Mkuu sasa unabore kilasiku thread zako ni Mnyika na Halima Mdee mbona huku kigamboni husemi acha unafiki una ujinga wa kitoto
una akili kama za kuku yaani mbili tu!kuwa na upinzani sio kwamba wote watakuwa wasafi,tuwe na ngozi ngumu ya kukosolewa,mwanza mea alikuwa chdm na madiwani wengi ni cdm na sheria za miji zinatungwa na kusimamiwa na cdm na mbunge akiwepo,unasemaje sasa?Kwa maajabu ya Tanzania na mfumo wake wa elimu, unaweza kuta mtu mwenye mawazo kama haya yako amemaliza chuo.
Parking ya gari anaamua mbunge kupanda au kushuka gharama yake?
Shida yetu hatufahamu mfumo wa maamuzi na utekelezaji katika maeneo yetu. Halmashauri zina nguvu ya kuamua hilo, sasa sijui juu ya nini hamzitumii kufanya maamuzi hayo. Kitu pekee anachoweza kufanya mbunge katika hilo ni kuwaomba madiwani wa chama chake waligomee hilo kwenye vikao vya halmashauri, Je, wapo wangapi katika halmashauri?
hapo manake hatoshi.inabidi uchaguzi ujao tumpe mbunge wa chama kilichopo madarakani ili aweze kutekeleza
Wenye akili timamu tunajua tunachofanya. Huyu mafilili kwani ye ni mkazi wa Jimbo gani! Segerea yupo, Ubungo yupo yupo kwenye majimbo yote yanayoongozwa na CDM. Fuatilieni thread zake za e nyingi tu ni kero kwa wabunge wa CDM.Wananchi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi kigumu cha kukosa mwakilishi aliye makini bungeni katika kipndi cha mwaka 2010 kuelekea 2015. Mbunge aliyeingia kwa mbwembwe nyingi Halima Mdee amekuwa ni zigo lisilosaidia wapiga kura badala yake anajisaidia mwenyewe.
Tangu amechaguliwa:
1. Hapendi kuitisha mikutano ili kupata mawazo ya wananchi
2. Wananchi wa Madale waliopatwa na mashambulizi ya polisi wamekosa pole na msaada wake
3. Wakazi wa Majipwande wanamlilia kwa kutopata msaada wa mali na faraja toka kwake
4. Mfuko wa Jimbo haujatolewa maelelezo kwa wananchi
5. Kushindwa kutekeleza ahadi zake za kuinua kiuchumi vikundi vya vijana na wanawake
6. Kushindwa kutatua matatizo wanayoyapata vijana wa bodaboda na bajaji
Hizo ni kero chache ambazo zilitakiwa zifanyiwe kazi na mbunge wetu.
Kwa kweli wakazi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi tete tunamkumbuka RITA Mlaki ambaye alikuwa karibu na wapiga kura.
Na
hajamaliza kusaga walio kwenye orodha yake. Atakuja tu msiwe na hofu.
Wananchi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi kigumu cha kukosa mwakilishi aliye makini bungeni katika kipndi cha mwaka 2010 kuelekea 2015. Mbunge aliyeingia kwa mbwembwe nyingi Halima Mdee amekuwa ni zigo lisilosaidia wapiga kura badala yake anajisaidia mwenyewe.
Tangu amechaguliwa:
1. Hapendi kuitisha mikutano ili kupata mawazo ya wananchi
2. Wananchi wa Madale waliopatwa na mashambulizi ya polisi wamekosa pole na msaada wake
3. Wakazi wa Majipwande wanamlilia kwa kutopata msaada wa mali na faraja toka kwake
4. Mfuko wa Jimbo haujatolewa maelelezo kwa wananchi
5. Kushindwa kutekeleza ahadi zake za kuinua kiuchumi vikundi vya vijana na wanawake
6. Kushindwa kutatua matatizo wanayoyapata vijana wa bodaboda na bajaji
Hizo ni kero chache ambazo zilitakiwa zifanyiwe kazi na mbunge wetu.
Kwa kweli wakazi wa jimbo la Kawe tupo katika kipindi tete tunamkumbuka RITA Mlaki ambaye alikuwa karibu na wapiga kura.
