Kirusi cha Mwilini na Kirusi cha Kijamii!

Kirusi cha Mwilini na Kirusi cha Kijamii!

Poor Brain ukimaliza huko upite na hapa maana naona notification tu 😎
Na unadhani ni sahihi kumtenga au kumzuia mtu ambaye amekuwa chanzo cha uharibifu mkubwa kwa wengine, kwa kiwango kinacholingana na madhara anayoyasababisha?

Ni sahihi kabisa... Mfano mkubwa mimi nina mdogo angu aiseeee 🙌 daah ni story ndefu ila naona mama mkubwa ana. Mlea sana huyu jamaaa
 
Dawa ya kirusi jamii ni sheria na katiba ya nchi ilionyooka.
Ukitumia maamuzi yako kumuona mwenzio kirusi ukamuangamiza kumbe wewe ndio kirusi konki kumbuka ukishaangamiza ni hakuna kuhuisha, sasa kama ulikosea?
 
Na unadhani ni sahihi kumtenga au kumzuia mtu ambaye amekuwa chanzo cha uharibifu mkubwa kwa wengine, kwa kiwango kinacholingana na madhara anayoyasababisha?

Ni sahihi kabisa... Mfano mkubwa mimi nina mdogo angu aiseeee 🙌 daah ni story ndefu ila naona mama mkubwa ana. Mlea sana huyu jamaaa
Huyo mdogo wako kafanyaje share kama hutojali
 
Dawa ya kirusi jamii ni sheria na katiba ya nchi ilionyooka.
Ukitumia maamusi yaku kumuona mwenzio kirusi ukamuangamiza kumbe wewe ndio kirusi konki kumbuka ukishaangamiza ni hakuna kuhuisha, sasa kama ulikosea?
Nimesoma mara ya kwanza
Nikarudia tena na tena

Asante kwa maoni mkuu karibu tena
 
Nimeupenda mfano ulioutumia kwa sababu umegusa jambo ambalo watu wengi huwa wanaliona lakini hawalipi jina.

Unajua kuna tofauti kati ya mtu kukosea kwa bahati mbaya na mtu ambaye uharibifu ni kama umekuwa sehemu ya tabia yake. Watu wote huwa tunakosea, lakini sio kila mtu ameyajenga maisha yake juu ya kuwaumiza wengine. Ndiyo maana binafsi huwa siamini kabisa kwamba kila mtu anayesababisha migogoro anastahili kutetewa kwa hoja ileile ya kusema ndivyo alivyo. Kuna wakati ukweli unapaswa kusemwa bila kuupamba.

Kuna msemo unaosema, character is a pattern, not an incident, hii ndiyo hoja kuu. Mtu anaweza kukosea mara moja na akajutia kosa lake lakini kama kila sehemu anayopita lazima anaacha migogoro, kila kundi analoingia linaishia kugawanyika, kila uhusiano anaouanzisha lazima uishie kwenye chuki na lawama, hatuwezi kusema hii ni bahati mbaya tena, bali ni tabia ambayo inakuwa ni sehemu ya utu wake.

Jamii nyingi huwa zinaanguka kwa sababu ya watu wachache wenye tabia za uharibifu kuachwa waendelee bila kuwajibishwa, huruma ni muhimu, lakini huruma inapaswa kwenda sambamba na hekima. Kumvumilia mtu ambaye kila siku anazalisha migogoro ni kuwatelekeza wale anaowaumiza.

Kuwalinda waathirika ni jambo la haki kama ilivyo kumpa mkosaji nafasi ya kubadilika lakini kama ameonyesha kwa muda mrefu kwamba hataki kubadilika, basi kumuwekea mipaka na kumuwajibisha inapaswa kuwa ni wajibu.

Kwahiyo kifupi ni kwamba, jamii ikishindwa kutofautisha kati ya mtu ambaye anahitaji kusaidiwa na yule anayehitaji kuzuiwa ni lazima itajikuta inalinda chanzo cha tatizo badala ya kuwalinda waathirika wake.
 
Kirusi... mara nyingi tunaposikia neno kirusi, tunafikiria maradhi

Kirusi ni maambukizi ambayo huingia mwilini na kuanza kuharibu taratibu, chini kwa chini(ma Doctor kama nakosea nisahihisheni)

Mara nyingi unaweza usigundue mapema, na ukichelewa kupata matibabu sahihi, madhara yake yanaweza kuwa makubwa, hata kusababisha kifo

Hapo naongelea kirusi cha maradhi, mfano UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukiza

Lakini je, umewahi kufikiria kuwa hata binadamu anaweza kuwa kama kirusi?

Kuna watu ambao popote walipo hawawezi kuhakikisha usalama amani au ustawi wa waliowazunguka

Badala yake, hueneza taharuki, migogoro, hofu na mkanganyiko Taratibu huathiri hisia, akili na hata maisha ya wengine

Yaani kuna wale watu hawawezi kutulia ila mpaka waone machozi au damu aridhini wana ka ushetani automatically

Je binadamu anaweza kua
Kama kirusi?
Maoni yangu 👇

Ndiyo, wakati mwingine mtu anaweza kuwa kama kirusi na kuleta madhara makubwa kwa wanaomzunguka

Na wote tunajua 👇

Kirusi cha mwilini hakipewi dawa za kukifanya kiwe dhaifu tu hutafutiwa tiba ya kukiangamiza ili kisizidi kuharibu mwili

Vivyo hivyo, mtu anapogeuka kuwa kirusi katika jamii kwa kuendelea kuwa chanzo cha uharibifu kwa wengine, unadhani jamii inapaswa kushughulika naye kwa namna gani ili kuzuia madhara yasienee zaidi?

Je, umewahi kuishi na binadamu ambaye ungeweza kumfananisha na kirusi?

