Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Basi sawa upo sahihi kabisa ndugu yangu

Uwe na usiku mwema
Katika wale wawili waliobisha kwamba Mungu hayupo,naona hapa amebakia mmoja,huyo mwingine ameenda wapi ? Unatakiwa kuahariri upya hiki ulichokindika.

Hapa naona wamekuwa wawili tena kama walivyo anza.

Hili la idadi sababu sio la msingi,nimelipuuza ila unatakiwa uwe makini sana.

Haya uliyo yaandika hayakuwa na maana zaidi ya swali la msingi,ni kuwa kwanini kuna utofauti wa dini na mitazamo ? Hili ndio swali la msingi na umetumia muda mwingi sana kuweka wazi jambo ambalo liko wazi,kufanya kwako hivyo kumeonyesha una udhaifu mkubwa sana wa kutafakari mambo na kuyaweka katika hitimisho moja na fupi.
 
Hapa inaonekana wazi kabisa tatizo lilianzia kwa wale wa kwanza walio andika Biblia kwa kushindwa kujua ni yapi maneno ya Mungu na yapi ni kinyume chake.

Hii ina maanisha ya kuwa kwa mchanganyiko huu Biblia si maneno ya Mungu.

Na pia kuna uwezekano katika maneno hayo ya binadamu ndani ya Biblia hakuna hata neni moja la Mungu,na hili hakuna anae weza kulipinga kielimu
Ukijichunguza vizuri utagundua wewe ndio una tatizo. Kwanini? Kwa sababu unakataa kitu ambacho unacho ndani yako.
Lakini pia, kando na hapo, hujui hasa Mungu ni nini? Hujui biblia ni nini? Na hujui dini ni nini?
 
Nakukumbusha ya kuwa nimekuuliza maswali kutokana na kile unacho kieleza,ajabu unashindwa kukitetea na kukijengea hoja.

Namjua Mola wangu kuliko unavyofikiri sababu namsoma na nitaendelea kumsoma mpaka naondoka hapa duniani,ama kuhusu tamko "Dini" kwa uhakika kabisa nalijua tamko hili kushinda wewe na unavyolisikia na kulitumia.

Kuhusu Biblia kweli siijui na huwa siisomi,ila huwa nahoji kutokana na nyinyi mnavyo ielezea,mwisho wa siku mnashindwa kuitetea Biblia yenu.
 
Bila shaka kabisa na wewe ni miongoni mwa wale walioshindwa kutofautisha hilo.

Kwa maana nyinyi mmeamua kuishi kwenye dhana katika maisha yenu yote.
Huwezi kuelewa haya ninayoandika kwani hujui hata hicho unachokipinga.
Bahati mbaya zaidi hata hicho unachoona ndio uhalisia hukijui.
 
Huwezi kuelewa haya ninayoandika kwani hujui hata hicho unachokipinga.
Bahati mbaya zaidi hata hicho unachoona ndio uhalisia hukijui.

Hili unaweza kulithibitisha pia,kwa kukipinga hiki ninacho kueleza na wewe kuweka usahihi wako kama wewe unasema kweli.

Nafasi iko wazi thibitisha kutokujua kwangu,ama kuishia kidai tu bila kuonyesha hilo unakiwa unaikosea adabu elimu na ukweli pia.
 
Kuhusu Biblia kweli siijui na huwa siisomi,ila huwa nahoji kutokana na nyinyi mnavyo ielezea,mwisho wa siku mnashindwa kuitetea Biblia yenu.
Hii tu pekee inatosha kuonyesha wewe ni mtu gani.
Mtu anayetaka kujua ukweli hawezi kuwa wa namna yako. Maana yake wewe ni mbishi tu: usiye jali.
 
Hii tu pekee inatosha kuonyesha wewe ni mtu gani.
Mtu anayetaka kujua ukweli hawezi kuwa wa namna yako. Maana yake wewe ni mbishi tu: usiye jali.
Hayo niliyo yahoji nimeyatunga au nimeyahoji baada ya wewe kuizungumzia Biblia ?

Ugonjwa wako usinitupie mimi. Kwangu mimi kusema sijui ni nusu ya kuwa na elimu,sababu kwanza nimejitambua kwamba sijui na hii ni hatua kubwa sana kwani wapo ambao hawajui kama hawajui.

Ulichotakiwa wewe ni kuukosoa ufahamu wangu na kunipa majibi ya kielimu,sasa ulikuwa unajichanganya sana,mwisho wa siku unani tuhumu mimi kuwa ni "Mbishi".

Siwezi kujali sababu kwa hakika sibishani ndio maana kufikia muafaka huwa si lengo la mjadala wa kielimu.
 
Ulichotakiwa wewe ni kuukosoa ufahamu wangu na kunipa majibi ya kielimu,sasa ulikuwa unajichanganya sana,mwisho wa siku unani tuhumu mimi kuwa ni "Mbishi".
Kimsingi, wewe ndio unachanganya kwa kushindwa kuelewa hasa maana ya maneno ninayoandika yamebeba nini.
Ukitaka kujua hilo rejea maswali yako unayouliza utagundua yanarudia kitu kile kile.
 
Kuthibitisha ni kubainisha kitu kwa uwazi, bila utata wala pingamizi la kimantiki linaloweza kuleta mkanganyiko wa ukweli.

