Kipindi cha Take One cha Clouds Tv chafungiwa miezi mitatu

Kipindi cha Take One cha Clouds Tv chafungiwa miezi mitatu

Inasemekana waarabu wapemba wanajuana kwa vilemba. Kama hao wakubwa wanakiona kama kituo cha mfano basi ni dhahiri wanafurahishwa na maudhui ya vipindi vya kituo hicho hivyo kuakisi uhalisia wa tabia zao pia. Kama Mkuu wa Mkoa ndio kituo chake teule cha kutangaza matamko yake wakati hapo hapo kituo hicho kinashadadia ufuska na ushoga basi ni wazi kuna dosari sehemu.
Exactly mkuu
 
TCRA ni wanafki sana, kwa nini wasikifungie kituo kama walivyofanya kwa vingine. Why Magic na radio 5 hawakufungia vipindi?? Yaan Clouds sijui wanachukuliwaje.
Shame on you! [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
Wababe wa media tz
 
Natamani TCRA wangekua humu niwachana nina mengi sana juu yao hata Instagram hamna nawatafuta sana
 
Hiki kituo kinasifiwa sana na wakubwa zetu, inakuwaje mara kwa mara kinafungiwa?
Usipende kukariri,mapenzi au hisia za mtu kwa kitu au vitu hubadilika, wala si msahafu au bible.
 
kumbe adhabu ya kufungia vipindi ipo mbona redio zongine ilikua ni kufungiwa radio na si vipindi vya redio? kipindi kimepigiwa makelele kuwa ni cha ovyo ovyo muda mrefu ndio mnakuja leo kweli...
inashangaza sana kuona vyombo vingine zinafungiwa program zote.....afu inapokuja ishu za Mawingu media wanajifanya kudil kimafungu....yawezekana hata hii azabu ikawa imeambatanishwa na kimemo cha kuwaomba mawingu msamaha
 
Zamaradi kwa vile kazaa na Ruge anajihisi hamna wa kumpangia maisha pale klauz anatukana wafanyakazi wenzie, anajisifia Ruge kamuweka mkononi ndo mana hata Joe Kusaga hawezi kumfukuza kazi.
Mbona na dini amembadilisha tayari si kumweka mkononi tu.
 
Heehee, mke kafungiwa kipindi hapa lazima mume akamuone mkuu wa mkoa ili anagalau adhabu ipinguzwe maana ni mpendwa wa clouz media.
 
Safi sana,Zama kiburi kimemjaa sana.
 
Clouds wanavyojifanya wabunifu wanaweza kuanzisha kipindi cha Take two..action wakaendelea kupiga mzigo kama kawaida,hawa jamaa si watu wa mchezo mchezo.
 
Lazima maadili tuhakikishe tunayazingatia. La sivyo tutakuwa tu tunajirushia vipindi kwa ajili ya kupata watazamaji na advertisements (money in other words) huku tukiiharibu jamii.
 
zamaradi bhana sijui alikuwa na lengo gani..hivi alianzaje kumtaka gigi ataje wanaume wote aliotembea nao?
anyway happy birthday zama muke ya le boss
Yanayotokea, ikiwemo hili la Zamaradi na hiyo Clouds, yana uhusiano mkubwa na jamii yetu ilipofikia. I tell u yapo mambo ya hovyo kabisa yanafanywa na hata wenye madaraka ya kufungia hicho kipindi au ya kusimamia taasisi muhimu. Fuatilia katika nyanja zote sasa; iwe ni katika siasa, elimu, uchumi, nakadhalika. Kwamba unapoona, kwa mfano, Msajili wa vyama vya siasa anakaa kimya pale wanasiasa wanapozuiwa kufanya siasa, lakini akashirikiana na polisi kumrudishia Lipumba uenyekiti na kumpeleka ofisini kwa maandamano ambayo yamepigwa marufuku na polisi haohao, ujue jamii imeoza.

Tunaweza kufungia kipindi cha Zamaradi, lakini tusipojitathimini kama taifa kwa habari ya uadilifu, hili wala haliwezi kutusaidia. Leo wengi wetu tumechagua kushabikia uovu na uhuni. Viongozi wetu wanashiriki uhuni, sisi wenyewe tunashangilia uhuni! Media zinazoathiri mfumo wa maisha ya watoto wetu kuanzia lugha hata mavazi ndio zinavutia audience na ndizo hizo wakubwa wetu wenye mamlaka "wanazipaisha". Haya ya Giggy money na Zamaradi ni tone tu katika bahari ya kukosekana kwa maadili ambayo taifa linaogelea.....
 
Tofauti na ilivyozoeleka kua wanasifiwa na kupaishwa kila mara leo tcra wamekifungia kipindi cha take one action kinachorushwa na clouds tv kwa kosa la kurusha vipindi vinavyohamasisha ngono kwa vijana.
 
Waifunge kabisa hiyo kampuni moja kwa moja kwani waliua wanamuziki wengi sana kwa kuwatwisha unga huko Afrika Kusini.
 
IMG_1475604977.327193.jpg


Je wadau hii adhabu ni sawa au?
 
Back
Top Bottom