Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote: ulimwengu huu unaoonekana na usioonekana, binadamu na viumbe vyote.
Dunia, binadamu na viumbe vingine vinavyoonekana, ni bayana na wazi wazi, visivyo na kasoro yoyote kimantiki.
Uwepo wa binadamu, dunia na viumbe vingine, jinsi ya kila kimoja, kwa chenyewe na ndani yake, ni uthibitisho wa asili moja.
Uwepo wa hivi: dunia, binadamu na viumbe vingine, kwa vyovyote vile sio suala la bahati nasibu.
Kumbe, kama wewe ni mchunguzi wa kweli wa mambo, utaona uwepo wa hivi vitu (dunia, binadamu na viumbe vingine), ni kwa NGUVU FULANI. Hii nguvu ndio huitwa Mungu.
Uwepo na uwamo wa nguvu hii ndani ya dunia, ndani ya binadamu na ndani ya viumbe vingine, hufanya viumbe hivi vifanye kazi hivyo vinavyoonekana kwetu.
Ulimwengu: dunia, binadamu na viumbe vingine, unavyofanya kazi: mfumo wake, mpangilio wake, ukamilifu wake, na uzuri wake, ni uthibitisho wa wazi wa uwepo wa Mungu.