Naam,
Mpaka sasa sijaona mtu aliyekanusha hili.
Kama Mungu yupo, ni muweza wa yote, mwenye upendo wote, ujuzi wote na kaumba ulimwengu huu, kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea.
Jibu la makosa ya mtu si jibu sahihi, Mungu angeweza kuumba dunia ambayo makosa hayawezekani.
Jibu la shetani si hibu sahihi, Mungu angeweza kuumba ulimwengu ambao shetani hawezi kuwepo.
Jibu la free will si jibu sahihi, Mungu angeweza kufanya mabaya hayawezekani kufanyika kama natural law, kama vile ambavyo hatuwezi kurudi nyuma katika muda, hatuwezi kurudi nyuma katika muda lakini wanaosema Mungu katupa free will hawasemi hilo linazuia free will.
Sijapata jibu la swali hili bado.