Kiranga sio atheist ni non-believer

Kiranga sio atheist ni non-believer

Kwa sababu hata kisichopo, usipokijua, kinawezakukuua.

Kama dawa ya ugonjwa haipo,na kinga ndiyo muhimu, mtu akaaminishwa dawa ipo, akaupata huougonjwa, akauziwa kanyaboya kama dawa, kutokuwapo kwa dawa hiyo anayouziwa kama kanyaboya kunamuua.

Mungu hayupo, nikama dawa hiyo ya kanyaboya.

Watu watatue matatizo yao wenyewe, kumtegemea Mungu ni kutegemea dawa ya kanyaboya.

Mtakufa kwa magonjwa kwa kutozingatia kinga na kutafuta dawa halisi kwa kuwa mmebweteka kwenye dawa ya kanyaboya.

Hapo ndipo utajua kwamba ujinga unaua.

Imani kwamba kitu kipo, wakati hakipo, inaweza kukuua.
Kwaivyo hii ndio jumla ya khasara anayopata Mtu anayeamini Mungu.!?

Ila ningekua safi kama ungeorodheshaa na faida wanazopata wasioamini Mungu
 
Hapana tofautisha fikra za mtu mmoja kama hapo kwenye mfano wako na uhalisia wa fikra katika wingi wake....
Abracadabra zako hazinipati mimi.

Huna mpya.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.
 
Prove kwamba sijui basi, kwa kumuelezea huyo Mungu wako kwa jinsi ambayo iko logically consistent na haiwezi kuwa contradicted.

Hahaha umewahi kusoma au kuona nahangaika kuthibitisha kwa mtu Mungu yupo?

Nimeshasoma mara nyingi ukisema mambo ya kuamini na wewe havipikiki chungu kimoja. Na hauwezi kutenganisha imani na Mungu. Kwa mantiki hiyo, siwezipoteza muda.

Lakini sababu kubwa ya kutokufanya hivyo ni moja tu. Ni jukumu la Mungu kujithibitisha na kujidhihirisha mwenyewe.

Sasa nnapokuuliza kitu kingine au kutaka maelezo unalazimisha au unajibu kwa muktadha wa uthibitisho wa Mungu, inanitatiza.
 
Nani kasema hiyo ni jumla?
We si Umesema ujinga wa kuamini Mungu Unaua.!? iyo ndio jumla au una nyengine.?

Sasa nataka utuoneshe werevu wa kutoamini Mungu unavyo huisha...

Au nimenukuu vibaya..!? yawezekana sijaelewa mimi
 
Abracadabra zako hazinipati mimi.

Huna mpya.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.
Hili ndio jibu lako ama ndio mtazamo wako? Achana na mambo ya kupatana ama kutopatana...
 
Kwa sababu Mungu hayupo.

Angekuwepo, kila kitu kingekuwa kinaoana bila hata juhudi.

Kwa andiko hili, unakubali kwamba ulichokiandika hakioani na nilichokiandika, haimaanishi vingeoana ningekua nimethibitisha kwako kwamba Mungu yupo.
 
Hahaha umewahi kusoma au kuona nahangaika kuthibitisha kwa mtu Mungu yupo?

Nimeshasoma mara nyingi ukisema mambo ya kyamini na wewe havipikiki chungu kimoja. Na hauwezi kutenganisha imani na Mungu. Kwa mantiki hiyo, siwezipiteza muda.

Lakini sababu kubwa ya kutokufanya hivyo ni moja tu. Ni jukumu la Mungu kujithibitisha na kujidhihirisha mwenyewe.

Sasa nnapokuuliza kitu kingine au kutaka maelezo unalazimisha au unajibu kwa muktadha wa uthibitisho wa Mungu, inanitatiza.
Huwezi kuthibitisha Munguvwako yupo.

Kwa sababu hayupo.
 
We si Umesema ujinga wa kuamini Mungu Unaua.!? iyo ndio jumla au una nyengine.?