CHADEMA kubalini kupokea ushauri ili huyo mbunge wenu wa kawe aendelea kutawala..... badala ya kutukana ..tatizo lenu hamtaki kupokea ushauri kwa mambo yanayohusu chama chenu..mnajiona muda wote mko sawa... ukweli uko wazi mdee hakuna alichokifanya hadi muda huu zaidi ya kupiga kelele bungeni kwa mambo ya jumla jumla tu..... mi nawambia ukweli 2015 wabunge wa upinzani hasa CHADEMA ni wa chache sana watakaorudi kuwa wabunge .... ushauri pokeeni ushauri huu haitajiki hata laki tano kwenda kufanya mkutano na wananchi kwenye maeneo ya wananchi wenye matatizo , yani kufanya mkutano kusikiliza kelo za wananchi nalo linahitaji ela za CCM???.AU USAIDIWE NA SERIKALI???. JITAZAMENI UPYA CHADEMA WENZENU WANATEKELEZA AHADI NINY MNAENDELEE NA MAANDAMANO SASA SIJUI 2015 MTASEMA TULIFANYA MAANDAMANO 100 AU TUMEJENGA ZAHANATI..KAZI MNAYOGombea basi wewe tukupe. We unataka mbunge ashugulikie kila kitu? hao wabunge wengine wamefanya nini? Magamba mna shida sana,, hizo pesa za jimbo waulize magamba wenzio maana wao ndo wanajua ziko wapi,,, wala usimlaumu Mdee. Na aliyekutuma mwambie huku JF tuko vizuri magorofani hatujadili hoja zisizo na mshiko. Huwezi anza kumlaumu mbunge wakati bado ana miaka miwili na ushee. Haya zile ahada 77 za mheshimiwa sana mbona huuliziii? kuna meli ngapi zimeshatengenezwa? Je kigoma imekuwa kama Dubai? Reli je? Nakushauri ukiwa bored badala ya kupost vitu kama hivi ingia hapa www.theudaku.blogspot.com:A S-coffee:
Angalau wewe Mkuu Mwita Maranya umejibu bila jazba lakini jawabu zako hazitoshelezi. Ingefaa ungeweka angalau data kidogo na/au ratiba kuhusu mikutano hiyo.Mkuu usikubali kusombwa na mafuriko ya siasa za maji ya chooni toka magamba.
Halima amekuwa anakutana na wananchi wa jimbo lake tangu bunge lilipomalizika. Mathalani wiki hii yote alikuwa na ratiba ya kukutana na wapigakura wake ofisini kwake kinondoni.
Lakini pia amekuwa akifanya mikutano mingi na wananchi huko mitaani, hata weekend hii ana mikutano kadhaa huko huko madale, mabwepande, chasimba na maeneo ya jirani.
Hawa magamba wanamzushia Halima ili kuhalalisha posho zao za kila siku.
CHADEMA kubalini kupokea ushauri
Angalau wewe Mkuu Mwita Maranya umejibu bila jazba lakini jawabu zako hazitoshelezi. Ingefaa ungeweka angalau data kidogo na/au ratiba kuhusu mikutano hiyo.
Ikiwa hoja ya mleta mada tunaona ni ya kipuuzi, ingekuwa busara na pigo kwa propaganda za Magwanda kuzizima kwa matokeo halisi na data, kuliko kulinganisha kwa kauli kavu na yaliyofanywa na Mkuu wa Wilaya/serikali, vyenginevyo kusingekuwa na haja ya kuwa na wabunge.
Kwa kuwa Mhe. Mdee huwa anaingia humu nahisi ni busara na yeye pia kufanya kama vile alivyofanya Marahemu Regia (R.I.P) au anavyofanya Mhe. Mnyika, aweke orodha ya ahadi zake jimboni na aliyofanya huko au pengine nchini, kulikoni sisi wapambe, wafuasi, wapenzi na wanachama wa CDM kuvurumisha makombora tu.
Mara kadhaa kuna watu humu wamesema kuwa udhaifu mmoja wa wapambe wa vyama vyetu vya upinzani hawapendi kukosolewa wala kupokea ushauri. Ni vizuri basi, haya yanayosemwa kuchukuliwa kama ni changamoto, ikiwa ni kweli zifanyiwe kazi na kama ni uongo zizimwe kwa nguvu ya hoja.
Ninakubaliana kabisa na wewe mkuu, lakini kuwanyamazia ndiko kunakowapa kidomodomo na kueneza propaganda zao. Kama nilivyosema, hapa pametolewa madi sita tu, pata muda au mwengine yeyote kutoka kawe, wamwagieni hapa data na matukio tuone kama akina MAFILILI na mwanakawe watakuwa na la kusema.Mkuu MAMMAMIA hawa watu wanafahamu fika shughuli anazofanya Halima Mdee isipokuwa kwakuwa wako kazini ndio maana wako busy kila siku kumtuhumu hajafanya hiki ama kile. Wakimaliza kwa Halima wanahamia kwa Mnyika, tena ni watu wale wale, leo wanasema wanakaa jimbo la kawe lakini kesho utawasikia wanajinadi kwamba wanakaa jimbo la ubungo.
Wakati mwingine mtu unaona hata uvivu kuwaandikia ratiba nzima ya mikutano ya Halima kwakuwa hawako hapa kwa nia nzuri. Mimi nakaa jimbo la Ukonga lakini bado ninafuatilia na kujua kinachofanyika kawe sembuse mtu anayejiita mwanakawe?