Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Ndugu naomba nikujibu hivi:
"Mungu", hili ni jina linalojaribu kuelezea, hapa niite nguvu iliyofanya ulimwengu, binadamu na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Jina hili " Mungu" lina maana hasa ya kuelezea uwezo wa mwisho wa binadamu kwenye kutambua hii nguvu kuu.
Ukweli hapa, ni 'hii nguvu' iliyofanya hivi vitu, ulimwengu, binadamu na viumbe vingine kwa jinsi hiyo ya ajabu: kamilifu, pangilifu na nyoofu.
Dini, hatahivyo, tangu mwanzo imekuwa na inaendelea kusema juu ya NGUVU HII 'MUNGU'. Yesu Kristo ni mfano bora zaidi kuliko mwanadamu mwingine yoyote (sublime moral) duniani aliyekuja kuifunua hii nguvu. Ingawa siyo kwa ukamilifu wote.
Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Kwako wewe Bublia si maneno ya Mungu sababu kuna vifungu vina pingana au ? Naomba ufafanuzi kidogo.
Hapana! Biblia ni, NENO LA MUNGU. Hakika biblia ni neno la Mungu.
Kupingana huku kwa masimulizi fulani fulani ya vitabu vya biblia kunaonyesha uwezo wa binadamu usivyo bado kuelewa na kuweza kueleza ukamilifu wa Mungu.
 
[emoji30][emoji30][emoji30][emoji30][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] swali la akili alishindwa kabisa/alichomoa kujibu
Akili ni nini?

Wewe uliyeuliza swali linalohusiana na akili ukishindwa hata ku define maana ya neno akili.

Usilete uongo hapa.
 
Au unahisi kwamba kuna siku watu watamuelewa Mungu vizuri kisha huko kujigonga kwa hayo maandiko kutapotea au kutabakia ?
Ulimwengu: dunia, mwanadamu na vitu vingine, hivi vyote vinasafiri. Binadamu yumo njiani anasafiri kuelekea utimilifu wake. Dunia nayo imo njiani inasafiri kuelekea mwisho wake. Hivyo hivyo kwa viumbe vingine.
Hivyo, utafikia muda: nyakati zinakuja binadamu atamjua Mungu wazi wazi. Binadamu atamwona Mungu uso kwa uso.
 
Ndugu naomba nikujibu hivi:
"Mungu", hili ni jina linalojaribu kuelezea, hapa niite nguvu iliyofanya ulimwengu, binadamu na vitu vyote vinavyoonekana na visivyoonekana. Jina hili " Mungu" lina maana hasa ya kuelezea uwezo wa mwisho wa binadamu kwenye kutambua hii nguvu kuu.
Ukweli hapa, ni 'hii nguvu' iliyofanya hivi vitu, ulimwengu, binadamu na viumbe vingine kwa jinsi hiyo ya ajabu: kamilifu, pangilifu na nyoofu.
Dini, hatahivyo, tangu mwanzo imekuwa na inaendelea kusema juu ya NGUVU HII 'MUNGU'. Yesu Kristo ni mfano bora zaidi kuliko mwanadamu mwingine yoyote (sublime moral) duniani aliyekuja kuifunua hii nguvu. Ingawa siyo kwa ukamilifu wote.
Yesu nae ni MUNGU?
 
Lakini je katika kutokuelewa u kugongana kwa hivyo vifungu je ushawahi kuotuhumu akili yako au elimu ya kuwa haijaweza kukidiriki kile kilicho zungumzwa katika vifungu hivyo ?
Hivi vifungu vyote, licha ya kupingana, ndani yake na kile vilichonacho ndio ukweli, yaani Mungu. Kwamba kupingana kwavyo ni kwa kibinadamu zaidi. Lakini ukiacha maneno ukatazama ndani utagundua kitu kile kile 'Mungu'.
 
Suala Ni kwamba

Kwanini hayo mambo au mandiko yanayoitwa ya Mungu yasiwe bayana kwa watu wote wakati yeye ni muweza..!?

Kwanini asubirie mpaka waliovimbirwa chai ya mohogo watafsiri maandiko yake na kusababisha utofautiano wayo..!?