Sasa nataka utuoneshe werevu wa kutoamini Mungu unavyo huisha...

Au nimenukuu vibaya..!? yawezekana sijaelewa mimi
Kuna vitabu na vitabu vimeandikwa kuhusu hilo jambo.

Unatakaje kupata jumla kwa post ya JF tu?
 
Huwezi kuthibitisha Munguvwako yupo.

Kwa sababu hayupo.

Sijawahi na wala hakuna mahali popote nilishasema naweza kuthibitisha Uwepo wa Mungu.

Nikaona kwa kuwa mambo ya imani na wewe hamuendi pamoja, nikaamua nikuulize maswali kwenye yale unayoyaandika. Unajua mwenyewe kilichotokea.

Mfano wa Kiranga nilioutoa haukutaja uwepo wa Mungu.

Nikakuuliza kuweka chanzo cha hizo sifa za Mungu, haujataja.
 
Mshana anachekesha sana!

Imepita miaka sasa toka tukubaliane kuwa aniroge lakini wapi!

Bado nipo nadunda tu hahahaa.
Unajua ngabu hata wafu hawajui kuwa wamekufa... Wanaojua ni wale waliobaki hai...
 
Unajua ngabu hata wafu hawajui kuwa wamekufa... Wanaojua ni wale waliobaki hai...
Kama vile wajinga wanaomuamini Mungu ambaye hayupo ambavyo hawajui Mungu huyo hayupo.

Wanaojua hayupo ni wasiomuamini Mungu huyo.
 
Kwa andiko hili, unakubali kwamba ulichokiandika hakioani na nilichokiandika, haimaanishi vingeoana ningekua nimethibitisha kwako kwamba Mungu yupo.
Waswahili walisema Lila na fila hazitengamani.

Wewe hata kuoana hujui ni nini

Ndoyo maana unaamini mauzauza ambayo hata kuyaelezea huwezi.

Utajuaje kipi kinaoana na kipi?
 
Kuna vitabu na vitabu vimeandikwa kuhusu hilo jambo.

Unatakaje kupata jumla kwa post ya JF tu?
Nataka maelezo yako wewe sio wao.

Tena kwa post ya hapa JF ndio kila kitu.hazina mawaa, kwa uchache tu...halafu jumla nitaipata we niachie mimi

Sitaki kusoma hizo faida kwenye mavitabu yawezekana aliyeandika hakuzimaliza, Na pia yawezekana Kafa.!

Nataka wewe ambaye Bado Wamotomoto unapumua.nisije nikamuonea Marehemu kumhoji au vitabu vyake...wakati wengine wapo Hai na Wanafikika kupitia JF
 
Wewe mawazo yote yako kwenye ramli.

Hata ukiwekewa logical argument unaona ramli tu.
Hiki kitu unakipenda sana mpaka kimekuwa ni kama ibada takatifu kwako hiki unachopenda kukiita 'logical argument ' ambayo hata hivyo ukiambiwa iweke, unaishia kuweka link za mabandiko ya wazungu yenye mkanganyiko mkubwa ... Kwako hawa ndio viumbe sensible....
 
Kama vile wajinga wanaomuamini Mungu ambaye hayupo ambavyo hawajui Mungu huyo hayupo.

Wanaojua hayupo ni wasiomuamini Mungu huyo.

Unapata wapi mamlaka ya kuita wanaoamini Mungu yupo wajinga?

Umeshawahi kufanya utafiti kupata hitimisho kati ya wanaoamini na wasioamini ni kundi lipi bora kuliko lingine? Mfano uwezo wa kuelewa mambo, kusimamia mambo, elimu, uongozi, uvumbuzi, maeneo tofauti ya kitaaluma na utaalam, uhandisi n.k

Kwa hiyo hata Albert Einstein au Isaac Newton kama waliamini uwepo wa Mungu nao ni wajinga?

Maoni au mtazamo wako ubaki kuwa wako na sio lazima watu wengine waukubali.
 
Back
Top Bottom