hashim mwamba
JF-Expert Member
- Sep 2, 2016
- 1,018
- 1,105
Apo fresh
...double standardskumbe adhabu ya kufungia vipindi ipo mbona redio zongine ilikua ni kufungiwa radio na si vipindi vya redio? kipindi kimepigiwa makelele kuwa ni cha ovyo ovyo muda mrefu ndio mnakuja leo kweli...
View attachment 411976
Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.
“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema Mapunda.
Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00
Nlikuwa napita wanajamvi nikaona clouds tv wamejikwaa tena SA sijui hii itakua n bahati mbaya au ni maksudi lakini mbona hiki kipindi kilishapewa onyo na TCRA juu ya kuhamasisha ushoga juzi tena wamekuja na dhidi ya kuhamasisha biashara ya ngono naona vyota kikatiba haviruhusiwi na ni kosa kisheria vp adhabu walioitoa TCRA kwa mtu yule yule na kipindi kile kile eti kufungia kipindi je ni sahihi kwa maamuzi hayo?
Mie naona TCRA iweze kwenda mbali zaidi ya hapo ili kuweza kutengeneza jamii iliuostaharabika je wewe unaonaje?
Kipindi kimoja tu kilitosha kuvifungia vituo vya redio 5 na Magic Fm jumla, Clouds kinafungiwa kipindi tu na sio kituo kizima, ni double standards au selective approach au ni mtoto wa tumboni vs mtoto wa mgongoni?! Tafakari