Kwanini wengine wayaelewe na wengine washindwe kuyaelewa huoni kupuuza kwake hilo kinasababisha mijadala Jf kumhusu yeye isiishe..?
Ninafahamu wewe (binadamu) unafahamu uko tofauti na viumbe vingine. Binadamu wewe hufanani, kwa mfano na viumbe kama ng'ombe, samaki, njiwa, kunguni, miti, na kadhalika.
Jinsi yako binadamu ni ya pekee kushinda viumbe vingine vyovyote vilivyoumbwa ulimwenguni.
Utafahamu wewe unayo akili na utashi: unavitumiaje?
Maandiko Matakatifu ya Mungu ni bayana kwa kila mwanadamu. Lakini mwanadamu anaweza kuchagua Maandiko Matakatifu ya Mungu yasiwe bayana kwake.
 
Nimekuaachia nafasi ya kupinga kwa facts.

Nikakwambia kama unasema Mungu yupo, thibitisha yupo.

Hujathibitisha.
Tangu awali nilikujibu kwamba, uthibitisho wa kwamba Mungu yupo ni huu:
Kwanza, Ulimwengu na vitu vinavyoonekana.
Pili, mwanadamu.
Zaidi nilithibitisha kwamba Mungu yupo kwa uthibitisho huu.
Kweli za wafu na maisha
baada ya kufa.
Labda tulejee kwenye neno lenyewe, "THIBITISHA, UTHIBITISHO", wewe unaelewa maana yake ni nini?
 
Ulimwengu na vitu vinavyoonekana vinathibitisha vipi kwamba Mungu yupo?
 
Hapana! Biblia ni, NENO LA MUNGU. Hakika biblia ni neno la Mungu.
Ili tamko liwe neno la Mungu linatakiwa liwe na sifa gani ?
Kupingana huku kwa masimulizi fulani fulani ya vitabu vya biblia kunaonyesha uwezo wa binadamu usivyo bado kuelewa na
Kwa maana hiyo Biblia kwa dhati yake haijipingi si ndio ?

Kama kupingana kwa vifungu ni kwa dhati yake huoni kama Biblia inakosa sifa ya kuwa neno la Mungu ?
 
Hivyo, utafikia muda: nyakati zinakuja binadamu atamjua Mungu wazi wazi. Binadamu atamwona Mungu uso kwa uso.
Kwa kauli yako basi hapakuwa na haja ya kuwepo vitabu hivyo sababu havimfanyi binadamu kumjua Mola wake vilivyi.

Kwetu sisi waislamu ni kinyume. Unahisi kwanini kumekuwepo hivyo vitabu na ili iweje ?
 
Hivi vifungu vyote, licha ya kupingana, ndani yake na kile vilichonacho ndio ukweli, yaani Mungu. Kwamba kupingana kwavyo ni kwa kibinadamu zaidi. Lakini ukiacha maneno ukatazama ndani utagundua kitu kile kile 'Mungu'.

Kwa maana hiyo unatakiwa kubatilisha kauli ya mwanzo na kusema ya kuwa tatizo si vifungu bali tatizo ni ufahamu wa binadamu na uchachefu wa maarifa yake,kama nilivyokudokeza hapo ya kuwa,lazima uhituhumu akili yako au elimu yako kwa kushindwa kuyadiriki yaliyomo kwenye vifungu.
 
Ungejibu swali langu kwanza. Kutoka hapo tutaendelea.
Nakuuliza tena:
"THIBITISHA au UTHIBITISHO", wewe unaelewa maana yake ni nini?
Leo utauliza mpaka maana maana yake nini.

Kuthibitisha ni kubainisha kitu kwa uwazi, bila utata wala pingamizi la kimantiki linaloweza kuleta mkanganyiko wa ukweli.

Hujaonesha kwamba ulimwengu unathibitisha uwepo wa Mungu, hili unalazimisha,

Hujaonesha uwazi wa kimantiki unaounganisha ulimwengu na Mungu, unalazimisha tu
 
Back
Top Bottom