Na unadhani ni sahihi kumtenga au kumzuia mtu ambaye amekuwa chanzo cha uharibifu mkubwa kwa wengine, kwa kiwango kinacholingana na madhara anayoyasababisha?

ShesRise_1 ✋️
Virusi vipo vingi sana- na kama baadhi ya wadau wametanabahisha vipo kila kona.
Kwa upande wa mwili kiafya ni vile viini vinavyosababisha maradhi(huingilia na kutatiza mifumo ya utendaji muafaka wa kazi mwilini.) Mtu anaweza kuvipata Virusi hivi kwa kuambukizwa au kwa bahati mbaya kutoka kwenye mazingira anayoishi hivi vinakuwa vitu miongoni mwa vitu hai (Microorganisms). Hivi huweza kutibiwa.
Kwa upande wa kompyuta, virusi ni mifumo(Programs) zinsizo ni miongoi mwa zile zilizojengwa na kuwekwa ndani ya kompyuta husika bali ni programs zinazoingilia na kutatiza ile mifumo iliyowekwa ndani ya kompyuta tangu kuundwa kwake. Hizi sio vitu hai - huweza kuangamizwa kwa kufutwa au kuzuiwa na antivirus programs.
Kwa upande wa Jamii; kirusi cha kijamii ni Watu/Mtu na Tabia zake, Utaratibu, Desturi, Mila au Imani fulani ndani ya jamii mahalia ambavyo ni vikwazo au vizuizi vya Ustawi na Maendeleo ndani ya jamii na huwa ni kero ndani ya jamii hiyo. Virusi hivyo ndo vinakuwa ndo visababishi vya kuwepo kwa Sheria (dawa ya kuvidhibiti na kuviondoa). Kwa mantiki hiyo; kila mtu ni kirusi kwa namna moja au nyingine kutegemea na yule anayefanya Tathmini. Kwa mfano uongozi katika Jamii unaweza kuwa ni kirusi kwa Viongozi kutokuwa makini (Not serious) kutumia vibaya madaraka yao kukandamiza na kuonea watu, Kufuja mali za Jamii(Misuse of public resourses/embezzlement), Kutofuata Taratibu zilizokubaliwa n.k. n.k. Virusi katika Jamii mara nyingi husababisha ukosefu wa Haki na Jamii kuwa na manung'uniko, lawama na malalamiko yasiyoisha, kukosekana kwa utulivu na amani.
Tiba mujarabu sana (Dawa) kwa Kirusi cha Kijamii huwa ni Majadiliano, Vikao/Mazungumzo ya hadhara na kuweka makubaliano au maelewano yahusuyo ni nini kifanyike-(the way forward) ili kuondokana na sintofahamu iliyojitokeza. Wahusika wajitambue na kuwa wanyenyekevu katika kikao hicho.
Matumizi ya Ubabe, Uwezo wa kiFedha, Ghilba, Ujanja-ujanja kwa lengo la kutibu Kirusi cha Kijamii haijawahi kufaulu hata siku moja tokea enzi na enzi kwa waliojaribu kuzitumia njia hizo.
Samahani jamani kwa kuandika gazeti. Asante
 
Nimeupenda mfano ulioutumia kwa sababu umegusa jambo ambalo watu wengi huwa wanaliona lakini hawalipi jina.
Shukran Twin
Unajua kuna tofauti kati ya mtu kukosea kwa bahati mbaya na mtu ambaye uharibifu ni kama umekuwa sehemu ya tabia yake. Watu wote huwa tunakosea, lakini sio kila mtu ameyajenga maisha yake juu ya kuwaumiza wengine. Ndiyo maana binafsi huwa siamini kabisa kwamba kila mtu anayesababisha migogoro anastahili kutetewa kwa hoja ileile ya kusema ndivyo alivyo. Kuna wakati ukweli unapaswa kusemwa bila kuupamba.

Kuna msemo unaosema, character is a pattern, not an incident, hii ndiyo hoja kuu. Mtu anaweza kukosea mara moja na akajutia kosa lake lakini kama kila sehemu anayopita lazima anaacha migogoro, kila kundi analoingia linaishia kugawanyika, kila uhusiano anaouanzisha lazima uishie kwenye chuki na lawama, hatuwezi kusema hii ni bahati mbaya tena, bali ni tabia ambayo inakuwa ni sehemu ya utu wake.

Jamii nyingi huwa zinaanguka kwa sababu ya watu wachache wenye tabia za uharibifu kuachwa waendelee bila kuwajibishwa, huruma ni muhimu, lakini huruma inapaswa kwenda sambamba na hekima. Kumvumilia mtu ambaye kila siku anazalisha migogoro ni kuwatelekeza wale anaowaumiza.

Kuwalinda waathirika ni jambo la haki kama ilivyo kumpa mkosaji nafasi ya kubadilika lakini kama ameonyesha kwa muda mrefu kwamba hataki kubadilika, basi kumuwekea mipaka na kumuwajibisha inapaswa kuwa ni wajibu.

Kwahiyo kifupi ni kwamba, jamii ikishindwa kutofautisha kati ya mtu ambaye anahitaji kusaidiwa na yule anayehitaji kuzuiwa ni lazima itajikuta inalinda chanzo cha tatizo badala ya kuwalinda waathirika wake.
Hakika kosa ni mara moja na mtu anapokosea ata hurumiwa na kupewa nafasi nyingine ya kujitasmini upya

Lakini tabia ya kuumiza wengine na kila sehemu mtu huyo anapokanyaga anaacha maumivu na masononeko huyu mtu huruma sio halali yake anatakiwa kuwajibishwa kwa sababu tayari yeye ni kirusi akiacwa na kuchekewa anaweza kufanya zaidi

So sometimes huruma sio malezi
 
Back
Top Bottom