Kirusi cha Mwilini na Kirusi cha Kijamii!

Kirusi cha Mwilini na Kirusi cha Kijamii!

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
17,264
Reaction score
40,900
Kirusi... mara nyingi tunaposikia neno kirusi, tunafikiria maradhi

Kirusi ni maambukizi ambayo huingia mwilini na kuanza kuharibu taratibu, chini kwa chini(ma Doctor kama nakosea nisahihisheni)

Mara nyingi unaweza usigundue mapema, na ukichelewa kupata matibabu sahihi, madhara yake yanaweza kuwa makubwa, hata kusababisha kifo

Hapo naongelea kirusi cha maradhi, mfano UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukiza

Lakini je, umewahi kufikiria kuwa hata binadamu anaweza kuwa kama kirusi?

Kuna watu ambao popote walipo hawawezi kuhakikisha usalama amani au ustawi wa waliowazunguka

Badala yake, hueneza taharuki, migogoro, hofu na mkanganyiko Taratibu huathiri hisia, akili na hata maisha ya wengine

Yaani kuna wale watu hawawezi kutulia ila mpaka waone machozi au damu aridhini wana ka ushetani automatically

Je binadamu anaweza kua
Kama kirusi?
Maoni yangu 👇

Ndiyo, wakati mwingine mtu anaweza kuwa kama kirusi na kuleta madhara makubwa kwa wanaomzunguka

Na wote tunajua 👇

Kirusi cha mwilini hakipewi dawa za kukifanya kiwe dhaifu tu hutafutiwa tiba ya kukiangamiza ili kisizidi kuharibu mwili

Vivyo hivyo, mtu anapogeuka kuwa kirusi katika jamii kwa kuendelea kuwa chanzo cha uharibifu kwa wengine, unadhani jamii inapaswa kushughulika naye kwa namna gani ili kuzuia madhara yasienee zaidi?

Je, umewahi kuishi na binadamu ambaye ungeweza kumfananisha na kirusi?

Na unadhani ni sahihi kumtenga au kumzuia mtu ambaye amekuwa chanzo cha uharibifu mkubwa kwa wengine, kwa kiwango kinacholingana na madhara anayoyasababisha?

ShesRise_1 ✋️
 
Homie,hakika binadamu nao ni virusi sana,kuna watu ambao nawajua kwa tabia zao za kupenda kuona wengine wanaharibikiwa,binafsi kuna watu kama wawili ambao wamechangia sana kuwafukuzisha watu kazi na kuharibu maisha yao

Huwa najiuliza je wanapata hisia gani kuona wenzao wakiharibikiwa? Wanapata furaha gani wengine wakimwaga machozi

Najua huenda wengine wapo humu na tunasomana sana,ndugu yangu unapata faida gani ukiwaharibia watu maisha yao,je unapewa cheo chao? Unapewa mshahara wao?

Je utaishi milele hapa duniani? Kuwa mtu mwema na wewe ndio uwe sababu ya watu kutabasamu
 
Mimi pia hujiuliza mtu unapata nini kua kama kirusi kwenye maisha wa watu

Au ndiyo huo ushetani wenyewe?
 
Back
Top Bottom