Hujaonesha kwamba ulimwengu unathibitisha uwepo wa Mungu, hili unalazimisha,

Hujaonesha uwazi wa kimantiki unaounganisha ulimwengu na Mungu, unalazimisha tu
Mungu ndiye Muumba wa vitu vyote: ulimwengu huu unaoonekana na usioonekana, binadamu na viumbe vyote.
Dunia, binadamu na viumbe vingine vinavyoonekana, ni bayana na wazi wazi, visivyo na kasoro yoyote kimantiki.
Uwepo wa binadamu, dunia na viumbe vingine, jinsi ya kila kimoja, kwa chenyewe na ndani yake, ni uthibitisho wa asili moja.
Uwepo wa hivi: dunia, binadamu na viumbe vingine, kwa vyovyote vile sio suala la bahati nasibu.
Kumbe, kama wewe ni mchunguzi wa kweli wa mambo, utaona uwepo wa hivi vitu (dunia, binadamu na viumbe vingine), ni kwa NGUVU FULANI. Hii nguvu ndio huitwa Mungu.
Uwepo na uwamo wa nguvu hii ndani ya dunia, ndani ya binadamu na ndani ya viumbe vingine, hufanya viumbe hivi vifanye kazi hivyo vinavyoonekana kwetu.
Ulimwengu: dunia, binadamu na viumbe vingine, unavyofanya kazi: mfumo wake, mpangilio wake, ukamilifu wake, na uzuri wake, ni uthibitisho wa wazi wa uwepo wa Mungu.
 
Kwa hiyo kama ulimwengu umeumbwa na gravity, gravity ni Mungu?
 
Ndio. Yesu ni Mungu.
Inasemekana kwamba YESU alikufa msalabani pale kulingana na hadithi za biblia. Ingawa tunaambiwa kwa MUNGU hawezi kufa. Sasa kwanini YESU ambaye ni MUNGU afe tena?

Pia, YESU alizaliwa na Maria pale Nazareth kulingana na hadithi za biblia. Kwa upande mwingine tunaambiwa kwaMUNGU hakuzaliwa.

Nne, Soma kitabu cha Yohana ndipo utaona YESU anakiri na kusema kwamba anaenda kwa baba yake. Na baba yake YESU anajulikana ni nani.
Yohana 14:2
Yohana 14: 6
Yohana 14: 28.

Kwa mujibu wa mafungu hayo, YESU siyo MUNGU.
 
Kwa hiyo kama ulimwengu umeumbwa na gravity, gravity ni Mungu?
Kama utakumbuka, nilishawahi kukuuliza: what is God. Wewe ukaleta uswahili kwenye mambo serious.
Kimsingi, wewe ni mtu usie jua chochote, mbinafsi, usiejali na usiye taka kujifunza.
Wewe si tu hujui hicho unachokitetea, lakini pia hujui sayansi, hujui psychology, hujui philosophy hujui theology. Ni shabiki tu usie jua hicho unachokifuata ni nini.
Ukitazama kwenye Profile yako hapo juu, you are titled JF Expert. Sitaki kujua ni vigezo gani wanaangalia. Lakini wewe huna chochote cha kustahili sifa hiyo.
Angalia unavyojenga hoja, angalia unavyofafanua hoja, tazama unavyopokea mawazo ya wengine. Hii yote inakuondolea sifa ya 'Expert'.
Ninachokusihi jifunze: tafuta taarifa sahihi juu ya elimu hizi: Science, Psychology, Philosophy na Theology, utaelewa ukweli.
 
Kimsingi, wewe ndio unachanganya kwa kushindwa kuelewa hasa maana ya maneno ninayoandika yamebeba nini.
Ukitaka kujua hilo rejea maswali yako unayouliza utagundua yanarudia kitu kile kile.
Mimi naweza kukuonyesha wapi ulipokuwa unajichanganya na kurudia jibu lile lile mwisho ukakubali ule muongozo nilio kupa ya kuwa kuna dhati ya matini na kuna maneno ya waandishi.
 
Inasemekana kwamba YESU alikufa msalabani pale kulingana na hadithi za biblia. Ingawa tunaambiwa kwa MUNGU hawezi kufa. Sasa kwanini YESU ambaye ni MUNGU afe tena?
Masimulizi ya biblia yanasimulia kweli. Hivi ndivyo ilivyokuwa: Yesu alikufa msalabani kweli.
Yesu alikuwa Mungu kweli na Yesu alikuwa mtu kweli.
Je, unafahamu Kifo cha Yesu kilikuwa kwa ajili ya nini?
 
Mimi naweza kukuonyesha wapi ulipokuwa unajichanganya na kurudia jibu lile lile mwisho ukakubali ule muongozo nilio kupa ya kuwa kuna dhati ya matini na kuna maneno ya waandishi.
Unajua Matini maana yake ni nini?
 
Unajua Matini maana yake ni nini?
Najua,ndio maana nimeandika,na mimi nimefundishwa juu ya kuongea au kuandika ninacho kijua,nisicho kijua huwa sikiandiki zaidi ya kuuliza au kutanguliwa na maelezo husika.

Unajua matini ni nini ?
 
Pia, YESU alizaliwa na Maria pale Nazareth kulingana na hadithi za biblia. Kwa upande mwingine tunaambiwa kwaMUNGU hakuzaliwa.

Nne, Soma kitabu cha Yohana ndipo utaona YESU anakiri na kusema kwamba anaenda kwa baba yake. Na baba yake YESU anajulikana ni nani.
Yohana 14:2
Yohana 14: 6
Yohana 14: 28.
Soma vizuri Biblia utaelewa kwanini Yesu ni Mungu.
 
Back
Top Bottom