Kisa cha kweli: Jinsi nilivyosengenywa na "kubaguliwa" na Watanzania wenzangu nchi ya ugenini

Hiyo tabia tunayo sana waswahili tukiona mtu huelewi kiswaz, siku moja tumetoka ubalozini tushapiga vyombo vya bure mara ndani ya metro na wazungu wamekaa ikatokea harufu kali ya ushuzi nahisi mmoja wetu pale alijamba, ushuzi wa maharage kabisa.
Basi bana tunaanza "mmh mmmmh, duh e bana kuna jamaa kaachia ushuzi"
Mwingine anajibu si huyo nguruwe hapo"mzungu"
Kadakia mwingine "sijui kala nini kumabake"
Mwingine "aah mayai visa hayo du e bana unanuka kishenzi"
Basi bana tunaendelea kumteta kumbe jamaa anajua kiswahili fasta akatujibu.
Mzungu"mmh SIJAJAMBA jamani usinisingizie sio mimi"
Dah ile noma tulishuka kituo kinachofata kwa aibu tunasubiri treni ingine 30 min bila kupenda.
 
Kuna jamaa alikuwa anasifia makalio ya dada mmoja hivi tupo supermarket, kumbe yule dada ni Msomali anaelewa kiswahili vizuri tu. Nikamuona dada anaishia kucheka tu.

Nilichojifunza, usimseme mtu hata kama hajui lugha yako, kwanza ni rahisi mtu kung'amua anasemwa kwa ile verbal expression tu. Mtu anaweza kukumind ukaishia kusema mbona mimi sijamfanyia kitu, huu ni ubaguzi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwangu huwa hakuna kazi duni!

Hivi, mtu anayekuhudumia mgahawani kwa nini umuone kuwa anafanya kazi duni?

Mimi mtu yeyote anayenipatia huduma yoyote ninayoihitaji namuheshimu sana.
Wewe mbeba boksi ndo mana unatetea, yaani mtu unaacha kupiga hata misheni town Lumumba unaenda kuwa mbwa Ulaya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah pole sana mkuu!mimi nilishawahi kutetwa na wadada wakipare kwenye daladala kwa sababu ya foni nilizovaa bila wao kujua kwamba sikuwa naplay chochote na kipare nakifahamu vizuri tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Hakuna mijitu inasengenya kama michaga, mimi nakunywa kwenye glossary yao na misengenyo juu napata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku tulikuwa mkoa mbali na nyumbani baba akachukua taxi kutupeleka nyumbani, ile gari ilikuwa mbovu sana Mzee akaanza kuponda kwa kikwetu kuwa gari ni mbovu sana na dereva ni feki hajui kuendesha vizuri, jamaa alikuwa mpole tu ile tunafika nyumbani jamaa akatuaga kwa lugha yetu akitutakia usiku mwema, tukapoteana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom