Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 3,542
- 3,451
Tanzania tuna hazina kubwa sana ya wosia ambao umegusa karibu kila eneo ambalo leo hii tunaouona kama changamoto kwa Taifa.
Mimi ni muumini wa falsafa ya ujamaa wa Kiafrika na katika maisha yangu ninatembea na vitabu viwili vikubwa yaani Biblia na Ujamaa.
Kitabu cha "Ujamaa" cha mwaka 1968 kilichoandikwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kuchapishwa na Dar es Salaam OXFORD UNIVERSITY PRESS.Ni kitabu cha pili cha maisha yangu Baada ya Biblia.
Kipindi tunataka kuwashawushi wawekezaji kurudi tukumbuke maneno haya
"..makampuni yanayotaka kuja katika Nchi yetu kuanzisha shughuli mbalimbali kwa manufaa yao wenyewe. Na sharti kubwa walitakalo jamaa hawa wenye fedha zao ni kwamba shughuli yenyewe iwe ni ya faida kwao na pia kwamba Serikali iwaruhusu kuondoa faida hiyo na kupeleka kwao. Huenda pia kwa jumla Serikali iwe na siasa wanayokubaliana nayo ambayo haihatarishi uchumi wao.
......Ni ujinga vilevile, kwa kweli ni ujinga zaidi, tukidhani kuwa tunaweza kuondoa hali hii ya unyonge wetu kwa kutegemea fedha kutoka nje badala ya fedha zetu wenyewe( uk, 21-22).
Itaendelea..