Kipindi cha Take One cha Clouds Tv chafungiwa miezi mitatu

Kipindi cha Take One cha Clouds Tv chafungiwa miezi mitatu

Radio five ilifungiwa kabla ya kuhojiwa tena ni ndani ya siku 7. Leo Clouds imepita mwezi mzima kabisa ndio wanakuja kufungia kipindi?
Mkuu zimwi likujualo ndio kinachoendelea.Huyo kafanya "mchezo wa kafungia"ili aonekana kwa umma taasisi hiyo inafanya kazi,asije mwaga unga au kutumbulia akienda kinyume na wale waliomteua.Hivyo kaona heri robo shari kuliko shari kamili kwani nae watamtosa akiwashuparia kisawa sawa,ndio Tanzania yetu.
 
Hiki kituo kinasifiwa sana na wakubwa zetu, inakuwaje mara kwa mara kinafungiwa?
Inasemekana waarabu wapemba wanajuana kwa vilemba. Kama hao wakubwa wanakiona kama kituo cha mfano basi ni dhahiri wanafurahishwa na maudhui ya vipindi vya kituo hicho hivyo kuakisi uhalisia wa tabia zao pia. Kama Mkuu wa Mkoa ndio kituo chake teule cha kutangaza matamko yake wakati hapo hapo kituo hicho kinashadadia ufuska na ushoga basi ni wazi kuna dosari sehemu.
 
zamaradi bhana sijui alikuwa na lengo gani..hivi alianzaje kumtaka gigi ataje wanaume wote aliotembea nao?
anyway happy birthday zama muke ya le boss
 
View attachment 411976

Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.

Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo, Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

“Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema Mapunda.

Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00
Kama wmefungia kipindi ca Take One haina shida wataanzisha kipindi kingine wakiite "ON SET"nawaza tu
AKILI ZA UGORO
 
TCRA ni wanafki sana, kwa nini wasikifungie kituo kama walivyofanya kwa vingine. Why Magic na radio 5 hawakufungia vipindi?? Yaan Clouds sijui wanachukuliwaje.
Shame on you! [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Kweli Tz. hakuna haki kabisa, Clouds na mambo yao ya hovyo hovyo ETI kipindi kinafungiwa! Ila Magic fm na Radio 5 wao walifungiwa kabisa stations zao! HAKUNA HAKI KABISA HAPA.
 
Kwanini Magic, na Radio Five zilifungiwa na Sio kufungiwa vipindi vilivyotoa maudhui yaliyowakera?


Kama ndivyo sheria inasema hivyo basi hata hapa wangefungia TV na sio Vipindi.



Sheria inasemaje? mtujuze
Tcra kwa clouds huwaambii kituu
 
Mbona wale wengine hawakufungiwa vipindi vyao? Kuna nini hapa
 
Zamaradi kwa vile kazaa na Ruge anajihisi hamna wa kumpangia maisha pale klauz anatukana wafanyakazi wenzie, anajisifia Ruge kamuweka mkononi ndo mana hata Joe Kusaga hawezi kumfukuza kazi.
Malkia wa mjengo hagusiki anawaona wenzie kama taka taka leo mrusha kipindi lazima alalee bar anampelekeshaga kama yuko na house girl wake
 
Back
Top Bottom