Kirusi cha Mwilini na Kirusi cha Kijamii!

Kirusi cha Mwilini na Kirusi cha Kijamii!

Shukran Twin
Hakika kosa ni mara moja na mtu anapokosea ata hurumiwa na kupewa nafasi nyingine ya kujitasmini upya


Lakini tabia ya kuumiza wengine na kila sehemu mtu huyo anapokanyaga anaacha maumivu na masononeko huyu mtu huruma sio halali yake anatakiwa kuwajibishwa kwa sababu tayari yeye ni kirusi akiacwa na kuchekewa anaweza kufanya zaidi

So sometimes huruma sio malezi
Sahihi kabisa, huruma inapaswa kuendana na uwajibikaji Twin.
 
Virusi vipo vingi sana- na kama baadhi ya wadau wametanabahisha vipo kila kona.
Kwa upande wa mwili kiafya ni vile viini vinavyosababisha maradhi(huingilia na kutatiza mifumo ya utendaji muafaka wa kazi mwilini.) Mtu anaweza kuvipata Virusi hivi kwa kuambukizwa au kwa bahati mbaya kutoka kwenye mazingira anayoishi hivi vinakuwa vitu miongoni mwa vitu hai (Microorganisms). Hivi huweza kutibiwa.
Kwa upande wa kompyuta, virusi ni mifumo(Programs) zinsizo ni miongoi mwa zile zilizojengwa na kuwekwa ndani ya kompyuta husika bali ni programs zinazoingilia na kutatiza ile mifumo iliyowekwa ndani ya kompyuta tangu kuundwa kwake. Hizi sio vitu hai - huweza kuangamizwa kwa kufutwa au kuzuiwa na antivirus programs.
Kwa upande wa Jamii; kirusi cha kijamii ni Watu/Mtu na Tabia zake, Utaratibu, Desturi, Mila au Imani fulani ndani ya jamii mahalia ambavyo ni vikwazo au vizuizi vya Ustawi na Maendeleo ndani ya jamii na huwa ni kero ndani ya jamii hiyo. Virusi hivyo ndo vinakuwa ndo visababishi vya kuwepo kwa Sheria (dawa ya kuvidhibiti na kuviondoa). Kwa mantiki hiyo; kila mtu ni kirusi kwa namna moja au nyingine kutegemea na yule anayefanya Tathmini. Kwa mfano uongozi katika Jamii unaweza kuwa ni kirusi kwa Viongozi kutokuwa makini (Not serious) kutumia vibaya madaraka yao kukandamiza na kuonea watu, Kufuja mali za Jamii(Misuse of public resourses/embezzlement), Kutofuata Taratibu zilizokubaliwa n.k. n.k. Virusi katika Jamii mara nyingi husababisha ukosefu wa Haki na Jamii kuwa na manung'uniko, lawama na malalamiko yasiyoisha, kukosekana kwa utulivu na amani.
Tiba mujarabu sana (Dawa) kwa Kirusi cha Kijamii huwa ni Majadiliano, Vikao/Mazungumzo ya hadhara na kuweka makubaliano au maelewano yahusuyo ni nini kifanyike-(the way forward) ili kuondokana na sintofahamu iliyojitokeza. Wahusika wajitambue na kuwa wanyenyekevu katika kikao hicho.
Matumizi ya Ubabe, Uwezo wa kiFedha, Ghilba, Ujanja-ujanja kwa lengo la kutibu Kirusi cha Kijamii haijawahi kufaulu hata siku moja tokea enzi na enzi kwa waliojaribu kuzitumia njia hizo.
Samahani jamani kwa kuandika gazeti. Asante
Matumizi ya Ubabe,Uwezo wa kifedha ghilba,ujanja ujanja kwa lengo lake kutibu kirusi cha kijamii haijawahi kufaulu hata siku moja tokea enzi na enzi kwa walio jaribu kuzitumia njia hizo!

Ahsante kwa maoni yako mjarabu wala huna haja ya samahani gazeti lime nyooka halina kipengele 🔥🔥🔥
 
Mimi pia Twin nilifanya kama wewe japo haikua rahisi hata kidogo nikachagua kujitenga kabisa

Nikakubali athari za muda mfupi
Kwa imani ya faida lukuki za mbeleni
Safi Twin maana kwenye game, ni ngumu kufanikiwa kama usipo-freeze baadhi ya watu.
 
