopping na kurudi hotelini,njiani story za hapa na pale...Tumefika hotelini wakawa wanachangishana pale wanipe shukrani yangu,basi wakaenda juu vyumbani wakashuka na box la pombe na hile pesa.Jamaa akanipa box la pombe nikapokea,halafu akanipa bahasha,nikamuuliza kwa Kiswahili fasaha "Humu umeweka nini?isije ikawa bomu la bahasha lililomuua Mondlane"...Jamaa walistuka sana, kabla hawajakaa sawa nikawaambia "Sisi Watanzania ni wajamaa,nimewasaidia kijamaa bila malipo,nachukua pombe sababu ni za bure mmepewa,pesa hapana,mkinilipa hamtakumbuka wema wangu"

Jamaa wakataka kujikojolea,nikawaambia sio kwamba naosha vyombo kwa dhiki,ni maisha tu,nachopata kwenye kuosha vyombo mfanyakazi wa Tanzania anakipata kwa mwezi mzima na huyo ni mwenye degree. Nafurahi kuwafahamu, natokea Tanzania na nimefurahi kuona mmekuja kuongeza elimu kwa ajili ya Taifa, jamaa walitepeta sana.

Mwisho nikawaambia,nina makovu ya ubaguzi wa rangi katika hii nchi sababu weusi ni wachache hasa katika huu mji naoishi,nilipowaona nilifurahi sana, lkn kwa sababu mlijua mie wa Namibia mkanisengenya sana,sio jambo zuri...Nikawaaga jamaa nikaondoka,mpaka natoka nje ya geti la hoteli jamaa wamesimama wananicheki natokomea na box langu la pombe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom