Kaka mimi ni shabiki wa uwezo wako wa akili na elimu ulonayo (kutoka kwenye hoja zako na uwezo wa kuchanganua mambo humu JF!). Nakiri!
Mimi ni 'Small Thinker'. And I am proud of it! Mimi ni Muislam. And I am proud of it. At times hua naziona hizi 'you so-call contradictions' kwenye vitabu vitakatifu. (Kwa hekima alonipa Mungu, ambae wewe huamini uwepo wake!) nimeamua kuichukua dini kama Lifetyle yngu).
Km hutojali, na ww tafuta imani yako (yoyote ile, be it paganism, etc!). Ifanye iwe dini itakayo shape your Lifestyle.
#Ghandi #Luther #Dr Hellen (Sabath) #Muhammad (May P.B.U.H) walizitafuta zao, zikawavutiwa watu, watu wakazifuata. Na ww tafuta yako.
Kwanza kabisa, nataka ksema kwamba, mimi sina nia ya ku bughudhi watu wanaoamini Mungu, wanaoamini dini.
Nina kawaida ya kuandika vitu kwa nuance, kama huelewi, kunichanganya ni rahisi sana.
Narudia, sina tatizo na wanaoamini dini, wanaoamini Mungu.
Naelewa imani ni jambo la faragha, ni jambo la uamuzi wa mtu binafsi.
Na zaidi, nikiona watu wanaoamini Mungu na dini wanaonewa, wananyimwa haki yao hiyo ya kimsingi, nitawatetea.
Nitawatetea hata kwenye jambo nisilokubaliana nao, kuhusu wai kuabudu Mungu anbaye sikubali yupo. Kwa sababu kwangu mimi, uhuru wa kuabudu kwa watu wote ni kitu cha msingi kuliko kama wanachoabudu ni kweli au si kweli.
Hivi karibuni rais Kagame wa Rawanda alisema atapiga marufuku makanisa ywenye wachungaji wasio na degree. Nilishutumu kauli ile kwamba inaingikia uhuru wa kuabudu, na watu wanatakiwa wawe na uhuru wa kuabudu kanisa lolote wanalitaka bila vikwazo.
Ungawa sikubali Mungu yupo, natetea uhuru wa juabudu wa watu wanaoamini Mungu yupo.
Mimi napenda uhuru wa kuabudu. Katiba ya Tan,ania inatoa uhuru huu.
Naoenda sana "The Universal Declaration of Human Rights" iliyopitishwa December 10 1948. Hii ni document ya UN inayotoa uhuru wa juabudu, iki nradi watu wasiingikie uhuru wa wengine na kuvunja sheria.
Kwa hiyo, nataka nikuhakikishie, sinatatizo na mtu anayesema ana imani fulani.
Nina tatizo na mtu anayesema anajua ukweli huyo Mungu wake yupo.
Huyu sasa anakuwa kajitoa katika imani, kajiingiza katika fact.
Na akishajiingiza katika fact tu, kanipa ruhusa kumuhoji.
Kwa hiyo ukiniambia niamini ninavyotaka, mimi sitaki kuamini vyovyote, nataka kujua.
Na ukiniambia nikuache unavyoamini, watu wanaoamini sijawahi kutaka kuwagusa, nawagusa wanaosema wanajua Mungu yupo.
Ukisema unaamini tu, that is not so special kwangu. Unaruhusiwa kuamini chochote.
Ukisema unajua Mungu yupo kweli, hapo nakuomba uthibitisho.