Hakuna kirusi kibaya kama binadamu, yaani kuna kirusi nilishakikataa toka mwaka 2019, juzi tu nikawa naongea na ndugu yake fulani tena baada ya kumsaidia hitaji lake, nikamwambia kabisa nasaidia halafu mnakuwa kama yule ndugu yenu na nilishamkataa sitaki chochote kile . Salamu, msaada wake wowote maana alichangia sana kunivurugia ikiwemo kunitapeli, kunipakazia maneno ya uongo ( bora mchawi unaweza ukajikinga naye kwa dua au maombi kuliko jitu liongo)

Kimsingi virusi vingine vya magonjwa au vile virusi vya mtandaoni vina tiba lakini BINADAMU ni kirusi kibaya mnoo
 
Matumizi ya Ubabe,Uwezo wa kifedha ghilba,ujanja ujanja kwa lengo lake kutibu kirusi cha kijamii haijawahi kufaulu hata siku moja tokea enzi na enzi kwa walio jaribu kuzitumia njia hizo!

Ahsante kwa maoni yako mjarabu wala huna haja ya samahani gazeti lime nyooka halina kipengele 🔥🔥🔥
Una upeo mpana sana Muslimah
 
Hakuna kirusi kibaya kama binadamu, yaani kuna kirusi nilishakikataa toka mwaka 2019, juzi tu nikawa naongea na ndugu yake fulani tena baada ya kumsaidia hitaji lake, nikamwambia kabisa nasaidia halafu mnakuwa kama yule ndugu yenu na nilishamkataa sitaki chochote kile . Salamu, msaada wake wowote maana alichangia sana kunivurugia ikiwemo kunitapeli, kunipakazia maneno ya uongo ( bora mchawi unaweza ukajikinga naye kwa dua au maombi kuliko jitu liongo)

Kimsingi virusi vingine vya magonjwa au vile virusi vya mtandaoni vina tiba lakini BINADAMU ni kirusi kibaya mnoo
Dah aisee issue ya 2019 mpka leo umemsaidia mtu na umekumbuka hakika huyo alikua kirusi haswa

Bora alikubakiza haja kuua
 
Kirusi... mara nyingi tunaposikia neno kirusi, tunafikiria maradhi

Kirusi ni maambukizi ambayo huingia mwilini na kuanza kuharibu taratibu, chini kwa chini(ma Doctor kama nakosea nisahihisheni)

Mara nyingi unaweza usigundue mapema, na ukichelewa kupata matibabu sahihi, madhara yake yanaweza kuwa makubwa, hata kusababisha kifo

Hapo naongelea kirusi cha maradhi, mfano UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukiza

Lakini je, umewahi kufikiria kuwa hata binadamu anaweza kuwa kama kirusi?

Kuna watu ambao popote walipo hawawezi kuhakikisha usalama amani au ustawi wa waliowazunguka

Badala yake, hueneza taharuki, migogoro, hofu na mkanganyiko Taratibu huathiri hisia, akili na hata maisha ya wengine

Yaani kuna wale watu hawawezi kutulia ila mpaka waone machozi au damu aridhini wana ka ushetani automatically

Je binadamu anaweza kua
Kama kirusi?
Maoni yangu 👇

Ndiyo, wakati mwingine mtu anaweza kuwa kama kirusi na kuleta madhara makubwa kwa wanaomzunguka

Na wote tunajua 👇

Kirusi cha mwilini hakipewi dawa za kukifanya kiwe dhaifu tu hutafutiwa tiba ya kukiangamiza ili kisizidi kuharibu mwili

Vivyo hivyo, mtu anapogeuka kuwa kirusi katika jamii kwa kuendelea kuwa chanzo cha uharibifu kwa wengine, unadhani jamii inapaswa kushughulika naye kwa namna gani ili kuzuia madhara yasienee zaidi?

Je, umewahi kuishi na binadamu ambaye ungeweza kumfananisha na kirusi?

Na unadhani ni sahihi kumtenga au kumzuia mtu ambaye amekuwa chanzo cha uharibifu mkubwa kwa wengine, kwa kiwango kinacholingana na madhara anayoyasababisha?

ShesRise_1 ✋️
Kwa ufupi sana
Mifumo ya kurekebisha tabia kama jela au gereza au mahabusu ilianzishwa kwa makusudi ili kuwatenga wanadamu virusi ili wasisababishe taharuki kwa wengine. Laiti kama mifumo hii ingetumika vizuri changamoto zinazosababishwa na hawa virusi nyingi zingepungua.
 
Back
Top Bottom