Kitu ambacho hujui ni kwamba, dawa hata iwe ya ukweli au uongo, ili iweze kumponya mgonjwa inategemea akili ya mgonjwa ilivyokubali kwa kiasi chote hiyo dawa, na anaempa hiyo dawa. Mfano, dawa inaweza kutibu malaria, lakini kama mgonjwa hajaikubali hataweza kupona.
Kwenye huu mfano wako wa watoto hapo juu, unatengeneza maswali mengi. Kwanza hatuoni ni ugojwa gani mtoto wa miaka mitano anaumwa. Hivyo ni kwa hakika gani tunaweza kuthibitisha kwamba dawa aliyopewa mtoto mwenye miaka mitano ni ya uongo? Lakini pia, mtoto wa miaka mitano anaumwa, tufikiri kwamba na yeye hajui anaumwa nini. Ni kwa namna gani utasema hiyo dawa aliyopewa kisha akapona haitibu ugonjwa huo, ni fake?