Mkuu wewe unaji contradict sana...si ndo nyie mnaodai kwamba eti kwanini anaachia mabaya wakati ana uwezo wa kuyaondoa..mara Oooh sijui kwanini hakuumba ulimwengu usiokua na mabaya .... sasa huku si ndo kumpangia katika maamuzi yake ama ??
Au wenzangu nyie hamuelewi hata hicho mnachokisimamia..tokea mwanzo sijaona solid arguments zenu zaidi ya kuuliza swali ndani ya swali.
Hapana, kumpangia ni hivi.
Mungu: Mimi ni Mungu mbaya, naua watu, nawapa magonjwa, sijali wakiwa na njaa.
Kiranga: Wewe Mungu ni mbaya, ungekuwa mzuri usingeua watu, usingewapa magonjwa, ungejali wakiwa na njaa.
Hapo utasema Kiranga anampangia Mungu.
Lakini hili si lililopo.Tunachoambiwa ni hiki.
Mungu: Mimi ni Mtakatifu sana, nina upendo wote, ujuzi wote, uwezo wote. Kisha, nina ghadhabu kali, nahukumu wana kwa makosa ya baba na babu zao, naua wanyama kwa makosa ya watu. Naruhusu mabaya duniani hata kama naweza kuyazuia na niliweza kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani. Naua mpaka vitoto vichanga kwa kuvifukia kwa matetemeko ya ardhi.
Kiranga: Mungu, mimi sikupangii, najua unafanya unachotaka kufanya, lakini mbona hueleweki? Mbona unasema wewe una uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, halafu unaachia mabaya? Kwa nini hukuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hapo sijampangia, nimehoji mbona yeye mwenyewe anajipinga ?